Uteuzi wa JK wa Mwandosya ni wa busara na hekima sana

Kumtoa kwenye wizara ya maji na kumpa wizara isiyokuwa na kazi maalum ni kummaliza kabisa hasa kwa msongo wa mawazo bora angemtoa kabisa akampa hizo kazi za ushauri ambazo zingeendana na afya yake kwa wakati huu mpaka atakapokuwa fit. kwa tabia za Jk kufanya hivyo ni sawa na kumnyonyoa kuku kabla hujamchinja..... ngoja tusubiri
 
hahahahahahahaha,waziri asiyekuwa na wizara maalum akiiingia ofisini asubuhi atakuwa anafanya kazi gani????TUSEME UKWELI KIKWETE ANAOGOPA BAKORA ZA RUNGWE KWA MWANDOSYA NA MBEYA KWA UJUMLA,HASA AKIKUMBUKA ALIVYOTUMIA KUNDI LA WANAMTANDAO KUMHARIBIA MWANDOSYA INABIDI AFANYE TU KINAFIKI,HAKUNA KITU HAPO NI ULAJI TU.
 
Psychologically itamsaidia prof. Mwandosya kurecover na nakubaliana kabisa na waliohusisha uteuzi huu na political reasons coz kwa pande zile za Nyanda za Juu Kusini, hiki ni kichwa hivyo kacheza Siasa vizuri hapa JK Lakini yote juu ya yote haisaidii kitu hii kwani Magamba ndo ivyoo wanapumulia machine sasa.
 
Sythizer unachoongea na kutaka kutueleza ni nini? Taifa lipo kwenye vita ya kupigana na umasikini hatuhitaji kupata stori zako zisizokuwa na mashiko eti fulani awe karibu na Rais au la. Mgonjwa anaugulia hospt anu nyumbani akipona anaweza kurudishwa kama kuna ulazima. Tunahitaji kupunguza gharama za uendeshaji wa serkali siyo kugawa mishahara na marupurupu kwa raslimali hewa. Mbadilike siyo wakati wa kufanya hayo sasa Movement for Change (M4C). Badilika kabla ya kupambazuka. Kama huna thread yenye mashiko ni bora kulala usipotezee watu muda
 
Wanayomchukia Mwandosya poleni.Kazi amepewa na mshahara atapata.JK angeona hafai angemuondoa serikalini.
Ameumwa ndio hakupenda iwe hivyo lakini yuko njiani kupona.Ameumwa kimwili lakini akili ziko pale pale.
Mwandosya amekua WAZIRI miaka 12 na mchango wake nchini umeonekana.Wizara maalum aliyopewa sawa kawaida wanawapa watu kwa heshima kama Mz Kawawa na Mz Kingunge, lakini kwa Mwandosya navyomjua atafanya kazi yoyote ambaye Rais atamtuma.Uwezo anao na akili pia anazo.JK angemundoa watu wangelalamika eti sio muungwana sasa amempa kazi bado wengine mnalalmika, hivi kazi hamna??
 
Back
Top Bottom