Utekaji (kidnapping): Chatu anayeitafuna Tanzania

UTEKAJI (KIDNAPPING): CHATU ANAYEITAFUNA TANZANIA:

Nianze kwa msemo wa Kiswahili kuwa "Chatu ukimfuga ili ameze watu, ipo siku atameza watoto wako kama si wewe mwenyewe".

Tukio la kutekwa bilionea kijana zaidi Barani Afrika, Mtanzania Mo DEWJI haikuchukua hata dakika 10 Taifa zima kurindima kwa taharuki, hofu na mashaka. Kutekwa kwa Mo DEWJI kunanifumbua macho kuwa kumbe Tanzania maisha kuna baadhi ya watu maisha yanathaminiwa zaidi kuliko ya wengine. Tofauti na ilivyo kwa Marekani ambapo kila maisha ya Mmarekani awe ni tajiri, masikini, mwanasiasa, nk maisha yao huthaminiwa na kulindwa kwa uzito ule ule.

Kwa nini nasema kuwa Tanzania ni sawa na animal farm (shamba la wanyama) ambapo wanyama wote ni sawa lakini wanyama wengine ni muhimu zaidi ya wengine (all animals are equal but some are more equal than others).

Jinanamizi la watu kutekwa na kupotea lilipoanza kuripotiwa familia za wahusika zilitelekezwa wahangaike wenyewe. Kupotea kwa msaidizi wa Freeman Mbowe anayeitwa Ben-Rabiu Wa Saanane kulishirikisha hili. Haikuishia tu hapo akapotea Mwandishi Azory Gwanda bado Taifa likapuuza tu, waliohangaika ni familia na marafiki zao. Serikali haikujishughulisha. Tumejijengea utaratibu wa kupuuza taarifa hizi, tunapuuza maisha ya watu. Tunathamini maisha ya mtu kwa kuangalia kuwa ana nini? Hii ni dhambi kubwa ni laana tena laana sumaka!

Kuna msanii aliwahi kuomba "Kutekana-tekana ni uhuni wa kishamba", lakini hatukufika hapa kwa bahati mbaya, la hasha! Tujikukumbushe kidogo tu tabia za kupuuza maisha ya Watanganyika kwa misingi ya kujenga tu kuwa huyu ni wa kwetu yule ni wao, huyu ana kitu na yule Hana, ni UJINGA tu...

1. Mauaji ya kinyama ya Kamanda Alphonce C. Mawazo. Mawazo waliuawa na mwili wake kuokotwa huko Geita. Sote tunakumbuka jinsi ambavyo jambo hili lilipuuzwa. Hata kibali cha eneo la kumuaga tu pale kiwanja cha Furahisha kilipatikana kwa mbinde mahakamani. Alipuuzwa, serikali ikasema inafanya upelelezi na uchunguzi kubaini waliomuua. Hadi leo ni kimya tu. Damu ya Mawazo inalia kwa sauti, amekataa kupumzika kwa amani. Anayedhani yuko salama leo na aseme sasa.

2. Wakati anapigwa risasi Tundu Lissu, baadae alihojiwa mbunge mwenzake, Elibariki Kingu, akasema "ni matukio ya kawaida, watu kutekwa, kupotea na kupigwa risasi". Mbunge anaona ni tukio la kawaida tu kwa mtanganyika mwenzake kupigwa risasi, tena anayeulizwa ni Mbunge na aliyepigwa risasi ni Mbunge. Nani aliyeko salama?

3. Bunge la Tanzania lilikataa japo tu kujadili hoja ya mmoja wa wabunge iliyowasilishwa bungeni ikiwa na lengo la kujadili "ulinzi na usalama wa Watanzania" baada ya matukio ya Kutekana-tekana kusambaa sana nchini. Bunge liligoma! Likapuuza maisha ya Watanganyika, kwa kuwa tu wao ni wabunge wanadhani wako salama. Nani aliyeko salama leo hapa Tanganyika?

4. Alipotoweka Ben Saanane mnamo November 28, 2017 watu wengine kwa sababu zao (labda na ujinga na ulevi tu) walitumia nguvu zao, muda wao, ndimi zao na kalamu zao kuuaminisha umma wa Tanzania na Dunia kuwa Ben amejiteka, wakaenda mbali na kusema "Freeman Mbowe KAMTEKA" hadi leo familia ya Saanane inaomboleza kijana wao, mke wake analia, bintiye kipenzi anamuuliza mama, mbona Baba kuchelewa kurudi.

5. Akapotea mwanahabari Azory Gwanda, anaulizwa waziri wa mambo ya ndani ya nchi kuhusu wapi alipo Mtanzania huyu anasema "Jeshi la polisi halihusiki kutafuta mtu ambaye amekwenda kutafuta maisha". Kauli kama hii Waziri akaitoa pale Marekani, Ufaransa, Uingereza au kwa majirani zetu Kenya amini nakuambia asingemaliza masaa 48 kabla ya kujiuzulu ama kwa hiari yake mwenyewe au kwa shinikizo la wananchi. Hapa kwetu kuna vichaa na walevi wachache wajinga waliomuunga mkono. Hadi leo Azory hajulikani alipo. Nani anayeweza kusema yupo salama hapa Tanganyika?

6. Wauaji wa Tajiri na mmiliki wa mabasi ya Super Sami, Samson Josiah almaarufu Super Sami, mkazi wa Magu, Mwanza wapo wapi? Tajiri huyu alipotea kwa muda, baadae gari yake inakutwa hifadhi ya Serengeti imechomwa moto. Siku chache anakutwa Mto Ndabaka akiwa kwenye sandarusi, marehemu tayari. Nani anayeweza kusimama mbele ya hadhara na kusema yeye yupo salama leo hapa Tanzania?

7. Tanzania imeokota maiti kwenye mifuko ya sandarusi iliyotupwa fukwe za bahari, mfano Coco Beach, maiti hizi ziliamriwa kwa haraka kufukiwa bila hata kufanyiwa 'postmortem' (kupata vinasaba) na ukizingatia wakati huo ndio tulikuwa tupo kwenye taharuki ya kumtafuta Ben Saanane. Tulipohoji kuliko,Waziri akasema miili hiyo ni kutoka nchi jirani na zingine ni za wahamiaji haramu. Nani aliyeko salama?

8. Mwanamuziki Roma Mkatoliki naye akatekwa. Baada ya Roma kutekwa akiwa studio, mkuu wa mkoa wa Darisalama anajitokeza hadharani haraka sana na kusema "Roma atapatikana Jumapili" na kweli akapatikana (sijui kwa namna gani) tulielezwa 'taarifa ya uchunguzi' itatolewa kwa umma. Hivi tumewahi kupata kuiona hiyo taarifa? Ipo? Haijatoka? Kwa nini? Kuna uzembe mkubwa kwetu wananchi. Hatulindani. Ubinafsi ni mkubwa kati yetu. Kila mmoja unadhani yeye yuko salama kuliko mwingine.

Jana ametekwa MO Dewji. Nani alitegemea kama huyu ataweza kutekwa? Nani aliyeko salama ajibu hili.

Kwa sababu jambo halipo katika familia yako, unafikiri upo salama. Unasubiri hadi jambo hilo likupate ndio unapiga kelele za kuomba msaada kwa watu ambao awali ulishindwa hata kuwasemea kwa sauti au maandishi. Hatujui kusimama upande wa wananchi, tumekuwa watu tuliogubikwa na uoga na uzandiki. Tutaangamia wengi sana.

Tunatambua, yanayomkuta Mo DEWJI ni ya kuhuzunisha, lakini si mambo ya kushangaza tena hapa Tanzania. Lakini hata Mohammed Dewji mwenyewe HAJAWAHI KUSIMAMA POPOTE kwa "status" yake na kukemea haya ambayo yanatokea sasa nchini, hakudhubutu kukemea utekaji, alichagua kukaa kimya wakati wengi kati yetu tunapotezwa. "MO was silence", hakuwahi kumsemea yoyote! Kukaa kimya wakati wengine wanateswa na kuuawa ni sawa na kuchagua kuwa upande wa mtesaji. Mchungaji Dr. Martin Luther King Jr aliwahi kusema kuwa " At the end we shall remember not the noise of our enemies but the silence of our friends ".

Hatupo tayari kupaza sauti wengine wanapodhulumiwa pengine kwa sababu za UJINGA tu kuwa wao si wa kada yetu. Ubinafsi ni mkubwa sana kati yetu. Tunaadhibiwa sasa. Hatuwezi kusimama na kumkemea adui, kwa sababu tayari tumegawanyika, na kwa sababu haujafikwa unafikiri wao waliofikwa ndio wenye matatizo! "MO" hajawahi kumtetea yeyote kati ya WALIOPETEZWA au KUUMIZWA au KUJERUHIWA! Hatumlaumu na hatutaacha kupaza sauti katika dhiki yake, Ila wengine tujifunze kitu kupitia hili.

Jalada la kesi ya Ben Saanane limefungwa hadi sasa. Namba yake ya simu yake ya mkononi (ambayo ni sehemu ya ushahidi muhimu) amepewa mteja mwingine wa VODACOM. Hili pia tumelisema tukaitwa "wapiga kelele". Tujiulize, kama MO ana nambari ya Vodacom, je Voda watagawa namba ya simu ya 'MO' kwa Mteja mwingine (ikiwa hatapatikana?) kwa nini?

Baada ya kutekwa kwa "MO" wanajitokeza viongozi kabisa wakubwa wa serikali hii bila hata soni na kueleza masikitiko yao. Na wengine wanaonesha kuumizwa na kuguswa na ambayo yametokea kwa bilionea huyo. Nchi hii imekuwa na Tabia za kupuuzia mambo sana. Tumekuwa watu na taifa la kuona kila kitu ni kawaida.

Katibu wa CHADEMA kata ya Hananasif, John Daniel alitekwa, akateswa, akatupwa ufukwe wa Coco. Polisi walipewa taarifa na hawakujali. Maiti ya Daniel ilikuwa huwezi kuitazama mara mbili, watekaji walijeruhi na kuharibu mwili wake kila pahali. Mwili ulikuwa hautazamiki mara mbili. Dar es salaam hii.

Mkuu wa mkoa anapata wapi ujasiri wa kusema matukio ya kutekwa kwa watu katika mkoa wa DSM ni "TENDO JIPYA AMBALO LINAIBUA HISIA TOFAUTI" hili linakuwa vipi tendo jipya ikiwa kuna watanzania zaidi ya watano wametajwa kupotea katika mkoa wa Dar es salaam? Au ni jipya kwa sababu ya "BILIONEA?"

Kwani ROMA MKATOLIKI hakuwa na familia? Hivi January Makamba kweli hujui kwamba hadi sasa LAURA BEN SAANANE amekosa kumuona kabisa baba yake? Hivi kuna sehemu January Makamba umewahi kutaja hata jina la BEN SAANANE kimakosa kuonesha kuumizwa na kupotea kwake?

January Makamba anasema "MO ANA FAMILIA na WATOTO WADOGO WANAHITAJI UWEPO WAKE" ni sahihi kabisa, kama ambavyo umetumia ukurasa wako wa Twitter kuonesha kuumizwa huku, nilifikiri ungetumia ukurasa huo kuonesha umuhimu wa kupatikana mwenyekiti wa halmashauri ya Kibondo, Simon Kanguye ambaye hadi sasa hajawahi kupatikana, huyu ni mwana CCM mwenzako wala si mpinzani Ila tofauti tu ni kuwa si maarufu sana na si tajiri mkubwa.

Godfrey Lwena Kule Kilombero alivamiwa na watu wanatajwa kuwa majambazi. Alikuwa Diwani kipenzi cha watu wa kata yake ya Namwawala kule Kilombero, alichinjwa, alikatwakatwa na kusasambuliwa. Sijawahi kusikia ambayo yameendelea baada ya hapo. January MAKAMBA hakuwahi kusema kuhusu hili, au Lwena yeye hakuwa baba kama 'MO' labda?

Tumefika hatua watanzania tunasema Tanzania sio salama tena, lakini mbunge wa CCM anakwenda kwenye vyombo vya Habari kwa kujiamini kabisa na kusema "MATUKIO YA KUTEKWA, KUPUGANA RISASI NA UHALIFU MWINGINE NI MATUKIO YA KAWAIDA SANA, BADO TUPO SALAMA TANZANIA". Tena mbunge huyo anaeleza kwa kujirudia-rudia kwa 'serikali ipo imara na haijashindwa'.

Wakati huyu mbunge wa Singida magharibi, Elibariki Kingu (CCM) anasema vitendo vya UTEKAJI na KUPOTEZANA nchini kwetu ni vya kawaida, na hata KUCHINJANA na KUPIGANA RISASI, alisahau TUNDU LISSU anauguza majeraha yake akiwa Ubelgiji kwa kupigwa risasi zaidi ya 38 mchana kweupeee, na waliomshambulia hawajawahi kutajwa.

Tundu Lissu ni mbunge mwenzake. Wanatoka mkoa mmoja wa Singida. Majimbo jirani. Lakini kitu cha ajabu huyu Kingu (magharibi) hajawahi kutoa japo salamu za pole, kumtembelea Lissu hospitali, kuomba kauli ya bunge, kutaka hata matibabu ya Lissu kugharamiwa na bunge, kuhusu Lissu (mashariki), Kingu anaibuka na kichefuchefu kingine hatari kabisa. Kwamba ni KAWAIDA. Ameshindwa hata kulaani tu unyama huu.

Achilia mbali mauaji mfululizo ya KIBITI ambayo yalidumu kwa muda mrefu na kuondoka na maisha ya wati na mali zao kuharibiwa. KIBITI, MKURANGA, RUFIJI na Pwani ilinuka damu na kutamalaki hofu. Baadae mbunge huyu wa Singida Magharibi anasema ni MAMBO YA KAWAIDA? Hawa ni sehemu ya watu waliotufikisha hapa tulipo sasa.

Hii Kutekana-tekana haikuanza kwa MO. Ni dhana ambayo imetoa matunda. Tuliomba watanzania kwa ujumla wetu tufanye mjadala wa kitaifa, kushinikiza serikali kuwa na wajibu wa kwanza kwa raia, kulinda usalama wao na mali zao. Wengine wakasema hayo ni mambo ya kawaida sana. Wakasema "nchi ipo salama Haya ya Kutekana-tekana ni mambo ya kawaida. Hata ulaya yapo" mjadala ukafa kifo cha mende.

Hii tulisema mapema. Utafika wakati, atakuwa hayupo ambaye yupo salama. Sio wanasiasa, viongozi wa Dini au hata wafanyabiashara achilia mbali wananchi ambao wao wanapotezwa kila uchwao kama sindano. Tulipaswa kusimama awali wakati yanatokea kwa wenzetu kama viashiria. Ubinafsi ukatawala wengi kati yao. Tunaadhibiwa kwa ubinafsi wetu.

Leo wanatekwa mabilionea, hadharani tena kwenye maeneo yenye ulinzi mkali. Je hali itakuwaje kwa mlalahoi wa Kibiti na Tandahimba? Tunashtuka, swali la kujiuliza sasa; TUMEFIKA VIPI HAPA? NANI AMETULETA KATIKA ENEO HILI? NANI AMBAYE ATATUNASUA KUTOKA HAPA? Tusiangalie tulipo-angukia, tuangalie sehemu tulipojikwa.. Kutekana-tekana ni uhuni wa kishamba tu.

Je ni nani aliye salama hapa Tanzania? Kama wameweza kumteka MO watashindwa nini kukuteka wewe? Tuache double standards.

Tuendelee kumuombea MO Dewji apatikane salama, pia tukumbushane kuwa maisha ya Ben Saanane, Azory, Alphonce Mawazo na wengine wengi yana thamani sawa na yeyote yule.

#FreeMoDewji

#BringBackBenAlive

#FreeAzoryGwanda=
Akuna ulikoacha kaka,tunachelewa kufanya maamuz 2 ila hakuna malefu yasiokuwa na n'cha iko siku kila jmbo litakuwa wz
 
Kuweni serious hata Marekani uhai wa Bill ni wa muhimu saana kuliko wa raia wa kawaida.

Uhai wa Mo kwa Tanzania ni muhimu hivyo akipotea lazima atafutwe kwa namna yoyote ile.

Kwa mwenyezi Mungu tu ndiko hakuna matabaka ila kwa binadamu tegemea yatakuwepo.
Nina wasiwasi na uwezo wako wa kufikiria
 
"Evil prevails when goodmen do nothing"

Tuendelee kumuombea MO Dewji apatikane salama, pia tukumbushane kuwa maisha ya Ben Saanane, Azory, Alphonce Mawazo na wengine wengi yana thamani sawa na y
"Evil prevails when goodmen do nothing" Burke

Hongera Omari kwa uandishi mahiri na wa kufidisha. Nidhahiri kua UDHALIM na UKATILI unaofanywa na serikali hii ya Magufuli ni matokeo ya wananchi hasa wenye elimu kukaa kimya, aidha kwa hofu au kwa kupuuza. Anaendesha nchi bila kafuata katiba, Waziri wa mambo ya ndani. anakuaje mpumbavu kutojua wajibu wake? Yaliomo ndani ya katiba ndio yameiweka nchi hii katika amani. Wanaoitupa katiba wana malengo yepi?

Nyerere aliandika hivi " WANACHAMA WA CCM wana Wajibu (ulazima) wa kukitazama chama chao, na kuona jinsi gani ya kuongeza DEMOKRASIA ndani yake. Wajibu huu si kwa chama chao tu, ni wajibu wa UZALENDO". akaongeza "OLE WAKE TANZANIA TUSIPOISADIA" Magufuli amekubali kua ana mapungufu kichwani hili linayakinishwa na matendo ya kutojali na kauli zake kama vule kufokea wafanyakazi wanaodai malipo yao akifoka Hela zenu mtapata lakini mtazitapika au kutukana wahanga wa tetemeko la Ardhi. na mengine mengi. Ni muhimu wananchi wafundishwe haki zao, ili walioelimika watakapo jitokeza kuitetea Tanzania wapewe sapoti. Nafikiri tumefika Njia Panda.

"Evil prevails when goodmen do nothing" JFK. "Udhalimu huendelea pindi watu wazuri wasipofanya kitu".

Hongera Omari kwa uandishi mahiri na wa kufidisha. Nidhahiri kua UDHALIM na UKATILI unaofanywa na serikali hii ya Magufuli ni matokeo ya wananchi hasa wenye elimu kukaa kimya, aidha kwa hofu au kwa kupuuza. Anaendesha nchi bila kafuata katiba, Waziri wa mambo ya ndani. anakuaje mpumbavu kutojua wajibu wake? Yaliomo ndani ya katiba ndio yameiweka nchi hii katika amani. Wanaoitupa katiba wana malengo yepi?

Nyerere aliandika hivi " WANACHAMA WA CCM wana Wajibu (ulazima) wa kukitazama chama chao, na kuona jinsi gani ya kuongeza DEMOKRASIA ndani yake. Wajibu huu si kwa chama chao tu, ni wajibu wa UZALENDO". akaongeza "OLE WAKE TANZANIA TUSIPOISADIA" Magufuli amekubali kua ana mapungufu kichwani hili linayakinishwa na matendo ya kutojali na kauli zake kama vule kufokea wafanyakazi wanaodai malipo yao akifoka Hela zenu mtapata lakini mtazitapika au kutukana wahanga wa tetemeko la Ardhi. na mengine mengi. Ni muhimu wananchi wafundishwe haki zao, ili walioelimika watakapo jitokeza kuitetea Tanzania wapewe sapoti. Nafikiri tumefika Njia Panda
 
Unamaanisha jinsi mtu anavyomiliki pesa zaidi ndio anavyokuwa na thamani zaidi ?
Mkuu sikupendezwa na kauli ya Trump lakin ukitafakari kwa kina utauona uhalali wa sisi kuitwa sh*t hole. Jalibu kupitia ata koment za wachangia tu..Afrika n Zid sh*t hole.
 
Yule mch wa kimarekani aliyekua kakamatwa Turkey marekan mzima imepiga kelele na vikwazo juu...Assume kama angelikua n mtanganyika,ata pole kwa familia yke hautoisikia kabisa.
 
wakuu kama Kichwa tajwa hapo juu ivi zigo hili alibebe nani? Kama Taifa tumeshindwa kukabiliana na vitendo hivi hovu vinavyopelekea uvunjifu wa Amani?
Kama Raia wa kawaida nashindwa kuelewa nchi hii kama ina vyombo vya ulinzi na Usalama.
Watu wana hofu kila mmoja anamashaka na mwenzake taratiiibu Amani inachikichia kusikojulikana kwasababu ya watu wasiojulikana.
Viongozi (Maraisi) wastaafu wako kimia kana kwamba nchi iko salama.
Kama Polis wameshundwa kwanini wasiombe JWT waingilie kati?
Wakuu tuachane na siasa nchi inakoelekea nipabaya sana leo kwangu kesho kwako. Usipotekwa wewe watamteka mkea au mmeo au Mtoto au ndugu, niwakati sasa wakulitaka jeshi la Polis nchini kutimiza majukumu yake.
Lakini pia swala ili linahitaji uwajibikaji waziri wa mambo ya ndani awajibike pamoja na Mkuu wa jeshi la polis ili kurudisha imani kwa wananchi.
 
Vyombo gani unavyosemea????
Jeshi la polis na Usalama wa Raia kwa ujumla ambao kila mala wamekuwa wakituhumiwa lakini wanashindwa kabisa kukana kwa kujibu hoja badala yake wanakana kwa vitisho, hili linazidi kupasua Taifa na wananchi kujiona hatuna mfariji ((Rais)
 
USALAMA WA TAIFA.
 
Habari wandugu
naipa pole familia ya mo na namuombea mo huko alipo.

mpaka sasa ni siku tatu zimepita na watanzania tunaona kama ndoto

tujiulize wangapi tulisikia matukio ya kupotea kwa watoto,
je tumejiuliza maswali mangapi na kupata majibu mangapi
jibu 1 tu watekaji watoto ni rahisi tu ni sale of human organs
lakini kwa MOHO majibu yatakuwa ni mengi sasa je mpaka atekwe mkuu wa nchi ndio tuwe serious kweli.???????????????????????????
 
Back
Top Bottom