Kwanza nawapongeza UTPC kwa kupata fedha ambazo pia zitatumika kulipa waratibu. Hilo ni jambo jema sana hakika mnstahili pongezi.
Lakini kilichonileta hapa ni baada ya kupokea barua kutoka UTPC ikitoa maelekezo kwa sisi viongozi wa Klabu tujaze fomu za maelezo (kama inavyoonekana hapo chini) na bila ya hivyo waratibu hawatalipwa.
Sikatai kuhusu clearance form ni utaratibu mzuri lakini je kwanini utaratibu huu haukutumika kabla hawa waratibu hawajaondoka?
Je, ni kisasi mnataka kuwakomoa kwa kudai haki zao hadharani? Je, ni makasiriko kwakuwa baadhi ya mambo yenu yamewekwa hadharani? Kwanini msiwalipe wakaondoka na nyie muweke mikakat ya kusafisha hayo yaliyosemwa?
Sisi viongozi wa Klabu tunajua mazingira ya kazi kwa hawa waratibu wetu. Liko wazi kabisa. Na taarifa zilizopo ni kuwa baadhi ya waratibu waliokuwa wanadai pesa zao kwa nguvu hawana mahusiano mazuri na Klabu zao na kuna wenyeviti wamefurahia hili jambo ili tu waratibu wao wasipate haki. SIO SAWA NDUGU ZANGU. TUNAKOSEA.
Bodi ya Wakurugenzi mmeonesha wazi kuwa na kisasi. Acheni kuendelea kuchafua taasisi. Huu mnaofanya ni utoto. Lipeni waratibu bila masharti waendelee na maisha yao.
✌️✌️✌️