Victor Mlaki
JF-Expert Member
- May 1, 2016
- 5,510
- 6,244
Naomba uzi huu usihusishwe na Dini yoyote ile na wala usihamishwe na kupeleka kwenye jukwaa la Imani kwa sababu kuu mbili zifuatazo:-
(i) Utoaji ni suala la asili ya uumbaji, kila mtu anacho cha kutoa kwa mwingine.
(ii) Mtu yeyote anaweza kuwa mtoaji au kujifunza utoaji bila kujali imani yake.
Kuna mambo makubwa na ya ajabu yanayofanyika katika ulimwengu wa roho pale mtu anapofanya tendo la kutoa alichojaliwa na Mungu iwe ni sadaka msaada au kitu chochote kile.
Hakuna imani Duniani isiyosisitiza juu ya utoaji kutokana na ukweli kwamba kutoa siyo suala la kimwili tu ila suala linalofanya kazi kwa namna ya ajabu sana katika ulimwengu wa roho.
Suala la utoaji haliangalii wingi wa vitu alivyo navyo mtu ila linajikita katika utayari na utii ndiyo maana upo msemo usemao " Kutoa ni moyo na siyo utajiri". Kuwa na vitu au kutokuwa navyo hakumzuii mtu kutoa na wala hakutoi uhalali wa mtu kutokutoa kwa sababu kutoa siyo suala la kutaka tu ila ni Kanuni ya asili inayofanya kazi katika ulimwengu wa roho.
Mafaninikio yoyote tunayoyaona leo yawe ni ya mtu binafsi au ya jamii na hata Taifa yalianzia na utoaji na kadiri utoaji unavyoongezeka maradufu ndivyo na mafanikio yanavyoongezeka. Unaweza ukashangaa sana juu ya hili lakini ndivyo ilivyo katika ulimwengu wa roho.
Fuatilia kwa karibu utakuta hata matajiri wakubwa unaowaona leo kuna kitu walikitoa sana kiasi cha kujinyima wao ndiyo maana leo wapo walivyo. Kumbuka hata kutoa muda wako kwa uaminifu ni sadaka inayoweza kukuvusha mahali ambapo kwa hali ya kawaida usingeweza.
Utoaji ndiyo njia ya kupokea. Katika ulimwengu wa vitu unapotoa unaona kama umepoteza lakini ni jambo la ajabu na la tofauti sana linalofanyika katika ulimwengu wa roho kwa sababu huko kutoa ndiyo kupata. Hakuna hasara ya kutoa katika ulimwengu wa roho lakini kuna hasara kubwa ikiwa hatutakuwa watoaji.
Jambo la kushangaza zaidi katika ulimwengu wa roho ni kwamba kadiri unavyotoa kitu unachokihitaji zaidi ndivyo unavyojiweka katika kupata vitu vya thamani zaidi kuliko ulivyonavyo sasa.
Kwa kifupi ni kwamba mafanikio yanayoonekana kwa macho ya nyama ni zao la utoaji uliofanyika katika ulimwengu wa roho. Kadiri tunavyokuwa wachoyo wa kutoa tunavyovipata tunajifungia kupata zaidi kutoka kwenye chanzo cha vitu vyote katika ulimwengu wa roho.
Hakuna kujitetea katika utoaji kwa sababu utoaji ni miongoni mwa sheria za asili za kumsaidia mtu kupata. Hakuna Mwanadamu ambaye hana chochote cha kutoa hata yule anayeonekana kama hana chochote kabisa yaani fukara na choka mbaya bado Kanuni hii inataka atoe ili apate na inaamini kipo cha kutoa.
Leo watu wengi ni masikini siyo kwa sababu hatufanyi kazi kwa bidii la hasha! Tatizo ni kwamba hatuzingatii Kanuni za asili hususani suala la utoaji? Tunaamini vile tulivyovipata ni vyetu na ndiyo sisi jambo linalotufanya kuwa wa binafsi na kijifungia milango ya kupata zaidi kutoka katika ulimwengu wa roho.
Tafiti zinaonesha tendo la utoaji wa dhati la kawaida kuimarisha mfumo wa kinga wa Mwanadamu kwa kumfanya mtu kuzalisha :serotinin" inayomuwezesha mtu kujisikia vizuri lakini cha kustaajabisha zaidi ni kwamba tendo la utoaji siyo tu kumsaidia anayetendewa bali wale watazamao pia tendo hilo. Tafakari utoaji ukishamiri Duniani jamii ya wanadamu itakuwaje?
Umasikini tunaousikia upo Duniani kwa kiasi kikubwa unatokana na watu kukiuka Kanuni za asili za utoaji jambo linalofanya maisha kuwa magumu kwa watu wengine. Dunia ina wezo wa kutoa chakula na malazi kwa wakazi wake wote lakini kutokana na tabia a ubinafsi inayokiuka asili ya uumbaji leo tofauti kati ya wenye matajiri na masikini inasikitisha. Duniani ni mahali pazuri sana pa kuishi jamii ya wanadamu ikiwa wanapata Kanuni za asili.