Utapeli wa Dawa ya 'HIT' katika kuua Mbu

Gentlemen_

JF-Expert Member
Nov 24, 2019
3,563
10,546
Hizi dawa zilikuwa vizuri miaka minne iliyopita ila hali ya sasa kwa kweli ni UTAPELI wa wazi.

1. Haiui MBU kwa kiwango kinachopaswa yaani katika Mbu 50 watakufa watatu (3).

Yaani mpk mbu afe ni umloweshe na hiyo dawa ndio atakufa ila ukipuliza kama inavyoelekezwa upulize ktk mazingira ya eneo waliopo, hakika hatokufa Mbu hata mmoja, ukitaka mbu afe ni umshike umpulizie usoni.

2. Hata Mbu kuzimia kidogo hakuna! Sana sana watajificha tu kwa muda wa lisaa limoja baada ya kupuliza ila watarudi na wakirudi wanarudi na NJAA ya kufa mtu. (Inawezekana hii Dawa ina wapa Appetite zaidi)

Si kwa HIT tu nimetumia dawa ya RUNGU pia haina matokeo mazuri ktk kuangamiza MBU.

Je wana JF mmekutana na hii changamoto?

Je mnapendekeza dawa ipi bora ya kuangamiza hawa viumbe?

NB: Nimezungumzia kwa upande wa Mdudu aina ya MBU tu kwa kuwa ndio mdudu anayenisumbua mahala nilipo, hakuna Mende wala wadudu wengine, hivyo ufanisi wa dawa hii kwa kuua viumbe wengine sijaupima.

Nawasilisha.
 
Ni kweli kabisa,mbu hawafi na hata rungu ni harufu tu inabaki muda mrefu lakini haziui.
Nimeamua kujibana narumia x pel bei sio poa Sana imesimama
Matokeo je? Inaua? Swala la bei si shida.
 
Alafu wanauza kwa bei kuubwa utadhani ina maajabu kumbe upuuzi tu.
miaka flani nyuma, kibanda hakijaisha vyema
niliziba madirisha, nilipiga chumbani, kwa kua inachoke nikatoka nje kwa mda wa dk 20

kurudi, nakuta mende, mijusi, nyoka wadogo, tandu, buibui, wote wamekufa wako pembeni
nilishangaa sana, ilihali lengo ilikua ni kuua mbu, nilishangaa pia kuona naishi na tandu chumbani 😅
 
Back
Top Bottom