Utawasikia wanasema binadamu wote ni sawa. Ni uongo!

Utawasikia wanasema binadamu wote ni sawa. Ni uongo!

Hayo yote uliyoandika haiondoi ukweli kwmba binadamu wote ni sawa. Mada ilipaswa iwe "Binadamu wote ni sawa, ila wanatofautiana hali za maisha". Binadamu yeyote yule haijalishi ni fukara au tajiri anahitaji chakula,mavazi na malazi ili apate kuishi.
I wonder why is sex not included in Maslow’s hierarchy of needs, a highly-respected theory. Au kuna binadamu hasiyehitaji sex?
 
Lifespan ya nchi gani unaongelea mkuu? Tanzania?
Unaweza weka ushahidi wa takwimu kuonesha kwamba life span imeshuka?
Jamaa uelewa wake ni mdogo na anajibu kwa hisia Ana hulka Za kumjadili mtu na sio hoja ya mtu.
 
Tajiri haendi chooni
Tajiri hakojoi
Tajiri halali
Tajiri ana macho matatu

Mtoa mada alimaanisha hivi.
Tajiri Anaenda choo cha namna gani,?masikini anaenda choo cha namna gani?,Tajiri analala wapi na analalia nini ukilinganisha na masikini?,kwa uelewa wako ukaelewa kwamba nilimaanisha hivyo,you are of low voltage and low power indeed
 
Tajiri haendi chooni
Tajiri hakojoi
Tajiri halali
Tajiri ana macho matatu

Mtoa mada alimaanisha hivi.
Tajiri Anaenda choo cha namna gani,?masikini anaenda choo cha namna gani,Tajiri analala wapi na analalia nini ukilinganisha na masikini?,kwa uelewa wako ukaelewa kwamba nilimaanisha hivyo,you are of low voltage,low power indeed
I wonder why is sex not included in Maslow’s hierarchy of needs, a highly-respected theory. Au kuna binadamu hasiyehitaji sex?
Hii ni nafasi ya wewe sasa kuikosoa hiyo theory na kuirekebisha kwa hoja yakinifu na ndio maana bado ni theory tu.
 
Usawa wa binadamu upo hapa... Kwamba wote tunazaliwa na mwanamke, tunaishi (kwa kutegemea kula na oksijeni) na hatimaye tutakufa regardless of kipato na hapa ndo penye msingi wa usawa

Ila linapokuja suala la ulizaliwa eneo gani, ukaishi wapi, ukala nini na hatimaye ukafia wapi ndo tofauti inapotokea.

Basically we are the same, but realistically we are different
“Basically we are the same,but realistically we are different “ over
 
Binadamu wote ni sawa mbinguni!
Duniani sahau hiyo kauli.
Huko mbinguni Hapana ..
Katika uislam tunaambiwa Kuna milango nane ya pepo means Kuna madaraja/levels nane za pepo.
Kulingana na matendo yako utaingia daraja linalofanana na wewe..
Sasa huko mbinguni usawa uko wapi?
 
Binadamu hatuko sawa isipokuwa tuna mahitaji ya msingi ambayo ni Sawa kama vile kula kulala kuvaa. Lakini Kuna mambo mengi hatuko sawa kama vile ustaraabu, akili, rangi maumbile, uwezo wa kufikiri na kutatua changamoto, uwezo wa kipato, kukabiliana na mambo n.k. mfano msomi wakiafrika hutegemea kuajiliwa na akijenga nyumba na kununua gari hapo hujiona ameyapatia maisha, Je jamii inanufaika vipi na usomi wake?
 
It's not what it is but what it ought to be....; It's about fairness, justice, and non-discrimination. Katika kupewa opportunities, resources especially likija suala la utaifa, kabila au status....

Kama human race that is our target.....; Mfano tunaposema kuna demokrasia sio kwamba kweli kuna Power of the people ila hio ndio utopian destination
 
Hata huko mbinguni sina uhakika,kama ni sawa na aliyetuumba ni yuleyule,why wengine wawe nacho na wengine wasiwe nacho wakati yeye ndio hutoa na wanasema ni wahaki na ukawa,bado hainiingii akilini kama huko nako kuna usawa.
Hakuna usawa ndo maana mwingine anaenda motoni kunako waka moto wa milele na mwingine anakwenda mbinguni kuliko na raha za paradiso
 
Maisha Yana siri na siri hiyo ndio maisha yenyewe.

Kuna watu wamekazana kusema binadamu wote ni sawa, sijui wanajifariji na umasikini wao ama vipi? Labda kama wanamaanisha ni sawa katika maumbile ya kibinadamu, lakini si katika uwezo wa kuyamiliki maisha.
Kuna watu wanakula maisha na kuna wale tunao liwa na maisha.

Mimi natembelea Raum, lakini kuna dogo anamiliki Cadillac ya mwaka 2024 na magari mengine ya bei mbaya.
Kuna watu hulipia watoto wao ada shule ya msingi 21M-60M+ kwa mwaka, halafu kuna wale watoto wetu wanasoma shule ya msingi Nachingwea, wakiwa na kidumu cha maji na mfagio mkononi.

Mimi nimepanga kwa Mzee Komba, nyumba rangi inabanduka ukigusa ukuta umechafuka, lakini kuna watu wanaishi kwenye nyumba ambazo kuta zimepigwa mawe ya Tanga kama siyo tiles za kisasa. Binadamu wote ni sawa au siooo? Wacha tujifariji.

Kuna watu wanamiliki minjengo ya mabilioni kwa pesa zao wenyewe, halafu kuna bwana mwalimu Selemani amejenga kakibanda kake ka 40M kwa mkopo kutoka NMB na ana vimba noma.

Nina kafeni ka Aliyons kananengua kiuno usiku kucha na bado ninasweat ile mbaya, halafu kuna wale wanaoishi kwenye nyumba zenye kiyoyozi full-time na wanajifunika mablanketi ya kutengeneza joto kwa umeme.

Kuna wana zizi la ng’ombe limewekwa kiyoyozi na ceiling fan, chini pamepigwa tiles maalum na kuna wafanyakazi wakusafisha banda kuondoa kinyesi kila ng’ombe anapojisaidia ili asichafuke. Sasa nadhani yatosha kusema kati ya anayeishi kwenye kageto ka 25k na makolokolo yote humo na huyo ng’ombe, ng’ombe amejulikana.

Kuna watu wameajiriwa, wanasubiri wastaafu wapewe kiinua mgongo ambacho ni 40M-1B, na kuna watu huingiza hiyo pesa kwa siku, wiki, au mwezi.

Maisha hayajawahi kuwa sawa, na binadamu hawajawahi kuwa sawa except katika uumbaji tu.
Unakutana na demu kapiga makeup ya bundi 5 na joto la Dar hata unyunyu wa 25k umemshinda; anakujiremba kote lakini anatema kikwapa ile mbaya. Halafu kuna demu akikatiza kwako hana makeup ila anavutia, ananukia vizuri. (Kuna wanaoweka unyunyu lakini bado wanatema.)

Kuna watu wakienda hospitali kutibiwa, bili ikitoka 100k wanalalama kama king’ora cha ambulance iliyobeba mgonjwa mahututi. Halafu kuna wale matibabu yao bili ni 10M na analipa cash bila zengwe; yaani wanaranda na begi la minoti hospitalini, ilhali wale wa kwa Mtogole pesa ipo kwenye akaunti ya Tigo Pesa.

Binadamu hatujawahi kuwa sawa na haitatokea tukawa sawa. Huu usemi ni manipulation za kuwafariji masikini tu. Mtu anatumia simu ya 8-20M na anazo kama tano, halafu kuna Ashura pale kwa Tegeta kwa Ndevu anachombo cha mawasiliano Infinix Hot 10 kaivalisha cover la kamdoli kapusi na ananata noma. (Anyway mtu chake bwana.)

Kuna watu wanakufa na kuna watu wanafariki. Kuna watu wanazikwa na kuna watu wanafukiwa. (Elewa hii dhana.) Kuna watu wanafariki si kwa kukosa matibabu, bali kwa sababu tatizo lake madaktari waligonga mwamba katika kila kona za dunia. Halafu kuna watu wanakufa kwa malaria au septicemia ambayo matibabu yake ni 20k tu.

Yamkini binadamu hatujawahi kuwa sawa, na haiji kutokea. Kila mmoja apambane amiliki pesa kwa namna yoyote ile. Kikubwa uwe nazo lakini usimwage damu. Pambana.

Kuna watu wakiumwa watoto wao wanawapeleka hospitali za bei mbaya si kwa sababu wameshindwa kuzimudu gharama. Lahasha, wanajisikia fahari kuwahudumia maana pesa ipo kwa kila mtu wa damu yao. Halafu kuna sisi, wazazi wetu wanatutegemea kwa kila kitu na hatumudu.

Tujitahidi kutengeneza mfumo wa kuingiza pesa kwa vizazi vyote. Mfumo usio kufa ili tuache kujifariji kishamba. Binadamu hatujawahi kuwa sawa na haiji kuwa hivyo.

Tunafanana kimuonekano. Kwamba binadamu wa kawaida ana kichwa tumbo na pia hata miguu.
😛
 
Huu uzi kwenye comments watu wanajifariji sana. Ila ukweli ni kwamba kiuumbaji sote kwa macho ya nyama ya kawaida TUNAJIONA tupo sawa ila SIYO KWELI.

Binadamu hatupo sawa hata kidogo.

Tunapenda tu kujitia moyo ila HATUPO SAWA hata kidogo.

Kiroho, Kimwili, Kiakili na hata kimaisha kwa ujumla hatupo sawa tusidanganyane hapa.

Mimi kuitwa BINADAMU na wewe ukaitwa BINADAMU haina maana sote tupo sawa au tunafanana.
 
Huu uzi kwenye comments watu wanajifariji sana. Ila ukweli ni kwamba kiuumbaji sote kwa macho ya nyama ya kawaida TUNAJIONA tupo sawa ila SIYO KWELI.

Binadamu hatupo sawa hata kidogo.

Tunapenda tu kujitia moyo ila HATUPO SAWA hata kidogo.

Kiroho, Kimwili, Kiakili na hata kimaisha kwa ujumla hatupo sawa tusidanganyane hapa.

Mimi kuitwa BINADAMU na wewe ukaitwa BINADAMU haina maana sote tupo sawa au tunafanana.
Mbona utawajua tu,na mapovu yao,wapambane na kujifariji kizembe
 
Back
Top Bottom