King Nkondo
JF-Expert Member
- Jan 1, 2023
- 1,268
- 1,860
Wewe mchumi tuambie unataka afanye nini?
Hakuna mamlaka ya kufanya hayo na hakuna utaratib wa utawala wa CCM wa kufatilia na kuchukulia hatua mamb hayo!! Bongo ni kanyaga twende ✔️Mamlaka husika naomba iingilie kati ijiridhishe kama kweli vyeti ya Udaktari wa Uchumi vya Dk. Mwigulu Nchemba ni vya kwake kweli au laa? ili kulisuru Taifa.
Taifa linakoelekea sasa ni kubaya na kwa mzaha huu unaondelea wa Waziri wa Fedha kuna siku Serikali itakuja kushindwa kulipa mishahara hata watumishi wake.
Fedha imeshuka thamani kwa spidi kubwa, mfumko wa bei umepanda mara dufu, biashara za nje zimekwama nchi haina Dola za Marekani, kama hayo yote yanaendelea chini ya Mwigulu Serikali itakusanyaje kodi maana biashara nyingi zitakufa.
Deni la Taifa litaongezeka mara dufu na fedha zote zinazokusanywa na nchi zitakwenda kulipa deni na huku huduma za kijamii zitaendelea kudorora kwa kiasi kikubwa.
Mimi nimelala na kuamka usiku na kuwaza hivi kweli kwa uwezo huu wa Mwigulu hiyo elimu ya udaktari wa uchumi ni yake kweli au vyeti ndiyo vina jina lake? Tusilichukulie mzaha hili jambo watanzania litatutafuna wote uchumi unakwenda kuanguka kwa kiwango kikubwa sana.
Duh 🙄Yeye ameagiza mapasi 6 mapya ya Ester
Masahihisho : siyo 6 ni 60Yeye ameagiza mapasi 6 mapya ya Ester
Acha roho mbaya Kwa hiyo ulitaka akondeane?Boss wake ananenepa tu kwa raha zake
Du jamaa anaishi kwenye dunia akeMasahihisho : siyo 6 ni 60