Utumaji wa message kwenye vipindi vya Redio na TV!!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utumaji wa message kwenye vipindi vya Redio na TV!!!!!

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Akili Unazo!, Jul 15, 2009.

 1. Akili Unazo!

  Akili Unazo! JF-Expert Member

  #1
  Jul 15, 2009
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 2,823
  Likes Received: 2,535
  Trophy Points: 280
  Kwa takribani kila siku nimekuwa nikisikiliza vipindi vya redio na TV kumekuwa na matangazo amabay yanamhitaji msikilizaji kutuma ujumbe kwa kutumia simu yake kupiga aidha kura au kumpongeza mtu fulani. Reference Cloud Fm na kipindi cha Ala za Roho,Leo tena, na vingine vingi.

  Hivi waku nani anayefaidika ni mtangazaji aliye buni hicho kipindi au kuna makataba maalumu ambao kituo hicho cha Redio au TV kinaingia na makampuni ya simu kwa ajili malipo.
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Jul 15, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  And worse enough, katika michezo hiyo sms moja hugharimu hadi tshs 1000/=! (refer kitu inaitwa VUNAVUNA TBC1)
  Naungana na Chaku, ni nani anayetajirishwa? ili tujue kama hela zile anapewa mtu mmoja au la ni ufisadi gani unaendeshwa hUko!!
   
 3. Kandambilimbili

  Kandambilimbili R I P

  #3
  Jul 15, 2009
  Joined: Nov 11, 2008
  Messages: 782
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mmelazimishwa KUPIGA???????

  Vunavuna unategemea utavuna nini kama sio kuchangiana hizo buku buku?????

  Vipindi vya kupiga simu havijaanza leo bibi/bwa chaku tangu zile enzi za radio one, na pia sidhani kama ni hapa TZ tu, kupiga simu ni njia moja wapo ya kundesha kipindi ili upate maoni tofauti tofauti, na pia kukifanya kipindi kuwa live, kuchangamsha, kupata wasikilizaji wengi, wadhamini kibao na HATIAMAYE mshiko wa nguvu kwa media husika.

  Uzuri hulazimishwi na garama za kutuma sms au kupiga ziko wazi so CHAGUA BEGA.......
   
 4. JosM

  JosM JF-Expert Member

  #4
  Jul 15, 2009
  Joined: Oct 11, 2008
  Messages: 684
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mkuu ni wizi mtupu,sasa hivi jamaa wa clouds FM wamekuja na wizi mwingine kuwa wanatafuta vipaji vya uimbaji,unachotakiwa ni kupiga namba flani hivi halafu ukisikia mlio (peep) unatakiwa uanze kuchana mistari yako.gharama yake ni tsh 1000/= kwa dakika.sio wizi kweli huu jamani?
   
 5. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #5
  Jul 15, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Sawa Kanda2, lakini swali la msingi bado hujalijibu kwa umakini.

  Umesema kwamba Media husika ndiyo inayofaidi, inakuwaje, wakati ile pesa inaingia kwenye kampuni husika la simu mteja aliko?

  Je hizo media wana utaratibu wa kwenda jioni kwenye makampuni ya simu kuchukua mahesabu ya kilichopatikana, au inakuwaje hii kamari?
  Weka sawa swali la msingi!
   
 6. Akili Unazo!

  Akili Unazo! JF-Expert Member

  #6
  Jul 15, 2009
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 2,823
  Likes Received: 2,535
  Trophy Points: 280
  Achana hicho kipindi kuna kingine cha kumtafuta eti Bibi bomba?yaani mpaka kero.
   
 7. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #7
  Jul 15, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  hehehehe hapo wakuu mnaliwa tu lakini tatizo la sisi wabongo tunapenda mtelemko na umaarufu wa bei chee utaona watu wanapiga licha ya kuliwa. Waache waendelee kuliwa tu.
   
 8. M

  Malyamungu JF-Expert Member

  #8
  Jul 15, 2009
  Joined: Jul 5, 2009
  Messages: 363
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Redio au TV zinapoenda kuomba udhamini kwenye makampuni ya simu huwa wana pata kwa kuutambua umuhimu wa Mdeia na pia wana mikataba yao ya kuvumbua product; kwa mfano; sales that is inclusive na isiyo na mipaka ya kibiashara mimi nafanya hivi nawe ufanye hivi. win/win solution. ni bomba sana.
   
 9. Dogo Tundu

  Dogo Tundu JF-Expert Member

  #9
  Jul 15, 2009
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 441
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  binafsi naungana na wadau kuhusu huu wizi wa akina nanilihii ila kwa staili nyingine, mi naona ni kama ufisadi vile?
  hivi kumbe na wazungu wezi eeh!
  sa kwanin wakubali huu ufisadi wa watu weusi.
   
 10. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #10
  Jul 15, 2009
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Kama kodi huwa inalipwa, kuna uwezekano sio kwa kiwango sahihi. Sioni kama ni rahisi kuwabana hawa; nadhani ndio maana utaratibu huu umeshamiri (ikiwa ni pamoja na bahati nasibu).
   
 11. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #11
  Jul 15, 2009
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145

  UONGO kabisa radio one kweli simu zilikuwa zapigwa BUT line ilikuwa toll free. Naikumbuka kabisa 996. Kama wanataka kipindi kuwa live basi walipie waendeshaji radio. Mtanzania anunue radio, anunulie betri redio yake, anunue simu, aweke credit kisha kishenzishenzi mumtege atumie credit zake hovyo hovyo na kubaki maskini. Hii si uhuru wa vyombo vya habari ila ni ushuru wa vyombo vya habari kwa wadanganyika. Acheni hizo ni matumizi mabaya ya fedha. Na ni wizi atiii.
   
 12. Kandambilimbili

  Kandambilimbili R I P

  #12
  Jul 22, 2009
  Joined: Nov 11, 2008
  Messages: 782
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  nimesema Media husika ndiyo inayofaidi kwenye talk show.

  hayo mengine siyajui na hayaniumizi kichwa kwani kupiga au kutopiga ni uamuzi wa mtu.
  ALL I KNOW is that pipo are in business so narudia CHAGUA BEGA....
   
Loading...