Faida ya Muungano kwa ujumla wake haipo. Wazanzibari ndio pekee wenye kufaidika na muungano huu. Huenda mmojawapo atakujibu. Wazazibari ndio wenye haki ya kujiita Watanzania. Wao wana uwezo wa kupata kila wakitakacho Bara na Visiwani. Wanachukua ardhi popote, wanapata madaraka (Mawaziri, wakurugenzi, mameneja n.k.) huku Bara. Wanakuwa na madaraka katika mambo yasiyo ya muungano. Wamejazana katika Bunge la muungano na kushiriki kikamilifu katika mijadala ya yale yasiyo ya muungano. Kule Visiwani (Pemba na Unguja) Mtanzania bara (Mtanganyika) huna chako. Huwezi kuingia Baraza la Wawakilishi, huwezi kuwa kiongozi wa Serikali yao, ardhi hupati, hata ukitaka kuoa huko utawekewa vikwazo utadhani uko uchina. Muungano wa sasa hautufai bila TANGANYIKA YETU. Watanganyika tuungane kupigania nchi yetu tukufu ya Tanganyika. Hakuna suluhu bila Tanganyika. Hakuna nchi iitwayo Tanzania Bara iliyopata Uhuru miaka 50 iliyopita. Tanganyika ndiyo inayoadhimisha miaka 50 ya uhuru!! Hivi viongozi wa nchi hii hawaoni aibu kutukuza nchi ya kufikirika na kuacha nchi yao halisi Tanganyika?