Utata wa Tanganyika na Tanzania

Utata wa Tanganyika na Tanzania

Hatusherehekei Uhuru wa nchi yoyote. Kwani wewe unasherehekea?
 
jamani hivi bado tunahitaji kujiuliza utanganyika na uzanzibar? leo hii ulaya mataifa makubwa yanaungana sisi bado tunawaza kujitenga kweli tutaweza kuwa na africa union? matajiri na wenye nguvu wanaungana nyie maskini na dhaifu mnatengana :spy:?

Issue si kuungana ni mmeunganaje! hivyo usipotoshe kwa kuwawekea watu umuhimu huo wa kufikirika pasipo kujenga hoja ya vipi tunaungana na tutafaidika vipi! na kwa taarifa tu ulaya tayari wanaujutia muungano wao upo hapo? Tuombe tu tupate viongozi kama wa akina Lincolin watupe muungano wa dhati otherwise tunaliwa tu.
 
Utata mtupu sio bara sio Zanzibar.

Constitutional conference for Zanzibar was held at Lancaster House in London in September 1963. At conclusion of the conference it was announced Zanzibar would be independent as from 10 December 1963. Thus after 73 years the British Protectorate in Zanzibar come to end. Habari ndio hiyo ,9 dec uhuru Tanganyika,10 dec uhuru Zanzibar.
 
Hivi ukimuuliza Mzanzibari rais wako ni nani? Harakaharaka atakujibu nini? Je ni sahihi kusema rais wa Tanganyika yuko ndani ya rais wa Tanzania. Ni wakati gani rais wa Tanzania anajigawa na kufanya mambo ya Tanganyika maana kuna mambo ambayo si Tanzania(muungano) au yale ya Tanganyika hayapaswi kufanywa na rais? Naishia hapa kujihoji Maana sina PANADOL.
 
Tanzania bara = Tanganyika kwa lugha ya kimuungano, ila labda tuanze kudai huduma muhimu kabla ya kudai jina la sehemu tunayoishi.
Ukubwa jalala.......tusubiri miaka 50 ya muungano watasemaje? wapemba wamewashika vibaya.
 
jamani hivi bado tunahitaji kujiuliza utanganyika na uzanzibar? leo hii ulaya mataifa makubwa yanaungana sisi bado tunawaza kujitenga kweli tutaweza kuwa na africa union? matajiri na wenye nguvu wanaungana nyie maskini na dhaifu mnatengana :spy:?
Kwa nini usishangae siku hizi kuna nchi inaitwa Southern Sudan na mji mkuu wake ni Juba? Unafki wa Watanganyika ndio huu, wao ya kwao wanayaona kama uhaini, lakini kwa wenzao wanakwenda kukenuwa meno. Unafki ni ugonjwa mbaya sana.
271081_181418668587412_100001578403231_529301_3696557_n.jpg
 
Tanganyika yangu wamekuzika huku ukiwa hai,,,wanatembea juu yako wanakukana...naipenda tanganyika nchi ya babu zangu,,,,,
 
jibu la moja kwa moja nchi hii inaitwa tanganyika; tarehe 9 december 2011 tutasherehekea miaka 50 ya uhuru. Wanaosema miaka 50 ya uhuru wa tanzania bara ni wanafiki wanaopotosha historia ya nchi yetu labda kwa maslahi yao. Naipenda tanganyika yetu.
naipenda tanganyika na siwezi kujidanganya kuwa nipo tanzania bara ,hata mwanangu huwa anahoji tanganyika ilipotelea wapi?
 
Jibu la moja kwa moja nchi hii inaitwa Tanganyika; Tarehe 9 December 2011 tutasherehekea miaka 50 ya uhuru. Wanaosema miaka 50 ya uhuru wa Tanzania bara ni wanafiki wanaopotosha historia ya nchi yetu labda kwa maslahi yao. Naipenda TANGANYIKA yetu.
NAIPENDA TANGANYIKA NA SIWEZI KUJIDANGANYA KUWA NIPO TANZANIA BARA ,HATA MWANANGU HUWA ANAHOJI TANGANYIKA ILIPOTELEA WAPI?:A S embarassed:
 
Kama wazanzibari wanautaka uzanzibari wetu basi na sisi tuchukue utanganyika wetu
 
wapendwa hapo juu it is so sad kama taifa lote tunafanya vitu pasipo kujiuliza kama hivi na tunaenda tu...kwa sababu inatakiwa na imesemwa!!!

if we real need tanganyika lets deny that Nyerere isn not the father of this nation!

why should we deny him as the father of the nation while he was the first president of the united republic of Tanzania from 1964 to 1985? there is a great connection between Nyerere and Tanzania, without Nyerere there wouldn't be Tanzania because he played a major role to engineer the union.
 
mimi nimezaliwa kwenye taifa linaloitwa Tanzania ila hainiingii akilini kuita miaka 50 ya uhuru wa Tanzania bara maana wakati kipindi mkoloni anakabidhi nchi ya Tanzania bara bali alikabidhi nchi ya Tanganyika kwa nini wakubwa wanapotosha ukweli
 
jamani hivi bado tunahitaji kujiuliza utanganyika na uzanzibar? leo hii ulaya mataifa makubwa yanaungana sisi bado tunawaza kujitenga kweli tutaweza kuwa na africa union? matajiri na wenye nguvu wanaungana nyie maskini na dhaifu mnatengana :spy:?

Hakuna anayewaza kujitenga labda wewe. Kinachotakiwa ni muundo usio na maswali wa Muungano. Tanganyika must be reborn!!
 
Tanganyika bado ipo hai, hujitokeza toka ICU katika michuano ya challenge, huwa nchi pekee ambayo hushiriki bila kuwa na serikali wala bendera yake.
Huwa inatia huruma kwa kweli.
 
Like the Serengeti, Tanganyika shall not die. Bila shaka tunahitaji muundo wa serikali tatu.
 
jamani hivi bado tunahitaji kujiuliza utanganyika na uzanzibar? leo hii ulaya mataifa makubwa yanaungana sisi bado tunawaza kujitenga kweli tutaweza kuwa na africa union? matajiri na wenye nguvu wanaungana nyie maskini na dhaifu mnatengana :spy:?
Hapa kinachoongelewa si uzanzibar wewe! Tunaongelea Tanganyika iliko,na hii miaka 50 ni nchi ipi? Kama ni tanzania mbona haijafikisha miaka 50? Kama ni Tanganyika mbona vitambulisho vyake havitumiki? Naona we ni kilaza wa kufikiri ndo maana unajibu kama mtoto wa chekechea,kama kitu hukijui uliza ili uelekezwe .
 
jamani hivi bado tunahitaji kujiuliza utanganyika na uzanzibar? leo hii ulaya mataifa makubwa yanaungana sisi bado tunawaza kujitenga kweli tutaweza kuwa na africa union? matajiri na wenye nguvu wanaungana nyie maskini na dhaifu mnatengana :spy:?


we kumbe ulikuwa hujui kuwa European Union kila nchi iko na dola yake huru na sheria zake wameungana kwa baadhi ya mambo tu moja ya issue yao kubwa ni kulinda nchi zao na border zake na baadhi ya business...sio ule muungano wa bandika bandua wa Tanganyika na Zanzibar kuwachanganya raia akili zao.
A%20S%20465.gif
 
Nasubiri 9december kusikia wimbo wa taifa utaimbwaje maana tz haina miaka 50. Sina ugomvi na ndugu zetu wazanzibar,ila linapoja swala utaifa naona kama wanajitenga.Kama uzanzibar basi uwepo UTANGANYIKA. Maana naona wimbo wa tanzania bara na tanzania visini umeshindwa kuimbika.Penye uzanzibar kuwepo UTANGANYIKA.Kwenye tanznia hakuna kitu kinachoitwa zanzibar,kuna tanzania visiwani. Na kwa nini zanzibar kusiwepo TANGANYIKA.Siamini kwenye selikari tatu maana itakua mzigo kwa taifa.Viongozi wetu waaje ghirba maana kwenye huu mungano unawanufaisha wao,ususani viongozi wa zanzibar. Ndiyo maana ukiongelea selikari moja wanaku
a wakali eti zanzibar aiwezwi kumezwa ni nchi kamili.Hivi TANGANYIKA sio inchi kamili? Na vile TANGANYIKA hatuna viongozi,zanzibar wavunja katiba viongozi wa tanzania wako kimya maana wanaogopa kuwanyoshea vidole.Nani kakwambia sultan anyoshewa kidole? Lazima tutambue kwenye wao kuna sisi.Wao wana wimbo wa taifa,sisi hatuna.Wao wana bendera taifa sisi hatuna.Kweli wimbo wa tanzania bara na tanzania visiwani unaimbika?au tumebaki majuha ndiyo tunaitikia,kiitikio bila kujua beti za wimbo zinaimbwaje? Imefika mida tuache unafki wanapozungumzia uzanzibar na UTANGANYIKA sio dhambi kama wanazungumza.Ila nitaendelea kusisitiza siamini kwenye selikari tatu,naana ni mzigo kwa wananchi .Najua kwa selikari moja kwa viongozi wa zanzibar litakua gumu maana hawana masrai nalo.Huu mungano naona ni mzigo kwa kiumbe alioubeba,mzigo unaoneka unakwenda ila mtu alio beba haonekani. Najua huyo kiumbe siku ya kuchoka kubeba huu mzigo wa mungano atajitokeza.''Bandugu heri ya 9december''
 
Back
Top Bottom