Utapeli wa nyumba unaoshika kasi Mbagala Chamazi na Chanika

Kuna wimbi la nyumba nzuri na za kisasa kwa mwonekano zinaziuzwa kwa bei chee 25m-45m Mbagala Chamazi na Chanika jijiji DSM.

Mchezo upo hivi:

Kuna jamaa wana viwanja vingi na wana mafundi wao ambao hujenga nyumba cha kiwango cha chini sana cement mfuko mmoja tofali 48+ tofali hufwatuliwa site na kujenga hapo hapo.

Bati gauge 32 wanapiga rangi wenyewe. Baadhi ya kuta wameweka play wood badala ya tofali kitaalam sana.

Kench zipo mbali mbali sana kubana matumizi ya mbao. Ndo maana nyumba zote laizma ziwe na gypsum kuficha mambo.
Nyumba huwa hazijakaliwa na watu means bado mpya.

Hazina lenta ndo maan lazima wapige plasta na kuweka gypsum kuficha. Kuna wataalam wa kuchanganya rangi ili kukubabaisha uingie kingi. Msingi tofali moja tu ishapanda

NB: Nyumba hizi hazichukui muda sana utaona nyufa balaa. Na walengwa wengi ni wastaafu ambao hutafuta nyumba za kuishi baada ya kustaafu.
Mkuu unaweza kutuwekea nyumba mbili tatu za aina hio? Ambao watu walinunua na sasa hivi zimebomoka au kutoa nyufa?! Maanake hizi Stori tumesikia muda mrefu.
 
Jenga uza ni nyumba Bora kabisa na za Bei nafuu kwa maisha ya Mtanzania hayo unayosema ni tetesi na uzushi tu. mfano hizi nyumba nimeziona kuanzia msingi mpka upauaji na zipo mbagala maji matitu mtaa wa kwa ma sista zipo vizuri.

IMG_20200814_135823_197.jpg
View attachment 1682208
 
Hapo kwenye Lenta umetulepeka puta jenga lazima ziwe na lenta na Kuhusu ubora inategemea na Aina yako ya Akili....nipo Chamazi ukitaka kuziona hizo nyumba zikijengwa njoo
Mkuu sisi nyumba ya familia haina linta ile ya kuzunguka ila kalinta kwenye madirisha na milango tu. Sasa hivi baada ya miaka ishirini ina nyufa balaa. Kuna wengine wanaweka frame halafu tofali zinapita juu. So inawezekana
 
Kuna watu wengi wanastaafu hawana nyumba au wana nyumba za kawaida so wanataka za kisasa na wengine wamefanya kazi mikoani sasa wanataka wakisfaaru waje waishi Dar.
Kha yan anatoka mkoan kuja dar uzeeni au anakua n mwenyeji wa dar, mkoan alikua kikaz?
 
Kuna wimbi la nyumba nzuri na za kisasa kwa mwonekano zinaziuzwa kwa bei chee 25m-45m Mbagala Chamazi na Chanika jijiji DSM.

Mchezo upo hivi:

Kuna jamaa wana viwanja vingi na wana mafundi wao ambao hujenga nyumba cha kiwango cha chini sana cement mfuko mmoja tofali 48+ tofali hufwatuliwa site na kujenga hapo hapo.

Bati gauge 32 wanapiga rangi wenyewe. Baadhi ya kuta wameweka play wood badala ya tofali kitaalam sana.

Kench zipo mbali mbali sana kubana matumizi ya mbao. Ndo maana nyumba zote laizma ziwe na gypsum kuficha mambo.
Nyumba huwa hazijakaliwa na watu means bado mpya.

Hazina lenta ndo maan lazima wapige plasta na kuweka gypsum kuficha. Kuna wataalam wa kuchanganya rangi ili kukubabaisha uingie kingi. Msingi tofali moja tu ishapanda

NB: Nyumba hizi hazichukui muda sana utaona nyufa balaa. Na walengwa wengi ni wastaafu ambao hutafuta nyumba za kuishi baada ya kustaafu.
Basi tuwaite wauaji wa wastaafu wetu,bado tunawahitaji wastaafu wa taifa letu, lugha nyingine senior Cetizen wetu
 
Ogopa sana rangi nyeusi! Juzi nimejifanya kuwa mimi ni mtaalam na mjuaji nikapeleka PC yangu mpya mpya hivi kwa fundi ili aniwekee ile kitu kama ujiuji ya kupoozea CPU matokeo yake amenibadilishia RAM pamoja na feni na PC imerudi nusu nati hazijafungwa!
Hii post ni ya mwaka jana lakini bado nakupa pole. Mimi nilipeleka simu yangu kwa fundi kuweka kioo cha mbele ikarudi nusu ya screw za ndani hakuna. Sijawahi kuona nchi ambayo watu hawako makini kama Tanzania. Halafu Kariakoo pale kuna mafundi simu wazuri kweli kweli. Tatizo lao kubwa ni kwamba hawa-concetrate wakati wa kufanya kazi. Unakuta fundi anatengeneza simu huku anafanya mambo mengine kama matatu kwa mpigo. Na uaminifu ni sifuri.
 
Nafikiri sio utapeli maana unapata mali according to your money, kama unataka cement itoe matofali 18 utalipa milioni 100, hao jamaa acha wahudumie hiyo market ya watu wa chini kuna watu wanahitaji na ndio wanapoweza, usitake Mercedes Benz kwa bei ya Toyota
 
Back
Top Bottom