Kinachoendelea Kigoma kuhusu kifo cha dereva wa John Heche

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,180
Reaction score
17,646
Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa, Deogratius Mahinyila, amesema ni muhimu taarifa zote kuhusu mazingira ya kifo cha marehemu Maradufu kuwekwa wazi ili kuondoa sintofahamu. Mahinyila ameeleza kuwa marehemu alikutwa na fedha taslimu kiasi cha Tsh. 428,000 ambazo alikabidhiwa, huku pia akibainisha kuwa mwili wa marehemu ulikuwa umetokwa na damu mdomoni.

1782992515297.png

Amesema wataalamu wa uchunguzi wa maiti (pathologists) waliowasili usiku wa kuamkia leo kutoka mikoa ya Mwanza na Geita walikuwa bado hawajaanza kufanya uchunguzi hadi majira ya saa nane mchana. Aidha, Mahinyila amesema walipata taarifa kuwa mtaalamu mwingine wa uchunguzi kutoka Dodoma anatarajiwa kuungana na timu iliyopo kwa ajili ya kuendelea na uchunguzi huo.

Soma: Dereva wa John Heche akutwa amefariki chumbani Kigoma

1782994995522.png

Mahinyila pia amehoji hatua ya wataalamu hao kupelekwa katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Simon Sirro, mara baada ya kuwasili asubuhi ya leo. Amesema haijulikani kikao hicho kilihusu nini na kama ni sehemu ya utaratibu wa kawaida wa kazi zao, huku akieleza wasiwasi kuhusu kauli ya Sirro aliyenukuliwa na Clouds TV akisema kuwa kwa uzoefu wa kipolisi, kifo cha Maradufu kinaonekana kuwa cha kawaida.

Amesisitiza kuwa muda ni mwalimu mzuri na ukweli utajidhihirisha kwa wakati wake, akibainisha kuwa wao wataendelea kuwepo Mochwari ya Maweni, Kigoma hadi uchunguzi utakapokamilika. Mahinyila amesema matokeo ya uchunguzi yatasaidia kuweka kumbukumbu sahihi ya tukio hilo na kutoa majibu ya maswali yanayoendelea kuibuliwa.

1782992396815.png
 
Simu yake ya mkononi nani anayo?

Je ilikutwa kwenye crime scene?

Je wahudumu wa hapo lodge walisikia purukushani zozote usiku huo?

Je waliona marehemu akiingia na mtu chumbani?

Kwanini wavunje mlango na kwenye lodge kuna funguo za ziada?
 
nadhani mtu aliempatia fedha hizo marehemu, anaweza kua shahidi muhimu zaidi wa mazingira alipokua anamkabidhi kitita hicho cha fedha, na watu ambao alikua nao wakati wa makabidhiano ya fedha hizo.

Ni muhimu sana pia,
kufahamu zilipoteka fedha hizo, na zilikua kiasi gani tofauti na hicho alichokutwa nacho marehemu,

na lengo la fedha hizo lilikua nini, na dhumuni la kumpatia fedha hizo dereva lilikua ni nini?🐒

R.I.P Suez Daniel Maradufu
 
Hayo maswali ndiyo wahalifu huyafanyia kazi kwa bidii ili wasikamatike.But,there will be a bit of an alibi to pin them down kukiwa na uwazi.
 
nadhani mtu aliempatia fedha hizo marehemu, anaweza kua shahidi muhimu zaidi wa mazingira alipokua anamkabidhi kitita hicho cha fedha, na watu ambao alikua nao wakati wa makabidhiano ya fedha hizo.

Ni muhimu sana pia,
kufahamu zilipoteka fedha hizo, na zilikua kiasi gani tofauti na hicho alichokutwa nacho marehemu,

na lengo la fedha hizo lilikua nini, na dhumuni la kumpatia fedha hizo dereva lilikua ni nini?🐒

R.I.P Suez Daniel Maradufu
Mkiwa kwenye ziara kulewa fedha ni lazima (per Diem). Kula, kulala inabidi ulipe.
Sasa unapouliza lengo la kumpa fedha dereva ni nini mbona unaleta u CCM?
 
RC Sirro - mkuu wa kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, amesha'pre-empty ripoti ya surbodinates wake - POLISI, unategemea waje na ripoti inayopingana na alichoripoti wakati wa mahojiano yake asubuhi ya leo??
 
Back
Top Bottom