Utaratibu wa mwanamke kupewa pasu kwa pasu baada ya talaka bila wao kuchangia ni wa Hovyo na kandamizi kwa wanaume?

Hii hbr ya kugawana mali pale inapotokea mmeachana mali inayogawanywa si ni ile ambayo ilipatikana mkiwa pamoja au inahusu hata mali ambazo alikukuta/alikuwa nazo?
 
Asilimia kubwa ya wanawake ni chanzo cha stress nyumbani, kwahiyo ondoa suala la "kuondoa stress"! Kukuzalia watoto?! Watoto gani?! Asilimia kubwa ya watoto wanaegemea na kutoa misaada zaidi kwa mama zao kuliko kwa baba zao! Sasa hapo kanizalia mimi au amejizalia mwenyewe?! Angetafuta mali huko kama walivyotafuta wanawake wangapi?! Hata ukiangalia orodha ya matajiri duniani, imetawaliwa na wanaume kwa zaidi ya 90%, na ukiona wanawake kwenye orodha basi ni ama za kurithi kwa baba zao wanaume au za kuachiwa na waume zao wanaume!!
 
Hakuna cha cost wewe, mazoea tu na ile kutaka kuendana na jamii. Siku hizi watu kibao hawaoi na bado wanaishi happier life kuliko hao walio kwenye ndoa ndoano! Mtu kama huna uwezo wa washing machine, kuna madobi kila kona! Kama huna uwezo wa kupika, ma-house girl 50K tu kwa mwezi, na hivyo ni viwango vya mijini kama Dar!! Hao watoto wakishakuwa wakubwa wanakuwa na msaada zaidi kwa mama kuliko kwa baba, kwahiyo hao wanawake hakuna wanayemlelea bali wanayalea maisha yao ya baadae na msitake kuonesha kwamba eti ni bonge la kazi!!!
 
Ndiomana wanachinjwa ovyo na waume zao mtu ana pigwa anataka kufa hataki kwenda eti anasubiri talaka ili wagawane Mali kuondoka kumwachia mumewe zile Mali yupo ladhi apigwage tuu na bwana ake
 
Najaribu kutafakari mtoa mada ametoka mkoa au ni kabila gani? kuna makabila hapa nchini na tena mengi yana mfumo dume uliopitiliza kuwa mwanamke hana chake hazalishi.
Wakati wewe unakwenda kazini yeye akikaa nyumbani anakupikia ugali unafikiri hapo yeye hachangii.Wakati wewe unakula starehe yako usiku na yeye unamuwekea kiumbe tumboni anakibeba kwa miezi tisa huo sio mchango wake?.
Suala la watoto ni hivi kama ni wadogo chini ya miaka saba sheria inasema wazi wawe chini ya uangalizi wa baba.
Muwaheshimu wanawake mwanamke akiamua kukuzimisha dakika sifuri au akakkufanyia kitu hata ukafa taratibu bila ushahidi wowote uwezo huo anao wanatembea wameshikilia roho zetu tuwaheshimu hawa viumbe.
Nchi zingine kama Australia na New zealand mwanamke anapewa asilimia 75% ole wako umuache huu kwetu tuna nafuu sana ndio maana wazungu wengine wanakuja na kupenda kuoa waafrca wenye ajabu eti mtu anakupa maji ukinywa amepiga magoti hadi umalize ndio ananyanyuka.
 
Ni shida
 
Mke wangu nilisha mwambia kama atataka kuachana nami sawa ila siwezi kugawana mali.
Abebe kila anachoona au nitoke nikaanze maisha mapya na nyumba namwachia.
Nashangaa wanaume wanalilia mali na wanawake.
Unakufa anamiliki vizuri
 
Kwahiyo mwanamke ni mfanyakazi (mtumwa) anayestahili kulipwa pasu pindi tukiachana?
Kama share anaipata kwasababu ya kulea watoto na kupika. Je, mimi silei hao watoto?
Akiondoka home siwezi kumwajiri house girl akafanya majukumu yote kwa imakini kwa ujira mdogo wa elfu 50 ?.
Siku moja wife alizingua (alileta wivu uliopita mipaka). Nikampa nauli asepe kwao. Nikamwambia na hati ya nyumba chukua Mimi ni mwajiriwa wa serikali tajipanga tajenga nyumba nyingine nzuri wewe utaishi kwa mateso kwenye nyumba nilioijenga kwa mshahara wangu. Nyumba haitakupa ugali wala chips. Mimi hata nikisema leo nikapange nina uhakika wa ugali.
Akaomba msamaha
 
Shikamoo Brother!!!!

Ndo maana huko huko Ulaya na Marekani tulikoiga hizi sheria zisizo na haki, hivi sasa watu wameshtuka na kusaianiana prenup kabla ya kufunga ndoa!

Prenup ndio solution maana wake zetu sasa ni kama wapalestina wanaangalia sana mali...wakishindwa kukurestisha wanaanzisha migogoro mgawane mali pasu kwa pasu.
 

Haielewi huyoo! Nilitaka kuandika same thing sema umeniwahi.
Zile Garama za kukupikia, kukufulia,!kukulindia nyumba na kukutunzia watoto malipo yake ndio hiyo pasu kwa pasu unayoona ni nyingi.
 
Acha uongo mkuu toka lini ulisikia watu wakigawana watoto,?
Kwamba mnagawana watoto, watoto wengine wanakua wanamuhusu baba tu na wengine wanamuhusu mama tu ,
We ulisikia waapii? A cha uongo
Nazani amemaanisha wengine wanaenda kwa baba wengine kwa mama, kama ni mdogo sana anabaki kwa mama.... kama wakubwa wanachagua au inaangaliwa nani anaweza kuwatunza
 
Haielewi huyoo! Nilitaka kuandika same thing sema umeniwahi.
Zile Garama za kukupikia, kukufulia,!kukulindia nyumba na kukutunzia watoto malipo yake ndio hiyo pasu kwa pasu unayoona ni nyingi.
Hause girl nae apewe robo labda maana wanaume wanalipia House girl ambao wanaofanya shughuli nyingine za nyumban
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…