Utata juu ya mwanaJF Ontario

Kati ya vitu vilivyonifanya kuielewa (kuvipenda/kuvutiwa navyo) sana JF miaka ya 2017 ni Ontario na Forex. Sema tu hyo issue nlikuwa naiona JF tu na nlikuwa guest.
 
Ukiona elimu ni ghali wanasemaga jaribu ujinga ati!
Sent using Jamii Forums mobile app
 
" hakuna mtu ambaye siye tapeli" futa hii kauli , au hujui kuwa utapeli/ wizi ni laana?

Sent using Jamii Forums mobile app
Watu wote ni matapeli, hata ww ni tapeli ushawah kumtapeli mtu Kwa nyakat fulan , Ila Kwa Sabab Ontario ana gain more Kwa kile tuanchokiita ni tapel bas tunamuonea nongwa , watu wanafanya utapeli kwenye mahusiano Yao, kwenye mapenz huko watu wanatapeliana kama kawa, huko makanisan watu wanatapeliana , Kwa waganga mtu anatapeli, kwenye maswala ya biashara ndo kabisaaa .....
 
I saw some of this guy's whatsapp screenshots, there was Machiavellian undertone in them.
He was trying to control them and exploit their weaknesses.

Ukisoma nyuzi zake hapa JF unaweza kuona ni mpambanaji sana, na ni kweli ni mpambanaji kwa ajili yake. Hilo sio kosa na wala havunji sheria bali anatumia fursa, uvivu wa watu kutafuta taarifa, tamaa ya mafanikio ya haraka, procrastination and lack of pragmatism.

Mtu hawezi kusoma kitabu cha maarifa flani akamaliza mwenyewe bila kitu cha kumsukuma hivyo anakatisha njiani na mwisho anakosa mafanikio ktk malengo yake.
Anapotokea mtu anaeweza kuwapa matumaini ya kuwawezesha kufanya hayo wanayo shindwa, akawajaza hamasa basi huwateka akili kwa manufaa yake.
Hiyo ni mbinu ya kibiashara kwa kucheza na saikolojia ya watu.

Forex ni legit kabisa sio utapeli, unatakiwa usome kisha ufanye mwenyewe lakini unakuta mtu anataka afanyiwe speculation, na mambo mengine ili yeye asiumize kichwa au asikose muda wake wa kutembelea mitandao ya kijamii n.k.
Mtu anamlipa Ontario mafunzo ya kitu flani pesa nyingi wakati mafunzo hayo hayo yapo bure kibao kwenye mitandao kama youtube n.k.

Kifupi wanataka mtu wa kuwafanyia kazi au wa kuwasimamia kutekeleza malengo yao sababu hawana nidhamu ya kujisimamia na kujali muda.
 
Kwani wewe ndio mnyama gani ndani ya Serengeti πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…