kulumba
Member
- Apr 10, 2020
- 36
- 130
Huu ni uzembe wa hali ya juu sana huwezi kumpa mteja ajaze namba mwenyeweHii kuna jamaa angu amepigwa laki 6 wiki iliyopita.
Kuna jamaa alikuja akaomba awekewe elfu 5, akaweka ila kabla hajaondoka akaja mtu mwingine akaomba atume/kuweka elfu 50, sasa huyu wa kwanza akawa anampigisha story yule mtoa huduma tena kuhusu mambo ya Corona na story zilikuwa tamu sana, basi mtoa huduma akampa simu yule mteja wa pili ili aweke namba za simu. Alichokifanya jamaa ni kwenda 'inbox' akajitumia sms na kisha akasave namba yake kama TIGOPESA kwenye simu ya mtoa huduma. Jamaa akarudisha simu na kumuambia muamala umekatika.
Mtoa huduma akafanya tena muamala na kufanikisha kutuma hela kwa mteja. Yule jamaa wa kwanza akachukua simu kwa jamaa wa pili na kumuambia mtoa huduma anatoa laki 6, kumbe aliedit ile sms ya salio la mwisho akaongeza laki 6 na kwa kuwa kule hii namba ikiseviwa kwa jina la TIGOPESA basi jamaa akatuma sms ya kawaida lakini kule kwa mtoa huduma likatokea jina la TIGOPESA kuwa amepokea laki 6 na salio jipya ni kadhaa, mtoa huduma si akaingia king akampa laki 6.
Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app