Utaratibu wa kuandika barua ya posa

Kwa familia ya JamiiForums,

Mimi Mwambadog, mtoto wa mzee Dog, ukoo wa Tanzania. Nimemuomba mzee Mwanza, kama mshenga wangu kufikisha ombi langu hili kwako

Nimevutiwa na kupendezwa na mtoto wako, Kidawa binti chapati, ninaomba unipatie awe mke wangu wa ndoa kulingana na imani yetu.

Nimeliridhika na tabia zake, kutokana na malezi bora uliyomlea kwa uzuri zaidi. Ninaomba mzee wangu, unikabidhi awe mke wangu wa ndoa.

Nasubiri kusikia kutoka kwako/kwenu ili kanuni na taratibu za kidini/kimila ziweze kutimizwa kama utanikubalia mzee wangu.

Natanguliza shukurani zangu kwako kwa dhati kabisa.

Ni mimi,

Mwambadog
Aiseeh! Asante mkuu
 
Habar wana JF
Kuna jamaa yang anatak nimpelekee posa mahali furah ubaya sijui wala cjawahi soma barua ya posa inaandikwa vip nimejalibu kumweleza kuwa cjui chochote lakn jamaa hatak kunielewa ananambia nijitaid nikapiga esabu nikasema hapo siwez kukosa mtu ambaye anajua kuandika au kuona jinsi inavyoandikwa plz nimekwamaaa
 
Toa details kama: Dini yake,kabila lake na kabila la huyo anayetaka kumposa pamoja na dini yake.Then tuendelee
 
Habar wana JF
Kuna jamaa yang anatak nimpelekee posa mahali furah ubaya sijui wala cjawahi soma barua ya posa inaandikwa vip nimejalibu kumweleza kuwa cjui chochote lakn jamaa hatak kunielewa ananambia nijitaid nikapiga esabu nikasema hapo siwez kukosa mtu ambaye anajua kuandika au kuona jinsi inavyoandikwa plz nimekwamaaa

Akipeleka tu Pesa / Hela tayari ni Posa tosha wala hakuna haja ya kuanza kupindishana migongo kuandika mibarua. Fwedha ndiyo kila kitu katika hii Digital World Mkuu asikudanganye Kiumbe yoyote yule.
 
Barua:
Salaam Mr & mrs fulani.
Familia ya yetu (mr&mrs fulani) tunapenda kifikisha kwenu hitaji la kijana wetu Fulani Bin Fulani, la kumuoa binti yenu Miss Fulani, hii ni baada ya kuwa wameishafahamiana na kutambulishana katika familia na wameridhiana kuishi pamoja kama mume na mke. Tumeambatanisha na kitu kidogo kama shukrani ya ninyi kuridhia hitaji la wanetu hawa.

Mr & mrs Fulani.

Imeisha hiyo hakuna mbwembwe, weka na kasenti kidogo humu ndani ikiwa tu wazazi wa binti ni waki- ordinary, ila kama ni wazazi wa kidigitali achana na habari za kuweka pesa humo.
 
Haya mambo yanachangamoto kuyafahamu..usione watu wameoana wengi wamefanyiwa haya mambo, hawayafahamu..

Suala la michakato ya uchumba inategemeana na dini pamoja na kabila...kuna makabila yanapeleka jembe tu na inakuwa ishafahamika nini kinaendelea.
 
Barua:
Salaam Mr & mrs fulani.
Familia ya yetu (mr&mrs fulani) tunapenda kifikisha kwenu hitaji la kijana wetu Fulani Bin Fulani, la kumuoa binti yenu Miss Fulani, hii ni baada ya kuwa wameishafahamiana na kutambulishana katika familia na wameridhiana kuishi pamoja kama mume na mke. Tumeambatanisha na kitu kidogo kama shukrani ya ninyi kuridhia hitaji la wanetu hawa.

Mr & mrs Fulani.

Imeisha hiyo hakuna mbwembwe, weka na kasenti kidogo humu ndani ikiwa tu wazazi wa binti ni waki- ordinary, ila kama ni wazazi wa kidigitali achana na habari za kuweka pesa humo.
namuona mleta uzi akikopi kila ulichoandika hapa.
 
Akipeleka tu Pesa / Hela tayari ni Posa tosha wala hakuna haja ya kuanza kupindishana migongo kuandika mibarua. Fwedha ndiyo kila kitu katika hii Digital World Mkuu asikudanganye Kiumbe yoyote yule.
Kuna nyumba hawaangalii pesa ndg utatolewa mbio
 
Back
Top Bottom