Utapeli mpya mjini | Mawakala wa huduma za kifedha kuweni makini sana

Mbona unaonesha wewe wakala hauna uhakika! Unapoamua kithibisha toka Airtel ni kwamba hauna uhakika na kazi yako, ulichokifanya usithubutu kumuuliza mtu mwingine kama ulikifanya unajifunga, kataa.
Sina uhakika kweli sababu nimefanya miamala mingi sikumbuki wa 5000 ni huyo au wa 50k ni huyo,unahudumia wateja zaidi ya 100 kwa siku utakumbuka wote? Na kiasi walichoweka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii kuna jamaa angu amepigwa laki 6 wiki iliyopita.

Kuna jamaa alikuja akaomba awekewe elfu 5, akaweka ila kabla hajaondoka akaja mtu mwingine akaomba atume/kuweka elfu 50, sasa huyu wa kwanza akawa anampigisha story yule mtoa huduma tena kuhusu mambo ya Corona na story zilikuwa tamu sana, basi mtoa huduma akampa simu yule mteja wa pili ili aweke namba za simu. Alichokifanya jamaa ni kwenda 'inbox' akajitumia sms na kisha akasave namba yake kama TIGOPESA kwenye simu ya mtoa huduma. Jamaa akarudisha simu na kumuambia muamala umekatika.

Mtoa huduma akafanya tena muamala na kufanikisha kutuma hela kwa mteja. Yule jamaa wa kwanza akachukua simu kwa jamaa wa pili na kumuambia mtoa huduma anatoa laki 6, kumbe aliedit ile sms ya salio la mwisho akaongeza laki 6 na kwa kuwa kule hii namba ikiseviwa kwa jina la TIGOPESA basi jamaa akatuma sms ya kawaida lakini kule kwa mtoa huduma likatokea jina la TIGOPESA kuwa amepokea laki 6 na salio jipya ni kadhaa, mtoa huduma si akaingia king akampa laki 6.

Sent using Jamii Forums mobile app
...mmmmm, hata sikuelewa! Inawezekana kweli?...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom