Utaratibu Upi Unafuatwa Kuuvunja Muungano?

peche luke

JF-Expert Member
Sep 8, 2013
365
0
Inapotokea muungano umefika pahala lazima uvunjike, ni taratibu gani za kisheria huwa zinatakiwa zifuatwe.
 
Nicholas

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
25,280
2,000
ipigwe vita tu atakayeshinda achukue kipande chote na kukifanya chake bila muunganiko wa karatasi. Zenji igawanywe vitalu mtanzania mwenye uwezo wa kuendeleza apewe,asiye na uwezo apewe pori bara na nyumba 10yrs biashara za akina Barubaru zinaisha.

Hawa jamaa wavivu sana ndio maana wana muda wa kuchagua hadi chakula wasichoweza nunua........wanasiasa wao wamewaprogramm vibaya hadi kuwaharibu kwa uongo na kuwapa rushwa ya chakula.
 
ilboru1995

JF-Expert Member
Oct 4, 2007
2,329
0
Muungano huu uvunjike si tu kwa Zanzibar bali hata na watu wa Kilimanjaro, Arusha na Tanga watengwe kwa kupewa madaraka kamili ya nchi yao ili wasiendelee kuwakera watawala wetu waliotukuka na ambao kila kukicha wanawabagua watu wa kaskazini! Nchemba, Nape na CCM yote fanyeni kweli kaskazini ijitenge...
 
Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
37,968
2,000
Inapotokea muungano umefika pahala lazima uvunjike, ni taratibu gani za kisheria huwa zinatakiwa zifuatwe.
Mkuu Peche Luke, umeuliza swali la msingi sana.
Kikawaida, miungano yote huwa lazima iwe na mkataba!. Muungano wetu hauna mkataba bali yale ni makubaliano tuu yalijengwa kwa dhima ya "tuungane!". Kile kinachoitwa hati za muungano, wengine wakiita mkataba wa muungano kiukweli kabisa, ule sio mkataba bali ni makubaliano tuu ila tuu yamewekwa kwenye maandishi!.

Ikitokea ukampenda msichana, ukaomba kuja kuishi kwako na mkawa mnaishi wote kinyumba, hiyo inaitwa "dhana" ya ndoa!. hayo ni makubaliano tuu kuwa mtaishi pamoja, hata mkiyaweka kwenye maandishi, bado ni makubaliano tuu, na siku mkichokana, mkiamua kuachanana, mnaachana tuu kama mlivyoanzana kwa kuitana, vivyo hivyo mtakavyo achana, kwa kuitana na kuagana!.

Ila pia sheria imeweka ukomo wa hii dhana ya ndoa, kuwa mama immeishi kwa muda fulani, ndani ya dhana ya ndoa, then ni mmoja tuu kati ya wana dhana ya ndoa hii ndio amemchoka mwenzie, na kufuatia kukaa ndani ya dhana ya ndoa hii kumekosesha mwanadhana mmoja fursa za kupata ndoa kamili au ndoa nyingine, then mnapoamua kuachana, kama hataridhika, anaweza kufungua shauri mahakamani kudai haki zake alizompatia mwana dhana mwenzake ili afidiwe ule muda alioupoteza kwenye dhana ya ndoa na mahakama itaihesabu hiyo ilikuwa kama ndoa kamili na mlalamikaji kupatiwa mgao wa mali.

Kwa upande wa muungano wetu kama nilivyosema, ni makubaliano na sio mkataba, kilichofanya yawe ni makubaliano tuu na sio mkataba, ni kufuatia makubaliano hayo kukosa sifa muhimu ya mkataba, ambayo ni kipengele cha kuvunja mkataba!. Ili mkataba uwe ni mkataba halali kisheria, unazi baadhi ya sifa kuu za mkataba moja wapo ni ridhaa, waingia mkataba wawe na umri halali kisheria, wote wawe na akili timamu, utekelezaji wa mkataba na kipengele cha kuvunja mkataba. Makubaliano yale ya muungano yalikidhi baadhi tuu ya vipengele hivyo kile cha kuvunja mkataba hakikuwepo, hivyo kubakia ni makubaliano tuu!.

Kufuatia kipengele hicho kutokuwepo, na waasisi wa makubaliano hayo hawapo, then wale wenye dhamana, ya utekelezaji makubaliano hayo, wakifika mahali wakachokana, au mmoja akachoka, anapaswa kumfuata mwingine kwa dhima ile ile kiwa tukubaliane kuachana!. Mkikubaliana, mnashikana mikono, mnaagana kila mtu anashika njia yake!.

Japo baadae zilitungwa sheria kadhaa wa kadha na wakati wa Nyerere, hata kufikiria tuu kuuvunja muungano ilikuwa ni uhaini, kwa vile muungano haipo kisheria, hivyo sheria zote zilizotungwa kuhusu huu muungano wetu, hazina uhalali wa kisheria!.

Mada hii niliwahi kuizungumza sana humu, Swali: Hivi Muungano Tanzania Upo Kweli?! au ni Dhana Tuu ...
na pia hapa Ikithibitika ZNZ Haikushirikishwa, P'seJK Simamisha Mchakato!- "Its ...
Pasco.
 
jogi

JF-Expert Member
Sep 25, 2010
25,614

Pasco unaniangusha kwenye kiswahili. umelitumiaje neno "dhima" mahala pa "dhana"

halafu unaandika maelezo mengi huku ukiujua ukweli kuwa IQ ya ndugu zako watanzania majority ni ndogo ku-condense hayo maelezo ili waipate point yako!!!!!

Ungewaambia pia kuwa sifa nyingine muhimu kabisa ya mkataba ni kuwa na kipengele kinachoruhusu kuu-review mkatba wenyewe (kuuhuisha).
 
nditolo

JF-Expert Member
Jul 2, 2011
2,382
2,000
Siutaki muungano na wala hauna faida kwa Watanganyika. Faida ya kuungana lazima u create soko lakini huu muungano wetu na akina yahe hauna lolote zaidi ya kungeza ajira na vyeo upande wa zanzibar.
 
peche luke

JF-Expert Member
Sep 8, 2013
365
0
Siutaki muungano na wala hauna faida kwa Watanganyika. Faida ya kuungana lazima u create soko lakini huu muungano wetu na akina yahe hauna lolote zaidi ya kungeza ajira na vyeo upande wa zanzibar.

Mbona tunambiwa mchele wa mbeya, viazi akukweti, nyanya, vitunguu nk, vina soko kubwa huko Znz.
 
peche luke

JF-Expert Member
Sep 8, 2013
365
0
Pasco unaniangusha kwenye kiswahili. umelitumiaje neno "dhima" mahala pa "dhana"

halafu unaandika maelezo mengi huku ukiujua ukweli kuwa IQ ya ndugu zako watanzania majority ni ndogo ku-condense hayo maelezo ili waipate point yako!!!!!

Ungewaambia pia kuwa sifa nyingine muhimu kabisa ya mkataba ni kuwa na kipengele kinachoruhusu kuu-review mkatba wenyewe (kuuhuisha).

Mkuu kwa kutumia IQ yako kubwa hebu tusaidie muungano mbao hauna mkataba wenye sifa za mkataba wa kisheria unavunjwa vipi? Maelezo mafupi tafadhali.
 
jogi

JF-Expert Member
Sep 25, 2010
25,614
2,000
Mkuu kwa kutumia IQ yako kubwa hebu tusaidie muungano mbao hauna mkataba wenye sifa za mkataba wa kisheria unavunjwa vipi? Maelezo mafupi tafadhali.

Ni mmoja kati ya waliokatibiana kukataa kutekeleza mojawapo kati ya makubaliano yao ama kuyakataa makubaliano yao yoooote. hapo patano linakuwa halipo tena na mkataba unavunjika.
 
jogi

JF-Expert Member
Sep 25, 2010
25,614
2,000
Na kwa kesi ya tanzania ni pale watanganyika watakapoidai tanganyika yao na wazanzibari kukataa kuwa chini ya linchi likubwaaa liitwalo tanganyika. hapo hakutakuwa na muungano tena.
 
peche luke

JF-Expert Member
Sep 8, 2013
365
0
Na kwa kesi ya tanzania ni pale watanganyika watakapoidai tanganyika yao na wazanzibari kukataa kuwa chini ya linchi likubwaaa liitwalo tanganyika. hapo hakutakuwa na muungano tena.

Je hilo likitokea mashirika kana imf yaliyo ikopa Tz yatamdai nani madeni yao?
 
jogi

JF-Expert Member
Sep 25, 2010
25,614
2,000
Je hilo likitokea mashirika kana imf yaliyo ikopa Tz yatamdai nani madeni yao?

Inakula kwao mazima! wakati wanatukopesha walitakiwa kuangalia usalama wa fedha zao kwa uangalifu mkubwa.

hapa ufanano wake ni biashara ya watumwa!!! wazungu wa leo wanagoma kulipa fidia kwa kisingizio kuwa sii wao ndo walitekeleza biashara hiyo haramu bali ni mababu zao, hivyo haitakuwa haki wahukumiwe wao kwa makosa ya babu zao. ingawa kwenye kufaidi matunda ya uchumi uliokuzwa na watumwa hapo inakuwa balaaaaaaaa.
 
Hii poa kweli kwa hiyo mimi naona hii ya weza kuwa sababu ya msingi kuuvunja huu muungano hasa tukiangalia mzigo wa madeni tulio nao kama Tz.

Tuuvunje muungano tupate muda wa kutafakari kuwa tunauhitaji, wakati tumeuvunja madeni nayo yatakufa. Baadaye tukiona tuna uhitaji tunaungana tena kwa jina lingine na tunakopa upya.
 
jogi

JF-Expert Member
Sep 25, 2010
25,614
2,000
Hii poa kweli kwa hiyo mimi naona hii ya weza kuwa sababu ya msingi kuuvunja huu muungano hasa tukiangalia mzigo wa madeni tulio nao kama Tz.

Tuuvunje muungano tupate muda wa kutafakari kuwa tunauhitaji, wakati tumeuvunja madeni nayo yatakufa. Baadaye tukiona tuna uhitaji tunaungana teja kwa jina lingine na tunakopa upya.

Tafadhali sana ndugu yangu usiyaandike kwa kidhungu maneno haya niliyokunukuu, manake utekelezaji wake ni faida kwetu na ni hasara kwao wadhungu.
 
mangatara

JF-Expert Member
Jul 6, 2012
14,547
2,000
Sikujua unazungumzia Tanzania.

Kwanza ieleweke, Muungano wenu ulivunjika siku Zanziba walipoiandika na kuihalalisha Katiba yao. Siku ile walipouzindua wimbo wa Taifa lao, siku ile walipoipandisha Bendera ya Taifa lao.

Tanganyika wakaachiwa jina kuubwa, Tanzania na bendera na wimbo wao. Tanganyika tukaachwa kwenye mataa. Jina kuubwa bila nchi.
Hakuna Muungano bila Zanziba. Siku moja Mh. Pinda akaulizwa swali bungeni; Je Zanziba ni nchi au? Akagwaya mazima.

Hatuna Muungano hivyo ilitakiwa kabla ya kuandika katiba ya Muungano tuwaulize wananchi wa hizi nchi mbili, Mwataka muungane?? Kile kilichowafanya Nyerere na Karume wauwaze muungano, hivi kweli bado kipo?

Wanaoushabikia muungano wa Tz ni wale wanaoufaidi tuu yaani wanaokula matunda ya juu.
 
peche luke

JF-Expert Member
Sep 8, 2013
365
0
Sikujua unazungumzia Tanzania.
Kwanza ieleweke, Muungano wenu ulivunjika siku Zanziba walipoiandika na kuihalalisha Katiba yao. Siku ile walipouzindua wimbo wa Taifa lao, siku ile walipoipandisha Bendera ya Taifa lao.
Tanganyika wakaachiwa jina kuubwa, Tanzania na bendera na wimbo wao. Tanganyika tukaachwa kwenye mataa. Jina kuubwa bila nchi.
Hakuna Muungano bila Zanziba. Siku moja Mh. Pinda akaulizwa swali bungeni; Je Zanziba ni nchi au?? Akagwaya mazima.
Hatuna Muungano hivyo ilitakiwa kabla ya kuandika katiba ya Muungano tuwaulize wananchi wa hizi nchi mbili, Mwataka muungane?? Kile kilichowafanya Nyerere na Karume wauwaze muungano, hivi kweli bado kipo??
Wanaoushabikia muungano wa Tz ni wale wanaoufaidi tuu yaani wanaokula matunda ya juu.

Kwa maoni yako muungano haupo, sasa mbona bado unakubali kuwa na matunda ya muungano?
 
mangatara

JF-Expert Member
Jul 6, 2012
14,547
2,000
Kwa maoni yako muungano haupo, sasa mbona bado unakubali kuwa na matunda ya muungano?

Ulivyonisoma ni kwamba nayakubali matunda ya Muungano kweli? Pole sana. Nimekuambia wanaouona muungano huo ni wale tu wanaokula hayo matunda ya muungano usiokuwepo.

Haswa Wazanzibari wanaobebwa kwa mbeleko hiyo yu muungano fake.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom