JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 625
- 938
Matapeli huko mtandaoni hutengeneza wasifu bandia kwenye tovuti halali za kutafuta wachumba. Wanatumia profaili hizi kujaribu kuingia kwenye uhusiano na mtu ili waweze kupata pesa zake na maelezo binafsi.
Tapeli atakuwa na uhusiano mzuri na mtu huyo wakishazoeana ataanza kuombe pesa ili kusaidia kulipia gharama zinazohusiana na ugonjwa, kuumia, kusafiri au shida ya familia.
Matapeli huwa wanachanganya kihisia kwa kuvuta moyo wa mtu. Wakati mwingine huwa wanatumia mda mrefu sana ili kumjengea mtu uaminifu na wakishajiridhisha kuwa wameshamteka na anawaamini ndipo wanafanya utapeli na kuondoka.
Hivyo ni vyema ukawa makini unapowasiliana na mtu usiyemjua. Usimtumie pesa mpaka uwe umekutana naye ana kwa ana na kumuelewa vizuri.