TAHADHARI, Kwa wanaonunua nyumba mpya.

MY LOVE

Senior Member
Oct 17, 2012
161
68
Jambo hili nimeliona sana huku maeneo ya mbagala, kongowe, mbande chamazi na maeneo mengine ya hii wilaya ya Temeke, sijui sehemu nyingine kama lipo au la. Kumekuwa na wafanyabiashara wasio waaaminifu ambao wanaitwa JENGA UZA wengi wao ni madalali, wananunua kiwanja wanajenga halafu wanauza nyumba, sina tatizo kabisa na hii biashara ila

HIZI NYUMBA ZIMEJENGWA CHINI YA KIWANGO MPAKA INATISHA NA KUSIKITISHA MNO, kwa kweli imeniuma sana. Matofali yaliyojengea yamejaa mchanga mtupu, lenta zimefungwa kwa nondo used tena ni vipande vipande, ila msingi upo juu ili kukudanganya mnunuaji, baada ya hapo mbao za kenchi sio treated zinapakwa dudu killer tena ni chachezile mbazo mtu ataweza ona kisha plasta na rangi na mapambo ya kichina nyumba nzuri baada yawiki tatu na mtu anauziwa na anatoa million kadhaa bila kinyongo.

WALENGWA; kuna vunjavunja inaendelea kurasini na mivinjeni, waathirika wanalipwa fidia kisha unapewa miezi miwili tu uhame, wengi wao wakipata fedha huamua kununua nyumba fasta kabla haijayeuka,sio mbaya ila NASHAURI bora ununue nyumba ya zamani uirekebishe mwenyewe kuliko hizi mpya zilizojengwa na walioiona fursa lkn hawana huruma kwa watanzania wenzao, au uwe na mafundi wakushauri ununue.
HAWA WANAOJENGA NI madalali wameshasoma soko lipo ndipo wakaitumia fursa.
 
Mmoja wa wafanyabiashara hiyo huku kwetu Mtoni Kichangani anaitwa Ngangari, huyu bwana amejenga nyumba kadhaa maeneo haya ambazo zote zinafanana kwa kuwa na kreki yaani hazifai kabisa.
 
Kweli adui wa mtanzania ni mtanzania

Wanajenga nyumba bila vieango hata kuwahurumia wanunuzi kwamba Itahatarisha maisha yao???
 
Wanaona poa tu kwa sababu hawapati hukumu yao pale nyuma ikileta madhara makubwa kwa wakazi wake.
 
Back
Top Bottom