Utaratibu wa Kumkomboa mtoto aliye zaliwa nje ya ndoa, kwa anayejua kutokana na kabila lake msaada tafadhali

Brightg

JF-Expert Member
Sep 24, 2013
366
1,000
Naombeni utaratibu wa Warangi, Wabondei, Wasambaa, Wachaga au Makabila mengine yanayo fanania kwa anaye fahamu kuhusu KUMKOMBOA mtoto aliye zaliwa na baba mwingine. Mfano nimeoa mke ambaye ana mtoto 1 na hajawahi hudumiwa na baba yake hadi umauti unamkuta baba yake, ila Wazazi wa Marehemu wako hai sasa nahitaji wamkomboe binti yao ili awe rasmi kwao.

Sasa utaratibu ukoje na huwa wanatoa nini na nini kumkomboa huyo mtoto zaidi sana ukizingatia mazingira ya kwao au baba wa mtoto au mama wa mtoto.
 
G'taxi

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
4,862
2,000
Unamkomboa kweni ametekwa? We fata mtoto wako na wakikataa muache akikua atakuja, maswala ya kumtolea mtoto wangu mwenyewe pesa binafsi siliafiki
 
Sim Card

JF-Expert Member
Dec 30, 2019
863
1,000
Unamkomboa kweni ametekwa? We fata mtoto wako na wakikataa muache akikua atakuja,maswala ya kumtolea mtoto wangu mwenyewe pesa binafsi siliafiki
Mkuu nafikiri kama mimemwelewa vizuri anataka kumkomboa mtoto kwa kuwa alimtelekeza.Yaani hakuwa anamhudumia mwanae kwa lolote.Sasa umefika muda anataka akae naye.

Nashauri afike kwa walezi au wazee wa anayemlea mtoto watampa utaratibu.Sidhani kama kuna gharama yoyote japo jiongeze hata na chochote kitu ukienda kwa mtoto ni hayo tu
 
Akilinjema

JF-Expert Member
Aug 9, 2016
6,417
2,000

Nimekosea kuuliza swali vizuri,

Hata hivyo nilikuwa na maana kuwa uzoefu unaonesha kabila la mama wa mtoto ndilo lenye kuonesha ni namna gani kimila mtoto anaweza kukombolewa.

Kwa sasa mtoto ni wa ujombani sasa ili arudi kwa baba yake taratibu ndiyo hutegemea kule ujombani wanautaratibu gani!

Ni kama wakati wa kutaka kutoa mahali au kuoa hutegemeana na kabila la mwanamke.

Kwa hiyo muulize yeye huyo ulozaa nae I Hawa kama siyo mwaminifu atafanya kukukomoa kukutajia gharama kubwaaa.
 
Akilinjema

JF-Expert Member
Aug 9, 2016
6,417
2,000
Pia inategemea Huyo mtoto anaumri gani?

Sababu mfano unapokomboa mtoto wa umri wa chini ya miaka 5 haiwezekani kuwa gharama sawa na anaekomboa mtoto aliyemaliza chuo kikuu kwa kusomeshwa upande wa mama !

Lakini uzoefu kwa mila za makabila mengi gharama huwa siyo kubwa sana!
 
Akilinjema

JF-Expert Member
Aug 9, 2016
6,417
2,000
Nazani pia inategemeana na mambo kadha wa kadha matharani:

Huyo mwanamke ana watoto wangapi?

Ulimkuta tayari ameshazaa na mtoto mwingine?
Au wewe ndiyo wa kwanza kumzalisha?

Kama wewe utakuwa wa kwanza kumzalisha huenda ukajumlishiwa na thamani ya mahali hata kama humuoi mama mtoto maana wanachukulia umemharibu wewe ubinti wake!

Kwa wazee wenye akili wanaweza kufanya hivyo.
 
Brightg

JF-Expert Member
Sep 24, 2013
366
1,000
ok ahsante sana kwa maelezo yako nimekuelewa sana, wala hukukosea kuuliza, ila sasa niulize kitu kwa maana hiyo kumkomboa inakuwa sawa na kutoa mahari si ndio maana yake.
Nimekosea kuuliza swali vizuri,

Hata hivyo nilikuwa na maana kuwa uzoefu unaonesha kabila la mama wa mtoto ndilo lenye kuonesha ni namna gani kimila mtoto anaweza kukombolewa.

Kwa sasa mtoto ni wa ujombani sasa ili arudi kwa baba yake taratibu ndiyo hutegemea kule ujombani wanautaratibu gani!

Ni kama wakati wa kutaka kutoa mahali au kuoa hutegemeana na kabila la mwanamke.

Kwa hiyo muulize yeye huyo ulozaa nae I Hawa kama siyo mwaminifu atafanya kukukomoa kukutajia gharama kubwaaa.
 
Brightg

JF-Expert Member
Sep 24, 2013
366
1,000
Pia inategemea Huyo mtoto anaumri gani?

Sababu mfano unapokomboa mtoto wa umri wa chini ya miaka 5 haiwezekani kuwa gharama sawa na anaekomboa mtoto aliyemaliza chuo kikuu kwa kusomeshwa upande wa mama !

Lakini uzoefu kwa mila za makabila mengi gharama huwa siyo kubwa sana!
Mtoto ana umti wa miaka 28 wa kike ameshakuwa mkubwa
 
Brightg

JF-Expert Member
Sep 24, 2013
366
1,000
Mkuu nafikiri kama mimemwelewa vizuri anataka kumkomboa mtoto kwa kuwa alimtelekeza.Yaani hakuwa anamhudumia mwanae kwa lolote.Sasa umefika muda anataka akae naye.

Nashauri afike kwa walezi au wazee wa anayemlea mtoto watampa utaratibu.Sidhani kama kuna gharama yoyote japo jiongeze hata na chochote kitu ukienda kwa mtoto ni hayo tu
Ahsante nimekuelewa vizuri sana
 
Akilinjema

JF-Expert Member
Aug 9, 2016
6,417
2,000
ok ahsante sana kwa maelezo yako nimekuelewa sana, wala hukukosea kuuliza, ila sasa niulize kitu kwa maana hiyo kumkomboa inakuwa sawa na kutoa mahari si ndio maana yake.

Hapana,
Inategemea na jinsi watakavyoamua hao wazee na inategemea uwezo wao wa kujenga hoja .
Mfano kama wewe ndiye uliyekuwa wakwanza kuzaa na huyo mwanamke na katika umri Mdogo kiasi cha kuona kama ulimharibu wengine kushindwa kuja kumuoa kama wanajielewa wanaweza kuthaminisha na gharama ya mahali ya mama wa mtoto wakichukulia kuwa kama ungemuoa ungelipa mahari ya shilingi ngapi?!

Lakini uzoefu ulivyo gharama za kumkomboa mtoto huwa si kubwa sana kutegemeana na kabila na kabila la kule ujombani.
 
Akilinjema

JF-Expert Member
Aug 9, 2016
6,417
2,000
Kwa hiyo unaweza kukuta gharama ya kumkomboa mtoto inaanzia kwa gharama ya mahari ya mama wa mtoto kama ungemuoa na malezi labda ya mtoto n.k

Na hapo ndipo utapata haki ya mtoto kuwa kwenu hata atakapooa au kuolewa huyo mwanao
 
Blasto Ngeleja

JF-Expert Member
Oct 27, 2014
277
250
WASUKUMA
Ni rahisi sana. Unawasiliana na wazazi wa mwanamke uliyezaa nae, unawaeleza nia yako ya kumchukua mtoto wako. Wazazi hao watakupa utaratibu ambapo ni kutoa kiasi cha pesa kama malipo kwakua hukumtolea fahari mwanamke uliyezaa nae. Mara nyingi huwa ni pesa kidogo sana kati ya 20k hadi 200k. Basi utaandaa watu wa kwenda nao wawili au watatu, mtaenda kutoa na kuchukua mtoto.

Jambo muhimu ni mawasiliano Mazuri na familia ya huyo mwanamke hasa mwanamke mwenyewe. Pia huyo mtoto awe na umri angalau miaka 3 na zaidi na wewe uwe na maelezo shawishi ya jinsi utakavyomlea.

USHAURI WANGU
Ili tusiwawekee watoto wetu mazingira magumu ya kuishi ni vyema kuepuka kuzaa watoto na mwanamke/mwanamme unayedhani hatokuwa mme/mke wako. Shuhuda nyingi huonesha watoto hao hupitia vipindi vigumu zaidi katika makuzi yao.

Asante
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom