mitale na midimu
JF-Expert Member
- Aug 26, 2015
- 10,420
- 17,701
Asante kwa kuquote mkuuPole sana, naona umeifunga akili yako
Asante kwa kuquote mkuuPole sana, naona umeifunga akili yako
Watu wa mfano wa Bwana Kiranga hata kama laiti Mungu angeliumba ulimwengu anayeutaka bwana Kiranga basi yeye na mfano wa watu wa kama yeye wangelimpinga Mungu wazi wazi kabisa. Kwa sababu tungelikuwa hatuna mapungufu, tungelijiona tumekamilika. Rejelea watu wa Qaumu Aad, walimwambiaje Mtume wao Hud a.s walivyopewa uwezo unaofanana anaoutaka bwana Kiranga.
Walimwambia Hud a.s " Man ash' shaddu minna quwa" Ni nani mwenye nguvu kuliko sisi? Tumekamilika sisi Hud, utatuambia nini? Kuhusu Mungu? Fanya unayotaka kuyafanya wewe pamoja na huyo Mungu wako. Lakini usichoke kumpa darasa, inawezekana akabadilika na akawa anapendeza zaidi kwa Mungu kuliko sisi wenyewe.
HAWA WATOTO WAPO ILA NI WATOTO TU AMBAO WANAZALIWA NA UWEZO MKUBWA WA AKILI...KWA AKILI ZILE WAKIELEKEZWA POPOTE WANAFIT....yaani endapo akielekezwa kwenye masomo ya shule atafit na alielekezwa kwenye dini pia atafiti...Mfano mmoja wapo kuna hili la uwepo
wa hawa watoto wa
ajabu ambao huitwa SHARIF. Binafsi nimekua na nimeweza
kushuhudia mmoja wa
watoto hawa wa ajabu.
Akina Sharif huwa ni watoto wa ajabu ambao
huzaliwa na karama ya kujua
mambo mengi ya kidunia na kidini ktk namna ya
ajabu kabisa. Na wengi
kama si wote huzaliwa ktk familia za kikristo na
hulia sana
wakiongozona na wazazi wao kuelekea kanisani. Nukta hii hunifikirisha sana.
Kuhusu aina hii ya watoto ipo tofauti kidogo mdugu. Hawa si kuwa ni jitihada za mzazi HAPANA. Huzaliwa wakiwa wenye kuhubiri na kuijua Quran bila hata ya kufundishwa.
Hiko kitu hakiwezekani.. Sasa ataongea lugha ipiMkuu edwayne. Mimi nimeyashuhudia maajabu haya kwa macho yangu. Kama pia unamjua yule anayeitwa Said John aliyezaliwa Arusha. Fuatilia kisa chake na utaona mambo mengi yenye kushangaza.
Yesu aliongea akiwa tumboni.Hamna mtoto anayezaliwa anaweza kuongea hilo jambo halijawahi tokea
Sheriff alieongelewa hapa ni polisi.I shoot the Sheriff - Bob Marley
Si ndio uislam sasa...
Yakobo : Mlango 1
27 Dini iliyo safi, isiyo na taka mbele za Mungu Baba ni hii, Kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao, na kujilinda na dunia pasipo mawaa.
Wale wote Ni scam .. hakuna shekhe sharifu Kama namna ambavyo jamii huwa inaaminishwa ile Ni michezo jombaaMkuu edwayne. Mimi nimeyashuhudia maajabu haya kwa macho yangu. Kama pia unamjua yule anayeitwa Said John aliyezaliwa Arusha. Fuatilia kisa chake na utaona mambo mengi yenye kushangaza.
Yesu aliongea akiwa tumboni.
Habari wanajamvi,
Kwa muda mrefu nimekua nikitatizwa na jambo la
imani kwa upande wa
dini hizi mbili za uislam na ukristo. Awali ya yote
ningependa
kueleweka kuwa nimezaliwa ktk familia ya kiislam.
Ningependa ku-stress
hapo kuwa sote tumejikuta ktk imani tulizonazo
baada ya kuzaliwa na
wazazi wenye imani husika.
Nirudi ktk lengo langu la uandishi. Binafsi, kuna
wakati niliwahi
kutatizwa na uwepo wa Mungu. Lakini kwa sasa
niweke wazi nakiri Mungu
yupo na ninaamini ana adhabu zake kwa wale
wanaowafanyia wengine
mabaya hapa ulimwenguni(nadhani hili linajibu hoja
ya wengi kwanini
Mungu atuadhibu anafaidika na nini?)
Utata wangu uliobaki kwa sasa ni juu ya ipi ni imani
ya kweli kati ya
UISLAM na UKRISTO dini ambazo zote zimekua
binafsi zikinitatiza hasa
ninapofanya kunasabaisha na historia mbaya ya mtu
mweusi hapa duniani.
Ni wazi dini hizi mbili zina historia mbaya au zina
nasaba ya moja kwa
moja na jinai mbaya tuliyowahi kufanyiwa waafrika
ya utumwa. Ni wazi
wamisionari walichangia pakubwa ktk kudhibiti na
kufanikisha ukoloni
kwa watu weusi hali ya kuwa wakijua kufanya hivyo
ni kumkosea Mungu na
watu weusi. Hivyohivyo mathalani tumewahi kusikia
mfano wa kikundi
kinachoitwa JANJAWEED cha waislam waarab wa
Sudan ambao wamekua wakiua
waislam
weusi kwa mrengo wa kibaguzi dhidi ya watu weusi.
Na mbaya zaidi jinai
hizi wamekua wakifanya kwa kujumuisha kuchoma
kitabu cha Qur'an
ambacho wao pia hukiamini na kukitumia. (Refer
Darfur Genocide for
clarifications)
Lakini hapo hapo huwa natatizwa na jambo moja
ambalo ndio hasa
ningependa tulijadili wanajamvi. Binafsi nimekua na
imani kubwa juu ya
uislam kuliko ukristo kwa kuangalia nukta kadhaa
ambazo zimekua
zikinifikirisha. Huwa ninaona kuna mambo mengi
ambayo Mungu amekua
akidhihirisha kupitia uislam na kufanya akili kufikiri
zaidi.
Mambo hayo yamejikita ktk maajabu ambayo
naamini wengi wenu mmewahi
kusikia na kushuhudia pengine. Nitaenda haraka haraka.
Mfano mmoja wapo kuna hili la uwepo
wa hawa watoto wa
ajabu ambao huitwa SHARIF. Binafsi nimekua na nimeweza
kushuhudia mmoja wa
watoto hawa wa ajabu.
Akina Sharif huwa ni watoto wa ajabu ambao
huzaliwa na karama ya kujua
mambo mengi ya kidunia na kidini ktk namna ya
ajabu kabisa. Na wengi
kama si wote huzaliwa ktk familia za kikristo na
hulia sana
wakiongozona na wazazi wao kuelekea kanisani. Nukta hii hunifikirisha sana.
Watoto aina hii
hufurahi na kulilia
kwenda msikitini. Maajabu ni mengi juu ya watoto
wa namna hii. Nimeorodhesha ajabu moja kati ya mengi.
Maajabu mengine nakumbuka zamani kidogo
niliwahi kusoma kwenye gazeti
la Alasiri juu ya binti aliyegeuka mnyama wa ajabu
kabisa baada ya
kupiga teke Quran aliokua anaisoma
mama yake. Licha ya juhudi za kumuombea yule
binti hakubadilika,
nafikiri picha za huyo binti mpaka hivi leo zipo.
Kisa kingine ni cha mbuzi aliyezaliwa na maandishi
ya aya za Quran
ubavuni huko Moshi. Pia kuna mtoto alizaliwa Urusi
kama sijakosea
ambaye alikua na maandishi ya Quran mwili mzima.
Kiukweli ni maajabu
mengi kati ya haya machache ambayo binafsi
yamekua yakinifikirisha
kiukweli na kujiuliza maswali mengi sana.
Kwanza najaribu kumuangalia mtu mweusi na
historia yake hapa
ulimwenguni dhidi ya dini hizi mbili kongwe. Kisha
natazama maajabu
haya yanayotokea yakiakisi dini ya Uislam na kubaki
na maswali yasiyo
na majibu. Naomba tujadili juu ya hili la maajabu ya
Mungu kwa kutoa
ishara hizi. Je, ni kweli Mungu anatoa ishara kudhihirisha Uislam kuwa njia ya kweli? Wewe binafsi mchangiaji una nini la kuongeza au una mtazamo gani juu ya haya machache niliyoandika?
Naomba waungwana tujadili kwa fikra huru bila
matusi wala kejeli. Kama huamini uwepo wa Mungu ni vema kuacha kuchangia chochote bali kutazama mjadala.
Huenda kama kuna litakalotuponza na kutupa adhabu kubwa mbele za Mungu ni kejeli na matusi dhidi ya imani za wengine kwa
kuona imani yako ni
bora kuliko ya mwengine na wakati huohuo kumtolea
hukumu mtu mwingine kwa sababu tu ya tofauti zenu za kiimani. Nimejaribu kuandika kwa mjumuisho lakini bila shaka maudhui ni yenye kueleweka.
Nawasilisha.