UTEUZI: Jaffar Haniu ateuliwa kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais (Ikulu); amrithi Gerson Msigwa

State house ndio government yenyewe
Mbona ni rahis. Hivi ni vyeo viwili tofaut na distinct maana mmoja ni 'Goverment spokesperson' na mwingine ni 'State House spokesperson'. Sioni namna yoyote ambayo hivyi vyeo viwili vikifanana wala vikingiliana kimajukumu. Maana mmoja anaripoti kuhusu serikali kwa ujumla wake kwa mantiki ya wizara na taasisi zote za serikali. Na huku kwingine huyu anareport habari zinazomhusu Rais na ikulu yake tumchukulie kama personal press secretary wa Rais na ikulu.
Kwenye coordinated government yeyote ile duniani hivi ni vyeo viwili tofauti kabisa sema kipindi cha mwendazake kwa sababu ya ubabe wake na lack of coordination ya serikali yake ndo maana ilifika kipindi Msigwa na Abasi wakawa wanaingiliana majukumu kila mtu hajui scope au JD ya kazi yake inakomea wapi na hukuna mtu aliyewahi kujitokeza na kulisemea hili maana ilikua ni mwendo wa 'one man show'. Hakuwepo kiumbe yoyote serikalini mwenye uwezo wa kujitoteza na kukosoa mwenendo wa utawala wa JPM. Ni sasa hivi tu ambapo hata wale wafia dini ndipo wameanza kuongea ata huko bungeni
 
Msigwa byebye, nadhani hii ndio itakuwa taarifa yako ya mwisho kabisa kuitoa kama Mkurugenzi Wa Mawasiliano Ikulu.
Lakini ndio kapewa cheo kikubwa,kuwa msemaji wa serikali ni zaidi ya kuwa mkurugenzi wa habari ikulu mkuu. Msigwa atakuwepo sana.
 
Rais Ni Samia Suluhu
Chief Secretary Ni Katanga
Katibu Wa Rais Ni Juma Suleiman
Chief of Protocol Ni Yusuph Mndolwa
DPC Wa Rais Ni Jaffary Haniu

Katika Wasaidizi Binafsi Katika Ofisi Ya Rais Ikulu (OBR) Ambao Jumla Ni 8, Wasaidizi 6 ni Waislamu na Wasaidizi 2 Tu Ndio Wakristo, Ambao Ni Felister Mndeme Maendeleo Ya Jamii na Nehemiah Mandia Sheria
Hawa wote ni Watanzania?? Au kuna Mrundi hapo??
 
Achana na civics ya sekondari, huko ni nadharia tu, Hapa Tanzania ikulu ndio serikali yenyewe.
Hapana. State house sio goverment. Sitaki kutoa lugha mbaya au kukukosea heshima mkuu ila ata watoto wa sekondari au primary wanaosoma somo la 'civics' ukienda kuwauliza tofauti ya 'ikulu' na 'serikali' watakupa majibu mujarabu.
 
Achana na civics ya sekondari, huko ni nadharia tu, Hapa Tanzania ikulu ndio serikali yenyewe.
Mwendazake aliiharibu sana hii nchi. Hakuna mgawanyo wa majukumu mpaka imefikia hatua ya watu kuona ikulu na serikali ni kitu kimoja. Siku zote aliisigina Katiba na kudai kuwa muhimili wake umejichimbia chini zaid maana yake yeye ndiye kila kitu. Angeendelea kubaki kwa miaka ya mbele zaidi watu wangeenda kusahau kama bunge na mahakama ni mihimili inayojitegemea.
Hakika huyu mama ana kazi kubwa sana ya kurudisha mambo katika uhalisia wake na kuongoza nchi katika misingi ya katiba na demokrasia maana tulikua tunaelekea pabaya sana kama taifa.
 
Back
Top Bottom