A
Anonymous
Guest
Ninatoa ushuhuda wangu binafsi pamoja na wa watu wengine ninaowafaham yaan wanangu sana kuhusu vitendo vinavyofanywa na baadhi ya kampuni za ubashiri, hasa Parimatch Tanzania, ambavyo vinaonyesha wazi dalili za udanganyifu kwa wateja.
Sisi ni waathirika wa moja kwa moja. Tumeshuhudia na kupitia hali ambapo mteja anajisajili na kuweka fedha (deposit), lakini muda mfupi baadaye akaunti yake inafungwa bila sababu ya msingi. Ukifuatilia unaambiwa umevunja taratibu za kampuni bila kupewa ushahidi wowote na hapo ndipo fedha zako ulizodeposit zinapotea kabisa.
Zaidi ya hapo, kuna tatizo kubwa la withdrawal. Fedha zinaoneshwa kuwa zimetoka lakini hazifiki kwa mteja. Mimi binafsi ni mhanga wa hili imepita zaidi ya mwezi mmoja tangu nifanye muamala, lakini sijawahi kupokea fedha zangu hadi leo. Hii si bahati mbaya, bali inaonekana kama mfumo wa makusudi wa kuwanyima wateja haki zao.
Pia, kukosekana kwa mawasiliano ya moja kwa moja kama simu, na kutegemea live chat na barua pepe pekee, kunaongeza mashaka kuwa kuna juhudi za makusudi za kujificha na kukwepa uwajibikaji.
Kutokana na ushuhuda huu, ninaeleza wazi kuwa vitendo hivi vinafanana na utapeli unaofanywa kwa mfumo uliopangwa. Hii si changamoto ya mtu mmoja, bali ni tatizo linaloathiri watu wengi.
Hivyo basi, ninatoa wito kwa mamlaka husika kuchukua hatua za haraka na za kisheria dhidi ya kampuni kama hizi, kuchunguza kwa kina mwenendo wao, na kuhakikisha kuwa wateja wote waliodhulumiwa wanarejeshewa fedha zao.
Aidha, ni muhimu kabla ya kuwapa leseni watu kama hawa wawaoneshe ofisi rasmi ambazo mteja anaweza kufika physically ili kutatuliwa shida zake. Pia ni muhimu kuwe na uwajibikaji wa kweli ili kuzuia wananchi kuendelea kuathirika.
Wafikishieni wahusika ili tusaidike