Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,774
Wengi wanamlaumu JK juu ya kumteua Prof. Mwandosya kuwa Waziri asiye na Wizara maalum. Nadhani upembuzi huo si sahihi. Mie nadhani JK amemheshimu sana Mwandosya. Kumbukeni Mwandosya bado hajarejesha afya yake vema, na hivyo JK hajampa Wizara kamili ambayo ingehitaji nguvu nyingi. Wengi tungeishia kusema Mwandosya bado mgonjwa kwa nini apewe Wizara kubwa wakati Watanzania wengine wapo.
Alichofanya JK ni sawa na kuamua kumpumzisha Mwandosya huku bado akimweka karibu ili asiwe mbali na yanayojiri katika Baraza la Mawaziri, ikimaanisha bado anahitaji busara za Mwandosya na anaamini atapona kabisa na kuendelea na kazi. Kumbukeni kuna wakati Nyerere alimpumzisha Sokoine akiwa mgonjwa kwa karibu kipindi cha miaka miwili. Sokoine alipopona kabisa ndipo Nyerere akamrudishia Uwaziri Mkuu. JK angempumzisha Mwandosya kwa namna hiyo watu ndio mngesema hata zaidi!
In fact JK kumfanya Mwandosya Waziri asiye na Wizara maalum Mwandosya atakuwa katika ofisi ya Raisi, ikimaanisha atakuwa karibu zaidi na JK kushauriana mambo yanayohusu Wizara yeyote ile. Mie binafsi ninaheshimu sana utendaji wa Mwandosya, na kwa hili alilofanya JK kwa Mwandosya nimeona JK katumia busara sana. Fikirieni kwa makini.
Labda cha kumsihi JK ni kwamba sasa atumie busara na umakini wa Mwandosya kwa namna kubwa hata zaidi kwa kuwa wako ofisi moja; Ofisi ya Raisi.