Utata wa malipo kwa mke wa Mudhihiri

Utata wa malipo kwa mke wa Mudhihiri

OTIS

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2011
Posts
2,252
Reaction score
833
Mbunge wa zamani wa jimbo la mchinga ndg Mudhihiri ambae kwa sasa ni mjumbe wa bodi ya korosho Tanzania, amekuwa akipokea malipo ya matunzo kwa ajili ya ulemavu wake wa mkono uliokatika mwaka 2008.

Malipo haya yamekuwa yakipokelewa na mke wake ili kumtunza kwa ajili ya kufanikisha majukumu yake kama mjumbe wa bodi.

Suala hili limeibua utata wa hali ya juu kwani yameibuka maswali mengi ilhali hakuna jawabu hata moja.

Ni sheria au kanuni gani zimetumika kuidhinisha malipo haya kwa mke wa Mudhihiri kisa ni mlemavu?

Ni majukumu gani mazito yanayohitaji kugharamiwa matunzo na serikali?

Malipo ya aina hii yanafanyika kwa wafanyakazi wa kada zote walio na ulemavu wa viungo au hili lamuhusu Mudhihiri peke yake.

Mudhihiri alivunjika mkono tangu 2008 akiwa mbunge,je bunge nalo lilikuwa linamlipa mke wake posho ya kumtunza mume wake?

Mudhihiri kwa sasa ni mjumbe wa bodi ya NSSF, kutakuwa na usalama huko?

Nge nge ngeeeeeeeeee,tafakari.
 
Walemavu wote wa viungo nchi hii tuanze kwenda na wake/waume/ndugu zetu makazini kama wasaidizi wetu na tudai walipwe mishahara au posho kama mke wa Mudhihir Mudhihir!

Sijawahi kuona sheria ya nchi ikutungwa kwaajili ya mtu mmoja tu!
 
OTIS

Afadhari umelisemea na hili ila wako wengi wa aina hii bahati mbaya sina tangible evidence ningekutajia
 
Last edited by a moderator:
Ndiyo mana hawataki kutuliapa tena NSSF na PPF zetu mpaka tujifie ili watoo waambiwe walete doc wakitegemea wengi watakaosa tu na watakuwa wamezizungusha....
 
Nimeingia leo ngoja kamba initoke kwanza miguuni.
Mwongozo wana jf.
 
Hata mimi sielewi kwanini Watanzania ni Masikini BY kikwete!:frusty:
 
Kuna ulaji sana kwenye hizi bodi.
 
Kama Mudhihir hajiwezi hadi apate msaidizi ni lazima afanye iyo kazi?
Hakuna watu wengine wa kufanya iyo kazi?
 
Karibu viongozi wote wanapata ulaji wa namna hii ila tatizo haijulikani,nchi inatafunwa na wachache bila wenye nchi ambao ni wananchi kujua.
 
Kwani lile fao la ulemavu linakuwaje??

Hili si fao la ulemavu.
bali ni malipo kwa msaidizi wake ambae ni mkewe.
na fungu hili latoka bodi ya korosho.sasa jiulize kama bodi ya korosho nayo yatoa mafao siku hizi,.
 
Kama Mudhihir hajiwezi hadi apate msaidizi ni lazima afanye iyo kazi?
Hakuna watu wengine wa kufanya iyo kazi?

kumbuka huyu ni mjumbe wa bodi tu
na wala hana kazi zozote za kiutendaji.
vipi kuhusu walemavu waliojiriwa kama walimu,wauguzi nk
 
Hili si fao la ulemavu.
bali ni malipo kwa msaidizi wake ambae ni mkewe.
na fungu hili latoka bodi ya korosho.sasa jiulize kama bodi ya korosho nayo yatoa mafao siku hizi,.

Kumbe ni malipo kutoka bodi ya korosho?? Huu kweli ni ufisadi.
 
Back
Top Bottom