Utata wa Tanganyika na Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utata wa Tanganyika na Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kwamwewe, Dec 5, 2011.

 1. kwamwewe

  kwamwewe JF-Expert Member

  #1
  Dec 5, 2011
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,314
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  Utata wa Tanganyika na Tanzania.

  Edson Kamukara

  SINA muda wa kupoteza leo isipokuwa naomba tujivue unafiki na kisha kila mmoja wetu ajihoji Desemba 9, mwaka huu, tunasherehekea Uhuru wa miaka 50 ya taifa lipi? Nahitaji jibu la moja kwa moja si siasa za upotoshaji, anayejibu swali hili anapaswa kujiweka katika nafasi ya mtoto mdogo anayepaswa kujua jambo fulani kiundani.

  Desemba 9, mwaka 1961, kulikuwa nchi yetu inaitwa Tanganyika ambayo ilipata uhuru wake. Ilipofika mwaka 1964 Rais wa Tanganyika Julius Nyerere na mwenzake wa Zanzibar Abeid Amani Karume, waliona ipo haja ya mataifa hayo kuunga.
  Muungano ni kuunda umoja na ushirika wa pamoja lakini nje ya hapo kila mtu anabakia kuwa kama alivyokuwa awali. Hii kwa bahati mbaya sivyo ilivyokuwa kwa huu muungano wetu.

  Baada ya Muungano kufanikiwa na kuundwa Tanzania, nchi moja ya Tanganyika ilinyongwa na ikabakia Zanzibar. Na ndani yake zikaletwa siasa za Tanzania Bara na Tanzania Visiawani.

  Hivi mtoto wa kizazi cha leo anapohoji kujua ilipo Tanganyika tunaweza kumweleza nini mbali na siasa? Zanzibar ipo Tanganyika ilikufa ikazaliwa Tanzania Bara ambayo kimsingi ndiyo hiyo hiyo Tanzania.

  Hii ndiyo historia ya nchi yetu, na tunathubutu kutembea kifua mbele tukijiaminisha kuwa tumekomaa kifikra vya kutosha wakati tunapotosha ukweli kuhusu Taifa letu?

  Leo watoto, vijana, watu wazima na mbaya zaidi viongozi kila mmoja anaimba kuwa Desemba 9, mwaka huu, tunasherehekea miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara ( Hii ni nchi ipi?).

  Zanzibar wana vielelezo vya utambulisho wao kama taifa, wana wimbo wa taifa, bendera, katiba yao, Bunge lao na mengineyo. Nchi inayoitwa Tanzania Bara haina bendera, wimbo wa taifa, Bunge badala yake wanatumia vielelezo vya taifa la Tanzania lililotokana na muungano wa (Tanganyika na Zanzibar).
  Hivyo, hata Desema 9 mwaka huu, kinachosherehekewa si miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika. Maana siku hiyo utaimbwa wimbo wa taifa wa Tanzania, itapeperushwa bendara ya Tanzania, Rais atakuwa wa Muungano, sasa hapa tutasemaje ni uhuru wa Tanganyika (Tanzania Bara kama tunavyojidanganya)?

  Hivi ndivyo tumeendelea kujidanganya kwa miaka yote. Tumekuwa na Bunge la Muungano ambalo linawashirikisha wabunge kutoka Zanzibar, kimsingi linapaswa kujadili mambo yale yanayohusu muungano tu.

  Lakini kutokana na udhaifu wa muundo wa muungano wetu hata kwenye mijadala ya mambo yasiyo ya Muungano wabunge wa Zanzibar wanaendelea kuwemo wanashiriki kutuamulia wakati kule kwao wana Baraza la Wawakilishi ambalo linajadili mambo yao pekee.
  Huu mfumo wa muungano wetu lazima tukubaliane kuwa una kasoro hata kama hatutaki kuambiwa ukweli. Ni bora kujitathmini kuanzia hapa ili itafutwe suluhu ya kuondosha upotoshwaji wa historia ya nchi yetu ya Tanganyika badala ya kuendelea kuzika vichwa mchangani kama kanga tukidhani tumejificha hakuna shida.
  Mfano mdogo wa mkorogano huu unajitokeza kwenye michezo hasa kwenye mashirikisho yanayotutambua kama nchi mbili. Kwa sasa hapa Tanzania yanaendelea mashindano ya mpira wa miguu ya Kombe la Shirikisho la Mpira wa Miguu la Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).
  Katika michuano hiyo Zanzibar wameingia kama nchi, wanatambulika kwa timu yao ya Zanzibar Heroes wakiwa na bendera ya taifa lao na wimbo wao wa taifa halafu eti sisi tumejibadilisha kutoka Taifa Stars tunajiita Kilimanjaro Stars.

  Lakini kinachofanyika kwenye timu ya Kilimanjaro Stars ni kile kile cha Taifa Stars, kwani wimbo na bendera wanavyotumia ni vile vile vya Tanzania. Na hata kocha kabadilishwa tu mwaka huu baada ya Wazanzibari kuhoji maana huyo huyo wa Taifa Stars ndiye alikuwa anafanywa wa Kilimanjaro Stars.
  Mimi ni mmoja wa waumini nisiyeona aibu kusema kuwa tunaadhimisha miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika, lakini siku hiyo ya Desemba 9 mwaka huu, sitasherehekea maana hakutakuwa na bendera ya Tanganyika wala wimbo wa Tanganyika ili kuniletea hisia za kumbukumbu ya kuachana na ukoloni.

  Naogopa sana unafiki na uongo wa kujidanganya kushiriki kuimba wimbo wa Mungu ibariki Tanzania wakati huo bendera ya rangi nne ya Tanzania ikipeperuka halafu nijiaminishe kuwa nimesherehekea miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika.

  Tafakari!
  edkamukara@yahoo.com/ 0714717115/ 0788452350
   
 2. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #2
  Dec 5, 2011
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 15,012
  Likes Received: 3,197
  Trophy Points: 280
  Swallowing,,please wait.,,,,
   
 3. Globu

  Globu JF-Expert Member

  #3
  Dec 5, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 7,975
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Uhuru wa Tanganyika. Hakuna kitu Tanzania bara.
   
 4. AirTanzania

  AirTanzania JF-Expert Member

  #4
  Dec 5, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 1,127
  Likes Received: 678
  Trophy Points: 280
  I want my country, my flag, my National anthem ndio niweze kusheherekea Uhuru wa nchi yangu [​IMG]
   
 5. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #5
  Dec 5, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  ni kweli mkuu huu ni uhuru wa TANGANYIKA HATA KAMA TUTAJIDANGANYA :poa
   
 6. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #6
  Dec 5, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,570
  Likes Received: 3,869
  Trophy Points: 280
  wapendwa hapo juu it is so sad kama taifa lote tunafanya vitu pasipo kujiuliza kama hivi na tunaenda tu...kwa sababu inatakiwa na imesemwa!!!

  if we real need tanganyika lets deny that Nyerere isn not the father of this nation!
   
 7. M

  Megawatt B JF-Expert Member

  #7
  Dec 5, 2011
  Joined: Aug 23, 2011
  Messages: 260
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  ...........tanganyika yangu naitaka!!!, shime tujitokeze kwenye mchakato wa katiba kudai tanganyika yetu!
   
 8. Crucifix

  Crucifix JF-Expert Member

  #8
  Dec 5, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 1,618
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Go to hell! Isn't Nyerere father of Tanganyika? He assumed the honor after Tanganyika independence. There is no need to deny Nyerere or what. We need Tanganyika at any price
   
 9. thereitis

  thereitis JF-Expert Member

  #9
  Dec 5, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 297
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Jibu la moja kwa moja nchi hii inaitwa Tanganyika; Tarehe 9 December 2011 tutasherehekea miaka 50 ya uhuru. Wanaosema miaka 50 ya uhuru wa Tanzania bara ni wanafiki wanaopotosha historia ya nchi yetu labda kwa maslahi yao. Naipenda TANGANYIKA yetu.
   
 10. n

  nyuki dume JF-Expert Member

  #10
  Dec 5, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 438
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Wako wapi wale waliokuwa wabunge miaka ya nyuma kati miaka 90 walioitwa G8 waliotaka taifa la Tanganyika liwepo, akina Njelu Kasaka,Ben Mkapa n.k mbona wamekaa kimya? au walichokuwa wanakitafuta wameishakipata ? Hawana tena haja na Utanganyika?
   
 11. M

  MAMENGAZI JF-Expert Member

  #11
  Dec 5, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 781
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Mi ninachofahamu Tanzania iwe bara au visiwani ina miaka 47, Tanzania bara ilipata uhuru kutoka wapi? Lini?

  Tunataka Tanganyika yetu bana, huu uchakachuaji wa mpaka nchi haukubaliki hata kidogo.
  TANGANYIKA my country, where are you?
  wamefisidi mpaka uhuru wako uliodai toka kwa mkoloni lol.
   
 12. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #12
  Dec 5, 2011
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,497
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
 13. O

  Omulangi JF-Expert Member

  #13
  Dec 5, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 1,026
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Huu muungano unaunganisha nini na nini eti? Ni Zanzibar na Tanzania bara? Ni Tanzania visiwani na Tanzania bara? Ni Tanganyika (iliyokufa) na Zanzibar (iliyo hai). Na hapo mfu anaweza kushikamana na aliye hai? Nakosa jinsi ya kufanyan reasoning nisaidie tafadhali.
   
 14. B

  Barphomet Member

  #14
  Dec 5, 2011
  Joined: Nov 7, 2011
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  jamani hivi bado tunahitaji kujiuliza utanganyika na uzanzibar? leo hii ulaya mataifa makubwa yanaungana sisi bado tunawaza kujitenga kweli tutaweza kuwa na africa union? matajiri na wenye nguvu wanaungana nyie maskini na dhaifu mnatengana :spy:?
   
 15. mgen

  mgen JF-Expert Member

  #15
  Dec 5, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 15,148
  Likes Received: 1,882
  Trophy Points: 280
  Wakuu, kuna haja na ni wakati muafaka wa kuhoji na kuitafuta haki hii ya Utanganyika Mahakamani! Jukumu hili tuwawezeshe wanasheria waangalie Jinsi! Huu muungano wa kishirikina wa kuchanganya udongo kwenye vibuyu na kuumwaga baharini na kuitoa kafara mama yetu Tg, ufe! Naomba mwenye wazo elekezi alete lifanyiwe kazi wana GrTh!
   
 16. J

  JRutenge New Member

  #16
  Dec 5, 2011
  Joined: Nov 26, 2011
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Upande huu wa muungano (bara) hakuna nchi wala serikali kwa sasa. Hati ya muungano ilitegemea masuala yasiyo ya muungano kwa upande huu wa Tanganyika yashughulikiwe na nani!!? Waziri wa Maliasili wa serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania anawezaje kushughulikia fukwe, misitu, mbuga za wanyama, milima, na vitu vingine ambavyo sio masuala ya muungano vilivyoko upande wa bara!?

  Kama waziri wa madini wa serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ndiye pia waziri wa madini wa serikali ya Tanganyika, kwa nini basi asiwe pia waziri wa madini wa serikali ya umoja wa kitaifa ya Zanzibar!?


  Miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika sio suala la Muungano, na kwa vyovyote vile halimuhusu Waziri wa Ulinzi wa sasa, Waziri wa Mambo ya Ndani wa sasa, Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa sasa na wengine wengi ambao ni raia wa Zanzibar.


  Serikali imeamua kutumia bendera ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, nembo ya taifa, wimbo wa taifa, Shirika la Utangazaji la Taifa, watumishi wa serikali, ofisi, vifaa na magari ya serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kusherehekea miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika. Je, hii ni sawa?


  Kitu kinachokera zaidi ni namna tunavyoharibu historia huku tukijua wazi kwamba watoto na wajukuu zetu wanafundishwa somo la Historia mashuleni. Hivi tunakifundisha nini kizazi hicho tunapotangaza miaka 50 ya uhuru huku tukionesha picha za marais wanne na miaka waliyoongoza Tanzania (au sijui ni Tanganyika au Tanzania Bara)!?

  Ni dhahiri kuwa kama tungekuwa na serikali ya Tanganyika mkanganyiko huu usio na ulazima usingetokea. Kwa nini tuogope kuujadili muungano wetu wenyewe tuliouunda kwa masilahi yetu na matakwa yetu wenyewe chini ya viongozi wetu wakuu wa nchi!?

  Kuna matangazo huwa yanaoneshwa kwenye runinga yakizungumzia namna ya kutatua matatizo ya kimahusiano kwa kuvunja ukimya. Huu ni wakati wa Tanganyika na Zanzibar kuvunja ukimya na kuizungumzia ‘ndoa’ yao kwa kuwa nina uhakika ‘walioana wakiwa wadogo’, kabla hawajawa na uwezo wa kupambanua maisha na kufanya maamuzi sahihi. Ni wakati wa kujadili ni mfumo gani wa ‘ndoa’ nchi hizi mbili ziwe nao. Ni wakati wa kuacha kupotosha historia yetu kwa kusherehekea tusichokijua. Na hiyo ndiyo kazi ya elimu tuliyoigharamia au kugharamiwa na ndugu zetu au serikali.


  Bila hivyo tutaendelea kuimba miaka 50 ya uhuru bila kujua ni uhuru upi, wa nchi ipi haswa, ulipatikana lini na wapi, na kwa nini tunausherehekea.


  Mungu atuongoze.
   
 17. t

  tisa desemba JF-Expert Member

  #17
  Dec 5, 2011
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 439
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  HATUTENGANI, Tanganyika is a sovereignty state it should be recognized.
  ULAYA wanaungana na haki za nchi zinalindwa, fuatilia...
   
 18. Maarifa

  Maarifa JF-Expert Member

  #18
  Dec 5, 2011
  Joined: Nov 23, 2006
  Messages: 2,880
  Likes Received: 1,049
  Trophy Points: 280
  miaka 50 uhuru wa Tanganyika ndo Mwanzo wa kurejeshwa Tanganyika yetu. Muungano siutaki hauna Faida, haufaia ni wa wakubwa!!. nasema siutaki. Naipenda Tanganyika.
   
 19. s

  semako Senior Member

  #19
  Dec 5, 2011
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 102
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tuungane tuitetee tanganyika yetu,mbona zanzibar ipo
   
 20. i

  ibangu Member

  #20
  Dec 5, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nadhani ni kwa interest ya Wazanzibari kuwa kuwe ka Serikali ya Tanzania, vinginevyo iwapo serikali ya Muungano ndiyo hiyo hiyo serikali ya Tanganyika, haiwezekani basi Mzanzibari kuwa Rais wa Serikali hiyo kwani atakuwa Rais wa Tanganyika pia. Nadhani wanaobisha hawajaliona hili kwa upeo. Kama Serikali ya Tanganyika iko ndani ya Serikali ya Muungano, basi Rais wa Muungano sharti awe Mtanganyika - vinginevyo utakuwaje na mtu za Zanzibar aongoze Serikali ya Tanganyika? Hebu fikirieni. Vinginevyo, Mzanzibari asiruhusiwe tena kuwa Rais wa Tanzania.
   
Loading...