Pope
Senior Member
- Dec 3, 2007
- 117
- 0
Kuala Lumpur - Malaysia.
Waziri Mkuu ambaye ndio kiongozi wa shughuli za kiserikali nchini Malaysia ameamuru mawaziri wote waliteuliwa hivi karibuni kuzitaja mali zao na zoezi hilo linatakiwa kukamilika kabla ya kikao cha kwanza cha Bunge Jumanne wiki ijayo 24 March 2008.Katika taarifa iliyotolewa na ofisi ya waziri mkuu Datook Badawi inasema kuwa, Katika form hizo za ku Declare mali mawaziri hao pamoja na mambo mengine wanatakiwa kusema Account walizonazo na yule mwenye Kima kinachozidi Ringit 150,000 (50,000 USD) anatakiwa aseme pia. Pamoja nao wake na waume wa mawaziri hao, watoto na wanafamilia wote wa karibu yao (immediate family members) nao pia wanatakiw mali zao zionyeshwe.
"Zoezi hili si la hiari, hii ni sheria na ni lazima ifuatwe ili kulinda imani ya wananchi kwa serikali yao...", alisema Badawi.
Zoezi hili haliishii kwa MAwaziri tuu bali ni utaratibu ambao viongozi wote wanaotumikia jamaa hutakiwa kufanywa na baada ya Jumanne, Ripoti ya mali za vigogo hao zitapatikana kwenye mtandao wa serikali kwa wananchi kujua na zitakaa hapo hadi baraza litakapovunjwa. Pia wananchi wanaruhusiwa kuhoji na kuperusi viambatanisho vya kila kiongozi katika office ya serikali, iliongeza taarifa hiyo.
Katika sheria hii, kiongozi akibainika kusema uongo au kuficha mali yake basi atafutwa kazi na kushitakiwa na ikiwezekana mali aliyoificha itataifishwa na serikali.
Baraza la mawaziri la Malaysia linaundwa kutokana na Vyama mbali mbali vya upinzani ikiwa ni kutoka chama Tawala na Upinzani (coalition).
Malaysia ni nchi yenye kufuata mfumo wa Vyama vyingi vya kisiasa na katika chaguzi iliyopita (wiki mbili zilizopita) Chama tawala kilipoteza baadhi ya Majimbo likiwamo jimbo la Penang ambako kuna wachina wengi.
Je mnaonaje utaratibu huu ukitumiwa na kwetu?