Utaratibu wa mwanamke kupewa pasu kwa pasu baada ya talaka bila wao kuchangia ni wa Hovyo na kandamizi kwa wanaume?

safuher

JF-Expert Member
Feb 11, 2019
11,161
15,839
Wakati wanaharakati wakihangaika kuwainua wanawake na kujifanya kuwatetea ndipo wanazidi kuwashusha na kuwakandamiza wanaume.

Hali inakokwenda kuna wanaharakati watajitokeza nao kuwa wanatetea wanaume dhidi ya ukandamizaji unaofanywa dhidi yao.

Mwanamke kutaka pasu kwa pasu ilhali hajachangia kinachostahiki kuwa pasu kwa pasu huo ni unyama kwa wanaume na pia kuzidi kuwalegeza wanawake.

Unapowatafutia shortcut wanawake manake unazidi kuwadumaza zaidi ili waje kuwa watu hatari zaidi katika jamii.

Kama ishu ni kwamba naye kalea watoto basi apate hao watoto wote wawe wake mana ndo nguvu kubwa ilikuwa huko.

Mwanamke apewe chochote lakini sio pasu kwa pasu wakati yeye hakuchangia gharama yoyote ya mali katika kukuza mafanikio ya mume.

Kama alichangia na mume pasu kwa pasu(nusu mume nusu mke)basi HAINA SHIDA IWE PASU KWA PASU,kama hakuchangia basi iangaliwe tu kipi apewe akaanzie maisha na sio mambo ya kuwafanya wanaume vitega uchumi.
 
Ndugu hao viumbe achana nao embu vuta picha mtu anaamka usiku anaendaa basi hajabeba ata buku ya soda kavaa tu kimahaba akifika huko ni mauno tu dinner vinywaji naul atapata huko huko we unaona huyo ni kiumbe wa kushindana nae.

Mm nimeshuhudia demu kaolewa baada ya mwez karud kwao anadai talaka kuja kuchunguza kumbe kapata bwana mwingine na mama yke ye anasubir mahali ndo maana akawa hampi suppprt mumewe.
.
Kaa mbal na mwanamke
 
Wewe naona ni mjinga kwahiyo ulizania mwanamke ni housegirl wako akupikie akufulie,akulindie nyumba yako akutunzie watoto miaka yote halafu useme hana haki ? Kwani yeye hawezi kwenda kufanya vibarua akajenga mji wake kwa huo muda wote miaka yote ulioishi naye? Kwanza ujue mwanamke alitakiwa azidishiwe robot tatu
 
Sasa mahpusegirl ndo wanakuwa na haki ya kulipwa kwa mujibu wa kazi walizofanya hapo nyumbani,

kwa hiyo wewe unapotaka mwanamke awe na haki ya kulipwa tena pasu kwa pasu kwa kazi alizokuwa akifanya maana yake unakubali kuwa MKE NI HOUSEGIRL aliyechangamka.

Maana kwa ambao sio mahousegirl wanafanya kazi za nyumbani na hawalipwi wala hawahitaji malipo mfano wewe ulikaa kwa wazazi wako ukafanya kazi mbalimbali ulipoondoka kwa wazazi ulidai chochote kwa kazi ulizofanya?

Bila shaka hukudai maana yake ungedai ulipwe maana yake wewe ungekuwa ni houseboy au housegirl

Kwa hiyo kutaka mwanamke alipwe kwa kuangalia uzito wa kazi aliyofanya maana yake mke kwa muda wote alikuwa ni housegirl.

Lakini pia Kwa hoja hizo zako maana yake mwanaume naye ni mtumishi wa mke miaka yote anajituma na kuhangaika kulisha familia, haiwezekani tukiemda kwa mfumo huo mzee.
 
Tukisema kuoa ni ujinga mnaanza kulialia ooh mbona wewe ulizaliwa, tuendelee kuwaonya au tuwaache tu!!
Solution sio tuache kuoa bali solution tuzikane sheria kama hizi.

Tukiacha kuwaoa tutakuwa tunatembea nao tu,shwria zitatufata huko huko zitatungwa sheria za uchumba kati ya mwanamke na mwanaume,inakuwa hatujakimbia tatizo.
 
Kwahiyo na nyie mnataka muanze harakati za Beijing kuandamana na mabango mtetee haki zenu!

Huko ni kulialia, mwanamme ni kiongozi siku zote, na hata hizo sheria za wanawake zilisimamiwa na wanaume.

Cha kufanya, hakikisha mkeo anazalisha kwa namna ambayo siku ikija ya pasu iwe pasu kweli kweli, au lah, uwe 'tayari' kiasi kwamba isitokee talaka.
 
wahiyo na nyie mnataka muanze harakati za Beijing kuandamana na mabango mtetee haki zenu!
Kama umehitimisha hivyo baada ya kuelewa sawa.
Huko ni kulialia, mwanamme ni kiongozi siku zote... na hata hizo sheria za wanawake zilisimamiwa na wanaume
Katika sifa ya uongozi basi ni kukemea linaloenda kinyume kama hivi mimi nimekemea.
 
Order iko hivi: MUNGU - KRISTO - MWANAUME - MWANAMKE.

hakika Yesu ni Bwana na Mwokozi
Screenshot_20210112-195809.jpg
 
Nashangaa kbs mtoa mada yani unasema kama ni hao watoto amezaa ndio haki yake aondoke nao. Nafikiri ingekuwa vizuri na wewe ungepewa nafasi ya mwanamke ujaribu kubeba ujauzito miezi 9, kila ukazae kwa uchungu, uanze kumlea huyo mtoto mpk awe mkubwa ndipo ungeona kazi ya Mwanamke kama hana haki ya kugawana nusu kwa nusu na mwanaume.
 
Nashangaa kbs mtoa mada yani unasema kama ni hao watoto amezaa ndio haki yake aondoke
Naam mkuu kama wao kigezo cha kugawana nusu ni hoja ya kulea watoto basi ilistahiki zaidi kila mmoja achukue kile ambacho kawekeza sana nguvu zake huko.

Tokea lini kulea watoto kukaendana na kutafuta mali.

Kutafuta mali kutabaki kutafuta mali,na kulea watoto kutabaki ni kulea watoto,hapo hakuna kitakachosimama kikawa mbadala wa mwenzie.

Mwanaume katumia nguvu nyingi kutafuta mali maana yake mpasuko ukitokea yeye ndo atakuwa na sehemu kubwa ya mali.

Mwanamke alitumia nguvu kubwa kulea familia maana yake mpasuko ukitokea yeye mwanamke atachukua sehemu kubwa ya kulea familia(watoto)huku huduma zikiendelea kutoka kwa baba.

Sasa kufananisha kati ya kulea watoto na kutafuta mali hilo sio jambo sahihi,kila kimoja kina hadhi yake havifanani katu.
Nafikiri ingekuwa vizuri na wewe ungepewa nafasi ya mwanamke ujaribu kubeba ujauzito miezi 9,
Mimi naelewa shida wanazopitia wanawake lakini shida hizo hata kama ukawapa mali pasu kwa pasu bado haziondoki,ndio maana mwanamke tajiri nae bado atakuwa na uchungu ule ule kama huyu mama amnaye anasubiri pasu kwa pasu.

Hivyo tabu za mwanamke haziondoki kwa kupewa pasu kwa pasu,hizi ni tabu za asili kaumbiwa na Mola wake.
9, kila ukazae kwa uchungu, uanze kumlea huyo mtoto mpk awe mkubwa ndipo ungeona kazi ya Mwanamke kama hana
Bado sio hoja mkuu kwa sababu zifuatazo..

Moja pasu kwa pasu haiondoi uchungu wa mama kulea.

Mbili kulea mtoto ni kulea mtoto na kutafuta mali ni kutafuta mali hakuna mbadala,kila mmoja aheshimiwe kwa mchango wake dhidi ya mwenzie.

Tatu suala la kupata mtoto wote wamejitahidi wakawekana mimba,baba kajitahidi kuhudumia mambo mbali mbali hivyo katika makuzi ya mtoto wote wamechangia,kazi ya mwanamke ni kuzaa na kulea na hayo yote asili ndio inafanya kazi.

Sasa huwezi kufananisha baina ya haya mambo mkuu
 
Shida ni hiyo pasu kwa pasu au?!!
Naona hata haitoshi kufidia maisha ya mwanamke uliyemfanya mke. Ukimfanya mke akawa tu nyumbani akikuondolea stress na kukuzalia watoto, muda ambao kama usingemuoa angekuwa anatafuta mali huko. Unadhani yeye mali atapata wapi. Na ndio maana mnagawana kila kitu hadi watoto.
 
Na ndio maana ndoa hua naitafsiri kama jela

Kwasababu migogoro mingi ya ndoa inashindwa kufikia breakup na kujikuta wakiendelea kuishi kwa kuvumilia maumivu kutokana na hii hatua ya mgawanyo wa mali kutokua tayari kuikabili maana siku zote mwanaume ndiye anaumia zaidi
 
Tunaumia zaidi wanaume kwa utaratibu huu mkuu.

Kulea watoto ni kulea hakuna mbadala wa hilo.

Na kutafuta mali ni kutafuta hakuna mbadala wa hilo.

Kulea hakuwezi kubadilika kukaja kuwa mbadala wakw ni mali wakati wa talaka,huku ni kutuumiza wanaume hasa.
 
Wewe naona ni mjinga kwahiyo ulizania mwanamke ni housegirl wako akupikie akufulie,akulindie nyumba yako akutunzie watoto miaka yote halafu useme hana haki ? Kwani yeye hawezi kwenda kufanya vibarua akajenga mji wake kwa huo muda wote miaka yote ulioishi naye? Kwanza ujue mwanamke alitakiwa azidishiwe robot tatu
aisee
 
Shida ni hiyo pasu kwa pasu au?!!
Naona hata haitoshi kufidia maisha ya mwanamke uliyemfanya mke. Ukimfanya mke akawa tu nyumbani akikuondolea stress na kukuzalia watoto, muda ambao kama usingemuoa angekuwa anatafuta mali huko. Unadhani yeye mali atapata wapi. Na ndio maana mnagawana kila kitu hadi watoto.
Acha uongo mkuu toka lini ulisikia watu wakigawana watoto,?
Kwamba mnagawana watoto, watoto wengine wanakua wanamuhusu baba tu na wengine wanamuhusu mama tu ,
We ulisikia waapii? A cha uongo
 
Back
Top Bottom