Maswali yatokanayo na katiba! Mambo yasiyo ya muungano huwa ya muungano katika kipindi gani? Au ni ubovu wa katiba?

Trable

JF-Expert Member
Jan 3, 2023
1,787
3,272
Wasalaam

Mara nyingi huwa nasikia huko Bungeni na kwa wanasiasa mbalimbali kwamba,

Muungano wetu ni wa kipekee, umezifanya nchi hizi mbili kuwa na mambo ambayo hayawezi kuingiliana na yale ambayo yanayoingiliana

Kuna yale yanakuwa ya Zanzibari pekee na yale yanakuwa ya Watanganyika pekee!

Kulingana na mfumo wetu ulivyo na katiba yetu, unaruhusu tuwe na Maraisi huku Tanganyika anayesimama kama Rais wa Tanzania, vivyo hivyo huko Zanzibar, yeye anasimama kama Rais wa Zanzibar


Kwa sababu hiyo, Huku Tanganyika ndiko haswaa kwenye chungu cha muungano kwa sababu mambo mengi hupikwa huku,

Rais wa Tanzania (Tanganyika) anayomamlaka kikatiba kuteuwa mawaziri wanaotoka Zanzibar na kuwapa wizara huku Tanganyika, sifahamu huko Zanzibar

Lakini pia, Huku Tanganyika, Rais pia aweza kutoka Zanzibar na akawa Rais wa Tanzania (Tanganyika)

Maswali yangu ni haya!

Ni wakati upi ambapo mambo yasiyo ya muungano yanaweza kulazimika kuwa ni ya muungano?

Je, Ni wakati Tanganyika ama Zanziba inapokuwa na Raisi kutoka Zanzibar ama Tanganyika?

Je, ni wakati ambapo waziri kutokea Zanzibar anapopewa wizara isiyohusika na muungano?

Na kama sivyo, Je, inapotokea Viongozi sasa wametokea upande mwingine na kutawala upande mwingine wanafanikisha mambo ambayo hayahusiani na muungano, katiba huwa inasemaje?

Na je? Kunakipindi Rais wa Zanzibar anaweza kutokea huku kwetu uzaramoni ama huko Kigoma akawa Raisi wa Zanzibar?

Au hilo nalo sio jambo ambalo limo kwenye muungano?
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom