Uteuzi wa JK wa Mwandosya ni wa busara na hekima sana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uteuzi wa JK wa Mwandosya ni wa busara na hekima sana

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Synthesizer, May 7, 2012.

 1. Synthesizer

  Synthesizer JF-Expert Member

  #1
  May 7, 2012
  Joined: Feb 15, 2010
  Messages: 4,334
  Likes Received: 3,127
  Trophy Points: 280
  Wengi wanamlaumu JK juu ya kumteua Prof. Mwandosya kuwa Waziri asiye na Wizara maalum. Nadhani upembuzi huo si sahihi. Mie nadhani JK amemheshimu sana Mwandosya. Kumbukeni Mwandosya bado hajarejesha afya yake vema, na hivyo JK hajampa Wizara kamili ambayo ingehitaji nguvu nyingi. Wengi tungeishia kusema Mwandosya bado mgonjwa kwa nini apewe Wizara kubwa wakati Watanzania wengine wapo.

  Alichofanya JK ni sawa na kuamua kumpumzisha Mwandosya huku bado akimweka karibu ili asiwe mbali na yanayojiri katika Baraza la Mawaziri, ikimaanisha bado anahitaji busara za Mwandosya na anaamini atapona kabisa na kuendelea na kazi. Kumbukeni kuna wakati Nyerere alimpumzisha Sokoine akiwa mgonjwa kwa karibu kipindi cha miaka miwili. Sokoine alipopona kabisa ndipo Nyerere akamrudishia Uwaziri Mkuu. JK angempumzisha Mwandosya kwa namna hiyo watu ndio mngesema hata zaidi!

  In fact JK kumfanya Mwandosya Waziri asiye na Wizara maalum Mwandosya atakuwa katika ofisi ya Raisi, ikimaanisha atakuwa karibu zaidi na JK kushauriana mambo yanayohusu Wizara yeyote ile. Mie binafsi ninaheshimu sana utendaji wa Mwandosya, na kwa hili alilofanya JK kwa Mwandosya nimeona JK katumia busara sana. Fikirieni kwa makini.

  Labda cha kumsihi JK ni kwamba sasa atumie busara na umakini wa Mwandosya kwa namna kubwa hata zaidi kwa kuwa wako ofisi moja; Ofisi ya Raisi.
   
 2. Ernesto Che

  Ernesto Che JF-Expert Member

  #2
  May 7, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,117
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Bahati mbaya mtazamo wako umeangukia katika kulipana fadhila na kuheshimiana kuliko kujali maslahi ya taifa. Kila siku kilio chetu ni ukubwa wa baraza la mawaziri, haiingii akilini kuweka mtu asiye na wizara maalum anawajibika wizara ipi? zote? Waziri Mkuu anakaa wapi?
  Nikiwa mzalendo wa kweli nafahamu nchi yangu imeyumba kiuchumi si wakati kupeana vyeo hovyo halafu kuzidisha matumizi ya serikali, hapo Rais kachemsha tena sana.
  Busara za Mwandosya si lazima awe waziri anaweza kuzipata hata bila kumpa uwaziri, ni mwana CCM kuna vikao vya chama pia. Kifupi JK anaogopa kivuli chake kwa kutaka kujisafisha na watu wa Mbeya ndo maana kafanya hivyo, still wrong move.
   
 3. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #3
  May 7, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Lakini pia Mwandosya ni mtaji wa kisiasa. Kikwete mwenyewe anajua kama si mizengwe asingeweza kumshinda 2005. Hdi hivi sasa bado mwandosya ana kundi kubwa nyuma yake ingawa hana makeke kama walivyo wanasiasa wengine
   
 4. Synthesizer

  Synthesizer JF-Expert Member

  #4
  May 7, 2012
  Joined: Feb 15, 2010
  Messages: 4,334
  Likes Received: 3,127
  Trophy Points: 280
  Labda uanze kwa kuniambia ni fadhira zipi JK atakuwa analipa kwa Mwandosya. Na kuhusu maslahi ya taifa, hilo ndilo usiloelewa; ikiwa tunalalamika kwamba tuna viongozi wengi ambao hawajali maslahi ya taifa, na wapo wachache wachapa kazi kama kina Mwandosya, kwa nini tuwatupe kwa kuwa tu kwa kuwa kwa kipindi fulani afya yao haikukaa sawa?

  Niliwahi kuuliza swali, kwamba wengi wetu humu ndani ni wafanyakazi; nani kati yetu aliyemchapa kazi hodari kwa miaka mingi angeona ni haki kuachishwa kazi kwa kuwa amekuwa mgonjwa kwa miezi kadhaa badala ya angalau kupewa muda wa kupona sawa sawa bila kuachishwa kazi?
   
 5. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #5
  May 7, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Mwandosya ana kundi la wazee wa Mbeya wale waliokuja kumtetea kwa Mkapa...
   
 6. pandian

  pandian Member

  #6
  May 7, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 37
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  No way! Huwezi endesha nchi kwa kulipa fadhila kama unavodai hapa. Wafanyakazi wangapi ktk seriakli hii na kwa ngazi mbali mbali hulazimika ama hulazimishwa kupumzika pale ambapo afya zao zinapoonekana kuyumba? This is done only by African govts ambao kwa kawaida, we are always, not serious!
   
 7. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #7
  May 7, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  J.K & the family ndo wanamlipa Mwandosya mshahara?
   
 8. M

  Mboko JF-Expert Member

  #8
  May 7, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 1,067
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Sasa huyu ndio wale wale duuh huyu Gamba kweli kweli lakini simlaumu sana kwani yuko kazini.Magamba wote wana akili sawa tu hakuna cha ajabu huyu alivyosema kwani moja kwa moja tunafahamu za Magamba ni kulindana so kutokana na hii ni kwamba huyu jamaa kazihirisha ule ukweli uliopo ndani ya Magamba Kulindana kulindana unataka niambia akiwa nje kama mbunge wa kawaida hawezi kumshauri Kikwete????Usiwe na mawazo mgando wewe raia wake up man kumbuka hata kama mtu sio Mbunge au waziri anaweza pia kutoa mchango wake na ukahesabiwa sema kwa Chama Cha Magamba hili halipo kwanza kabisa ili mchango wako wa mawazo ukubalike lazima uwe na mijipesa na wao hata hawajali umeuwa binadamu kama wengi wanavyouuwa ndugu zetu wenye matatizo ya ngozi wao hawajali hayo na pia sishangai kwani wao ndio wako mstari wa mbele kuwamaliza hawa ndugu zetu,Mungu atawalaani nyie subirini kwani mpaka sasa yanaonekana.
   
 9. P

  Paul S.S Verified User

  #9
  May 7, 2012
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Kama anahitaji busara zake angemfanya mshauri wake tu ingetosha nadhani
  Hili ni tatizo la kuingiza kujuana zaidi kwenye kazi kuliko uhalisia
  Inaonekana ni kama dhambi kutompa uwaziri kwasababu afya imeleta shida
   
 10. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #10
  May 7, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,819
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  Tuwe na subira, ipo siku umma utakuja kugundua nini kilimsibu our renowned Professor. Nina mpongeza sana kwa busara zake na hekima nyingi za kuchagua kutozungumzia afya yake ovyo ovyo. Otherwise I personally believe kwamba uteuzi wake kuwa a minister without portfolio was inevitable; upon a cost-benefit analysis, handling the repercussions za kumwacha ni more costly. Otherwise mungu atamjalia na kumrudisha katika afya yake ya kawaida kwani tunamhitaji sana kama taifa
   
 11. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #11
  May 7, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  kuna kazi na kazi! Kwanza J.K hajampa Mwandosya kazi yoyote amempa mshahara wa bure.
   
 12. M

  Mboko JF-Expert Member

  #12
  May 7, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 1,067
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Sasa huyu ndio wale wale duuh huyu Gamba kweli kweli lakini simlaumu sana kwani yuko kazini.Magamba wote wana akili sawa tu hakuna cha ajabu huyu alivyosema kwani moja kwa moja tunafahamu za Magamba ni kulindana so kutokana na hii ni kwamba huyu jamaa kazihirisha ule ukweli uliopo ndani ya Magamba Kulindana kulindana unataka niambia akiwa nje kama mbunge wa kawaida hawezi kumshauri Kikwete????Usiwe na mawazo mgando wewe raia wake up man kumbuka hata kama mtu sio Mbunge au waziri anaweza pia kutoa mchango wake na ukahesabiwa sema kwa Chama Cha Magamba hili halipo kwanza kabisa ili mchango wako wa mawazo ukubalike lazima uwe na mijipesa na wao hata hawajali umeuwa binadamu kama wengi wanavyouuwa ndugu zetu wenye matatizo ya ngozi wao hawajali hayo na pia sishangai kwani wao ndio wako mstari wa mbele kuwamaliza hawa ndugu zetu,Mungu atawalaani nyie subirini kwani mpaka sasa yanaonekana.
   
 13. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #13
  May 7, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Nimekusoma...

  Kwa kifupi Prof hakutaka kutumia afya yake kama mtaji wa kisiasa. Sio opportunist kama Mwakyembe and Co
   
 14. S

  Shaabukda Member

  #14
  May 7, 2012
  Joined: Apr 18, 2012
  Messages: 96
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hivi isingekuwa busara zaidi kwa mh Mwandosya kuomba apumzishwe? Hii ingemrahisishia sana kazi JK. Hili la waziri asiye na wizara maalumu naona ni kuongeza mzigo tu kwa serikali ombaomba!
   
 15. pandian

  pandian Member

  #15
  May 7, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 37
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Waziri asiye na Wizara Maalum dunia ya leo? Ama kwel mna mawazo mgando na fikra zenu zimegota. Najua hta Mwandosya mwenyewe anapata tabu sana na tiltle hii aliyopewa. Chukulia hata anapotoka nyumban kwake anaagaje; Jaman nakwenda ofcni. Ofic ipi hata yeye hajui
   
 16. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #16
  May 7, 2012
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Ni sawa uonavyo wewe,ila ukweli ni kwamba Kikwete amem-retain Mwandosya kwa ajili ya maslahi ya chama chake.Ikumbukwe kwamba mkoa wa Mbeya ni miongoni mwa mikoa ambayo imekuwa shubiri kwa CCM.So kuwaengua Mwandosya na Mwakyembe ingezidi kuiweka pagumu CCM kwenye uchaguzi wa 2015.Lakini pia alichofanya Kikwete ni kama kupulizia baada ya kuuma.Nadhani ninaeleweka.Ni kuficha makucha.
   
 17. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #17
  May 7, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Hapa unachanganya chama na serikali. Hivi ni vitu viwili tofauti na ni makosa kuweka mbele maslahi ya chama serikalini. Huyu Mwandosya ni mgonjwa na kuna vijana ambao wapo vizuri na wangeweza kuchapa kazi vema kwa kuwa wananguvu. Kuhusu waziri asiyekuwa na wizara kwangu mimi ni ufisadi tu. Hakuna kitu kama hicho kwenye dunia ya leo. Atalipwa kwa kazi gani? Atakuwa na bajeti ya kazi gani? Itafanyiwaje ukaguzi! Kama rais aliona anahitaji ushauri na busara zake angemchagua kuwa mshauri wake na sio waziri maana anaigharimu serikari bila sababu za msingi.
   
 18. S

  Shaabukda Member

  #18
  May 7, 2012
  Joined: Apr 18, 2012
  Messages: 96
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hivi isingekuwa busara na uzalendo zaidi zaidi kwa Mh Mwandosya kumuomba Rais ampumzishe? Hii ingemrahisishia sana kazi JK. Au inawezekana amefanya hivyo lakini Rais akakataa? Hili la waziri asiye na wizara maalumu naona ni kuongeza mzigo tu kwa serikali ombaomba!
   
 19. Memo

  Memo JF-Expert Member

  #19
  May 7, 2012
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 2,147
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  More costly kwa nani??!
  Kwa chama au kwa maslahi ya nchi!?
   
 20. Synthesizer

  Synthesizer JF-Expert Member

  #20
  May 7, 2012
  Joined: Feb 15, 2010
  Messages: 4,334
  Likes Received: 3,127
  Trophy Points: 280
  Unajuaje kwamba hakomba apumzishwe akaambiwa bado unaweza kuwa na manufaa kwa nchi? Labda uwaulize wale ambao wamekuwa mawaziri, kwamba je, Mwandosya amekuwa na mchango wowote wa busara katika vikao vya Baraza la Mawaziri? Na wakikuambia ndio, jiulize ni jinsi gani JK angeweza kuendelea kutumia busara za Mwandosya katika vikao vya Baraza la Mawaziri katika mazingira kama haya. Kumbuka hata manaibu waziri hawaingii kwenye vikao vya Baraza la Mawaziri.

  Mie binafsi nimewahi kushiriki vikao ambavyo Mwandosya amekuwapo, hapa nchini na nje ya nchi. Na nakuhakikishia kwamba that man bwana ana uwezo wa kupembenua pumba akatoa mbegu kwa namna ya pekee kabisa.

  Kuna waziri mmoja aliwahi kusema kuna baadhi ya mawaziri hawampendi Mwandosya kwa kuwa akitoa point zake kwenye vikao vya Baraza la mawaziri anafanya waonekane ni watupu mno!
   
Loading...