GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 56,805
- 109,483
Jpm anampenda Mungu. Na hiki ndicho kinampa sifa kubwa Tanzania na duniani kwa ujumla
I like this! Kama taarifa ni ya kweli, maana siku hizi, Mkuu, sikuelewi elewi haha haaa! (Take it ease, Mkuu!)Mwishoni kabisa Wote 'walisikika' wakisema kuwa laiti kungekuwa kuna uwezekano wa 'Kukopana' Marais hata kwa muda fulani tu basi kwa 'Taabu' ambazo wanazipitia sasa 'Waganda' na Maisha magumu 'waliyonayo' tokea Janga hili la CORONA lianze huku 'wakizuiwa' Kufanya Shughuli zao mbalimbali za 'Kiuchumi' basi wangetuomba Watanzania 'tuwakopeshe' Rais wetu huyu Dkt. Magufuli.
I like this..! Kama taarifa ni ya kweli, maana siku hizi, Mkuu, sikuelewi elewi haha haaa! (Take it ease, Mkuu!)
Let them be very careful, otherwise they may get what they are wishing for!
Jpm anampenda Mungu. Na hiki ndicho kinampa sifa kubwa Tanzania na duniani kwa ujumla
Mungu yupi? Hakuna mtu anayempenda Mungu wa mbinguni anayeweza kutamani wale wanaoishi kama malaika waishi kama mashetani. Halafu Mungu anaweza kumtumia mtu yeyote hata kama ni mbaya kama shatani. Mungu alimtumia mfalme Koreshi mpagani kuwaruhusu Israeli kwenda kujenga upya kuta za Yerusalemu na Hekalu.
Huko Uganda nakumbuka kuna jamaa alikuwa anaitwa Kibwetere, alichokifanya kwenye nyumba yake ya ibada kunaonyesha akili za Waganda. Hivyo sishangai baadhi ya Waganda wachache wakija na porojo hizi. Hata hivyo nilimpongeza Magufuli sio kwa kupambana na Corona maana hajawahi kupambana nayo, bali kutokutuweka lockdown maana nisingekubaliana naye, hatimaye ningeonekana napinga kila kitu. Maamuzi haya ni baadhi ya maamuzi machache sana niliyowahi kukubaliana na Magufuli toka awe rais.
Siku hizi nakupenda na naanza kukuelewa hasa katika 'Michango' yako hapa JF kwani hufanyi 'Criticism' kwa JPM bali unafanya 'Critique' tu. Heko!!
aende huko uganda akawe rais wao sisi hatumtaki.
Kwahiyo Wananchi wa Uganda na Viongozi wote wa 'Dini' wa Uganda hawayaoni 'Mema' au 'Mazuri' ya Rais JPM hadi Wewe 'Umchukie' namna hii?
waganda wako frustrated, Wamemchoka Museveni wanaona Magufuli ana nafuu kwao, lakini hiyo haimaanishi kuwa Magufuli ni raisi mzuri. Waliovunjiwa nyumba zao Mbezi Kimara wanakubaliana na mimi
Sijasema nimemchukia ila nimekusaidia kujua kwamba kutumiwa na Mungu siyo sababu ya mtu kuwa mcha Mungu. Hata hivyo waganda siyo Watanzania. Biblia inasema asiyewajali wa nyumbani kwake ni mbaya kuliko asiyeamini. Inasaidia nini kusifiwa na Waganda wakati Watanzania wengi wamehudhunishwa?