Utapeli tiGOPesa!

Tigo wezi ata makato yao sio sh1 kwa sekunde kama wanavyodai na kwenye akounti za tigo pesa wao wanaiba fedha za watu bila ya kutoa maelezo yeyote

tunaomba tume ya mawasiliano ianze kudhibiti wizi na pia kuangalia kama kampuni hizi zinalipa kodi ipasavyo.. nadhani ipitishwe sheria ya kuweka mkurugenzi mmoja nanayewakilisha serikali katika haya makampuni makubwa kuzuia wizi wao
 
Hili tatizo ni kweli lipo, mimi toka asubuh nimenunua muda wa maongezi kwa tigo pesa lakini mpaka sasa bado salio halijaongezeka na ktk tigo pesa wameshakata. Leo hii ni kama mara ya tatu hivi katika wiki mbili kitu kama hiki kinanitoke.
kwa hiyo unataka kusema kuwa kunapokuwa na tatizo katika mfumo wa kompyuta ni lazima liwe limesababishwa na hacking??!!
 
NAPENDA KUWAJULISHA WALE WOTE MLIOJIUNGA NA TIGO PESA, M PESA ZAP NA NYENGINEZO KAMA HIZI,KAMA HAMJUI KUTUMIA HUDUMA HIZI NI BORA MKAJIFUNZA KWANZA. M2 ANAENDA KWA WAKALA JINSI YA KUTOA PESA HAJUI. ANAMPA WAKALA AMFANYIE MUAMALA. UKIMPA MGONGO ATAKUUMIZA SIKUYEYOTE AKIPENDA. SI WAKALA TU HATA M2 WAKO WA KARIBU ATAKAPOJUA NAMBA YAKO YA SIRI NI RAHISI KUKUIBIA. NINI KINAFANYIKA? BAADA YA WAKALA AU MTU ATAKAEJUA AKAUNTI YAKO IMESHIBA. ANAIUA LAINI YAKO (SWAP.THEN ANAKUWA NAYO YEYE ANAENDA KWA WAKALA ANAJICHUKULIA ATAKAVYO. KWA KWELI MITANDAO HAIUSIKI KWA HILO ITAONYESHA WEWE NDIO ULIE TOA PESA. KWA MAELEZO ZAID wanatamani@gmail.com
 
tiGO pesa wameanza mchezo mchafu wa kuwaibia wateja wao (wakala). Ukiweka pesa bank ili wakuwekee kwenye line, baada ya muda line inafungwa. Na ukifuatilia line unakuta pesa zote zimetolewa na mtu usiyemjua. Cha kusikitisha ukienda ofisi za tiGO kuuliza majibu yao ni kama choo kichafu. Hawaonyeshi ushirikiano kabisa. Wahusika tiGO pesa: 1. Sisi tunaofanya biashara nanyi hatuokoti pesa. 2. Niambieni nifanye nini ku-recover pesa zangu. 3. Ajirini watu waaminifu na wenye kutoa ushirikiano, siyo majibu ya ovyo.
 
Back
Top Bottom