Utawasikia wanasema binadamu wote ni sawa. Ni uongo!

Utawasikia wanasema binadamu wote ni sawa. Ni uongo!

Binadamu wote ni sawa, ila wanatofautiana hali za maisha". Iwe inasomeka hivi.
 
Hayo yote uliyoandika haiondoi ukweli kwmba binadamu wote ni sawa. Mada ilipaswa iwe "Binadamu wote ni sawa, ila wanatofautiana hali za maisha". Binadamu yeyote yule haijalishi ni fukara au tajiri anahitaji chakula,mavazi na malazi ili apate kuishi.
Similarity and congruence principles,utofauti wa maisha ndio comparative factor ya equality,zingatia utata wa lugha ya Kiswahili.
 
Huwezi kuzungumzia maisha na kuishi kwa sasa ukajitenga na material things,hayo yote ndio kipimo kikuu cha utofauti wa watu ndugu,wewe ulipoajiriwa kwa mfano uliwaza kununua tv kubwa,sofa nzuri nk,ukawa na uhakika wakufanya muda wowote na hapo ndio ulianza kuona ahueni ,huwezi kutenganisha kuisha na material needs never.
We bado mtoto na unaishi katika illusion.


Ungesema materials things inaongeza life span , inajenga Afya na inakufanya unaishi long life ungekuwa sahihi.


Unajua kuwa life span imepungua Sana sasa hivi though kuna material things nyingi.
 
Binadamu ni sawa katika kupata haki za binadamu, huko kwingine hata urefu hatuko sawa kuna warefu na wafupi.
Hata hizo haki Za binadamu hatuzipati kwa usawa,mfano kuna watu wanakufa kisa wamekuwa matibabu ilihali walipaswa kupata matibabu ili waishi,kuna watu wanafungwa maisha wakati hawana hatia kisa wamekosa wakili wakuwatetea maana hawana cha kuwalipa,na kuna mtu Ana hatia kabisa lakini anaonekana hana kosa.
 
Kuna hii post huwa inanifurahisha na kunikumbusha kuwa wote tupo sawa tu😊

1000016620.png

Siku moja tulikuwa tumekaa kijiweni. Akapita tajiri mmoja wa mtaa tunaoishi kwenye Range Rover mpya, kali sana. Alikuwa anajukana kwa utajiri wake. Tulikuwa tumekaa na mzee mmoja, akaanza kuchoma choma ardhi kwa kijiti, tena kwa ghalabu huku akisema, ''hata uendeshe gari gani, wote njia yetu ni moja tu, tunaelekea huku'', akimaanisha ardhini. Na mara wote tuliokuwa pale tukajisikia kuliwazika na tukajiona na furaha, kama tumetua mzigo mzito.
 
Kwa upande wa isuue za Dr Janabi binadamu ni sawa kwa sababu haijalishi maskini au tajiri itabidi mshindie kipande cha boga na juice ya mwarobaini.
 
Binadamu wote ni sawa mbinguni!
Duniani sahau hiyo kauli.
Hii kauli yako nitaiandika nyumu ya Gari langu mbuvu nililonunua kwa shilingi laki tisa ambayo huku mtaani watu wamelipa jina la 'tetanus' kutokana na kuvamiwa na kutu kwa kukosa service.
 
We bado mtoto na unaishi katika illusion.


Ungesema materials things inaongeza life span , inajenga Afya na inakufanya unaishi long life ungekuwa sahihi.


Unajua kuwa life span imepungua Sana sasa hivi though kuna material things nyingi.
Sijawahi ishi kwa illusion na wala sio mtoo,jenga hoja zako watu wakuelewe, yamkini huelewi mantiki ya falsafa ,kwa mifano chukulia mfano falsafa ya muda.

Sioni faida yakuwa na life span kubwa halafu huwezi ku afford life.

Nadhani nilichokiandika mimi ni sahihi na sio hicho unachotaka niandika hivyo ,hata katika fikra ndani ya hoja hii hatupo sawa mentally maana umeahindwa kung’amua
 
Usawa wa binadamu upo hapa... Kwamba wote tunazaliwa na mwanamke, tunaishi (kwa kutegemea kula na oksijeni) na hatimaye tutakufa regardless of kipato na hapa ndo penye msingi wa usawa

Ila linapokuja suala la ulizaliwa eneo gani, ukaishi wapi, ukala nini na hatimaye ukafia wapi ndo tofauti inapotokea.

Basically we are the same, but realistically we are different
 
Watu wote sio sawa katika namna yoyote ile.

Kuanzia maumbile mpaka maisha yote.

Jambo lililowashinda wakomunisti ni kudhani kuwa usawa unawezekana walifail vibaya sana.
 
Msemo wa usawa ni kwenye uumbaji, haiwezekani tuwe swa kwenye uchumi ndugu, kama ulikuwa unawaza hivo uko mbali mno ndugu.
 
Back
Top Bottom