Utitiri wa masomo tunayosoma mashuleni na mavyuoni, hatuyatumii makazini na hayatusaidii maishani

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,581
Hapa kwetu Tanzania, mashuleni na vyuoni tumekuwa tukisoma masomo mengi sana ya ajabu na magumuuuu ukiacha yale machache muhimu. Unamkuta mtu ana lundo la madaftari kwenye begi mpaka mtu anashindwa kuconcentrate kwenye yale machache. Anakuwa na " lugha gongana" kichwani, kazi inakuwa kukariri (kumeza) badala ya kuelewa. Wale wa vyuoni ndo maana bila "simbi, madesa" ni ngumu sana kutoboa elimu ya Tanzania, unaliwa kichwa (kufeli) mchana kweupe.

Mathalani shule ya msingi utakuta Kiswahili, hisabati, uraia, historia, jografia, sayansi kimu, dini, maarifa ya jamii, kiingereza, sayansi nk. Unakuta unamfundisha mtoto mambo ya Mtemi Mkwawa, Kinjekitile Ngombare Mwiru, Zama za mawe za kale nk.

Ukienda sekondari unakutana na Math, English, Kiswahili, Civics, History, Physics, Chemistry, geography, Biology, dini, Adv Math, Book keeping, Commerce nk.

Vyuo vikuu ndo kuna utitiri sana wa masomo,mengiiii mpk kero.

Ukienda kazini, unakuta masomo useful labda mawili au matatu tu. Mengine yote yanakuwa yamekuchosha tu na kukuzeesha. Ukiwa kazini unajikuta umeyasahau macourse yote within a very short time. Kwann chuoni mtu asifundidhwe masomo may be 5 au 6 tu from first year to final year? Ukiwa chuo first year unaletewa utitiri wa masomo mpk kero.


Hali hii inasababisha watu wanachoka haraka, wanakariri, wanashindwa kuconcetrate na vitu vichache na mwishowe wanasjindwa kwenda na maisha mtaani. Kichwa kinakuwa kimejaa maVolumes/manuals mpaka kinavuja.

Mtu akishajua lugha, halafu akabase kwenye masomo ma4 au ma5 tu, anafika mbali zaidi kiuelewa kuliko kubeba zigo la notes mpaka bega moja linakuwa chini lingine juu.
 
Ni kweli kwa mfano shule za msingi unasoma masomo tisa Lakini ukichunguza masomo hayo hayamsaidii mwanafunzi zaidi ya kumpa mzigo
 
Acheni ujinga! Masomo yote unayofundishwa shule na chuoni yanatumika, kinachotumika!. Mfano Mimi mwenyewe nimesoma masomo ya kihandisi pamoja na ujasiliamali pale mlimani, lakini cha ajabu, somo LA ujasiliamali ndilo lililonitoa kimaisha hadi nimekuwa mfanyabiashara mkubwa.

Masomo yote yanatumika sema ww hujui! Unaweza soma hadi level ya uprofesa lakini ukaja tumia somo moja tu likakutoa, mengine yanabaki akiba.

TATIZO KUBWA LA WATANZANIA NI KUTOKUJUA KARAMA ZETU; kuna rafiki yangu kasoma divinity/bible knowledge secondary halafu chuo akasomea uhandisi lakini baada ya kugraduate kaamua kuwa MCHUNGAJI. So katumia somo la divinity kuishi
 
Binafsi naona yote yanasaidia.

Dunia ya sasa yenyekubadilikabadilika mtu mwenye kujifunga sehemu moja.
Basics zile karibu zote zinamaana sana kwa kumjengea flexibility na adaptability muhusika kwa maarifa na field yoyote mpya.

mfano. Primary Soma general kila kitu,

Secondary O-Level. Agriculture kama Somo la lazima, Soma pia Masomo ya biashara hadi form 2, ili ukifika form three unaweza kuamaua pa kwenda science,art,au biashara lakini unatips za kuanzia.

Binafsi ninaona yanamaana yote
 
Masomo yote uliyosoma tangu shule ya msingi mpaka chuo yanasaidia, tatizo watu wanataka mpaka aone directly kwenye eneo lake la kazi lile somo linatumika. Kwanza kwa kusoma masomo yote tu yale uwezo wetu wa kufikiri umeongezeka na ndio maana humu kuna watu huwa wana lugha ya kejeli haswa kwa mtu akitoa point ambazo hazijakaa sawa aka PUMBA utasikia "nenda shule which means shule ya aina yoyote bila kujali aina ya masomo", mwanamuziki au mwanamtindo akifanya mambo ya ajabu pamoja na kwamba ana fedha utasikia "angekuwa na shule kubwa huyu mambo yake yangekuwa safi zaidi.

Kwa ujumla masomo tuliyosoma shuleni yanatusaidia kupambana na changamoto zinazotuzunguuka bila watu kugundua kwamba wamefika hapo kutokana na hayo hayo masomo na ndio maana kadri unavyokwenda juu mtu unakuwa unajikita katika masomo au taaluma flani
 
Binafsi hesabu za "integration" na "differentiation" zinasaidia sana kupambamua mambo kwa haraka huku mitaani. ..
 
Back
Top Bottom