Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,506
- 113,624
Mkuu kwa kutumia IQ yako kubwa hebu tusaidie muungano mbao hauna mkataba wenye sifa za mkataba wa kisheria unavunjwa vipi? Maelezo mafupi tafadhali.
Mnauvunja kama mlivyoauanza. Mnaitana mnaambiana. Mnatayarisha madokezo,mnayapitisha bungeni na BLW, yanaridhiwa, mnawatangazia umma, kisha mnaitana, mnagawana ule udongo tuliochanganya, mnashikana mikono, mnaagana, kila mtu anashika njia yake na khamsini zake!.
Kinachofuatia ni kwa Tanganyika kulirudisha jina lake na kumuandikia Katibu Mkuu wa UN ili kukifuta kiti cha URT na kukirejesha kiti cha T vivyo hivyo kwa Zanzibar.
Baada ya hapo ni ama kuwapa uraia wa moja kwa moja Wazanzibari walioko bara ambao watapenda kuwa Watanganyika au kuwatimua wao na mali zao zinazohamishika kisha waombe rasmi wakubaliwe ndipo waje. Zanzibar nao wataamua hatima ya wabara walioko huko.
Mali zote za muungano zisizo hamishika zinakuwa ni mali ya nchi husika mahali zilipo!. Zanzibar itafaudu!, mjengo kama ule wa BOT Zanzibar ndio utakuwa mali yao!.
Sisi wengine wenye kupenda weupe na ule ubwete wa Zanzibar tutaathirika!, maana kwenda huko sasa itakuwa kuingia kwa viza na mpaka uwe na passport!. Du! Itakuwa shida!.
Happy New Year
Pasco