Uthibitisho: Mathias Kipara mgombea UVCCM kafoji umri

Uthibitisho: Mathias Kipara mgombea UVCCM kafoji umri

Mpaka sasa tunashindwa kuelewa kipi ni kipi, Mgombea uenyekiti UvCCM kwa mara nyingine tena vyeti vimeonekana vikionyesha amezaliwa 1970. Kama inavyoonekana hapa chini. Hii movie hii
IMG_1511936690.201332.jpg
 
Hivi umri wa kuachwa kuitwa kijana unaisha mtu akifikisha miaka mingapi?
 
Majambazi nyie nendeni na habari zenu za kinafiki za lumumba


Swissme
 
Inanikumbusha issue ya Masauni, Huyu Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani

Ili akidhi vigezo vya kugombea UVCcm alitengeneza gumashi kuwa kazaliwa 1980 lakin akasahu kurekebisha Cheti chake cha Shule ya Msingi kinachoonesha alianza darasa la kwanza 1979!

Alichaguliwa baadae ndo ukajulikana akapigwa Mtama na kina Ridhwaan

Jk akapiga Kijembe Eti Jamaa kaanza Shule Mwaka Mmoja kabla hajazaliwa!
 
Ndio michezo ya CCM hiyo, haijaanza leo. Ukighushi vyeti, umri unazawadiwa madaraka makubwa zaidi siku za usoni (Mf Bashite, Masauni).
 
Tuwe wakweli kabisa, kama Kipala amesema ana miaka 29, huo ni uongo wa wazi. Jamaa tumehitimu naye pale UDSM mwaka 2011alikuwa mbabu tu,iweje hadi leo miaka sita baadae aje kuwa na miaka 29?. Sema ndo hivyo tena kwa vile ni mzee wa kitengo kule kwa wazee wa kaunda suti na miwani nyeusi.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Stori zako hazipo tofauti na Mange makengeza

Umri ndio Tatizo lako!

Masauni alikuwa Mwenyekt wa UV CCM Taifa na alitumbuliwa kwa kughushi Umri!
Uliza Wakubwa zako wakupe taarifa zaid
 
Acha kubashili kijana.....Ila tambua kama ni mzee basi ndio chaguo la Vijana wa UVCCM.

Kila kijana ana maamuzi yake binafsi mbona walioingizwa kwenye kinyang’anyiro hiko karibia wate vibabu inakuwaje mumvute shati huyu pekee....

Pambanen na vyama vyenu ya UVCCM waachieni UVCCM.
Mkuu mimi sikatai Kipala kuchaguliwa na UVCCM, kwa utendaji ni mtendaji mzuri sana na nina imani ataiongoza vyema UVCCM kama atachaguliwa lakini hilo haliondoi ukweli kwamba hana miaka 29. Na kwa jinsi alivyo mtu wa system hakuna atakayemgusa na ndiye atakayepata hiyo nafasi liwe jua iwe mvua.
 
Tuwe wakweli kabisa, kama Kipala amesema ana miaka 29, huo ni uongo wa wazi. Jamaa tumehitimu naye pale UDSM mwaka 2011alikuwa mbabu tu,iweje hadi leo miaka sita baadae aje kuwa na miaka 29?. Sema ndo hivyo tena kwa vile ni mzee wa kitengo kule kwa wazee wa kaunda suti na miwani nyeusi.

Wema Sepetu mpaka Leo hajafikisha Miaka 30!

Kwa Miaka Kama mitano mfululizo alikuwa anafanya birthday ya kutimiza Miaka 26

Kidoti mpaka Leo Yule Mdogo wake Bwabwa kishamzidi umri , maana wa kwake haubadiliki!
 
Back
Top Bottom