Sisi tumelizwa 1,300,000/= kwa njia hiyo hiyo uliyoelezea Mjasiliamali. Tena siyo waswahili kama unavyodhani kwani rugha wanayoongea ni kiingereza ambao ni watu weupe tena waliyoenda shule.
kweli maisha ni magumu mkuu, lakini katika pilikapilka za kutoka ndio hivyo tena, watu hawaishihii kuwatapeli watu tu bali mambo ya kuuwa maalbino, ushirika, ulokole usio na kichwa wala miguu na mengineyo mengi ili mradi kama wewe ni mtafutaji lazima uibiwe, ukipona kwa hao matapeli bac utakamatwa kwa mganga au kwa Mtumemaisha magumu mkuu ndio maana watu wanabuni mbinu za kujiongezea kipato, na kama utagundua hawawaibii walala hoi, so sio mbaya wanagawana uamskini, ilaa tuwe makini na hizo njia mpya za utapeli
deal yoyote inayolipa zaidi ya mara mbii ya fedha uliyoinvest ni WIZI, UTAPELI ama HARAMU..................
Ama kweli bure ghali!
Hivi hivi watu wali[peleka pesa yao DECI eti izae na wakapoteza viakiba vyao. Sijui tutajifunza lini kwamba unavuna ulichopanda?
Hao watu washawaliza wengi na hata majuzi tulitaka kuwakamata mitaa ya Sinza wakakimbia!
Mimi nimerecord hadi sauti yao! But if it is a police case ni rahisi kuwakamata through serial number za simu-handset. (baada ya registration ya simcard itakuwa rahisi through mobile number). Chukua simu yako, piga *#06# utaona serial number ya handset yako, hii ndo police wanatumia kuwapata wahalifu wasio wajanja, mhalifu mjanja atatumia call box ama simu yake then anaitupa, ama atatuma msg (ukituma msg kwenye mtambo wa simu serial number hai-display, ndo maana ilikuwa vigumu ku-trace wabaya wa Mwandishi Kubenea!).
Waalifu wengi wanajisahau wanapiga simu then wanabadilisha simcard wakifikiri huwezi kuwapata! Atabadili line ya Tigo, Zain, Voda ama Zantel, lakini simu ni ile ile. Kama unakumbuka wezi wa CRDB Azikiwe, na NBC moshi walikamatwa kwa staili hii, baada ya waalifu kutupa simcard na polisi kuikota.
Kawaida polisi wanatumia serial number na kuangalia watu unaowapigia mara kwa mara, say mkeo/mmeo ama mtu yeyote wa karibu, then from there upelelezi unaanza!
Wanawatapeli wengi hawa watu hasa wakitegemea kwamba December ni mwisho wao baada ya simcard registration!
POLICE WAKIWA SERIOUS WANAWAKAMATA!
Story hii ni kweli kabisa. Katika ofisi niliyomo tuna biashara mbali mbali ikiwemo ya fumigation. Mnamo February 09 meneja wa kitengo cha fumigation alipigiwa simu akaambiwa kwamba kuna dawa zinatakiwa kwenda Sudan ya Kusini kwa ajili ya kuifadhi chakula cha UNHCR. Kwamba mtu anayezichukua dawa hizo atatokea UNHCR Ngara mara tu itakapodhibitika kwamba dawa zipo atapanda charter toka Ngara hadi Dar Es Salaam nawakutane airport.
Mimi binafis nilihusika kuzungumza kiingereza na mzungu (mwenzangu hajui kimombo vizuiri) aliyejifanya yuko Ngara na aliniambia tukipeleka madawa hayo airport atatulipa cash hapo hapo na faida ilkuwa kubwa. Dawa zenyewe tuliambiwa zinapatika kwa supplier pale Mwenge na kila chupa $6,000 na zinatakiwa chupa 2. Kwa nini wasinunue direct toka Mwenge? Tukaambiwa supplier wa Mwenge hatoi commision.
Kwa bahati nzuri meneja wa kitengo cha fumation anafahamiana na watu wa UNHCR hapa Dar ES salaam, kwa hiyo kitu cha kwanza aliwapigia simu kuhakikisha kwamba dawa kama zile ni za kuhifadhi chakula wakamwambia sio. Tena wakamwambia pia kituo cha UNCHR kule Ngara kilishafungwa hivyo tukajua huyo "Mzungu" hayuko Ngara kama alivyodai.
Hata hivyo tukaamua kufuatilia tuone mwisho wake.Tukachukua blank cheque kuelekea Mwenge. Tulipofika Petrol Station ya Bamaga tukaambiwa tusimame pale mtu atakuja na dawa tumpe $12,000 atukabithi dawa. Alipokuja tukaingia kwenye gari yake akatuonyesha "dawa". Tukamwambia tunalipa kwa cheque akarusha. To cut the long story short baada ya hapo simu zilizopigwa na yule "mzungu" akilalamika kwamba yuko tayari airport na nasubiri dawa zilikuwa nyingi mno. Ni kweli ni mtandao wa hali ya juu wa kitapeli na wazungu wamo!! BEWARE.
kwanza kabisa if you are smart and informed, mi naona ni ngumu kutapeliwa na hawa mabwana! Eti dawa inahitajiwa na unhcr kwa ajili ya kuhifadhi chakula! Shirika linalohusika na chakula duniani si unhcr, ni un-wfp, hata kambini wanaotunza chakula ni wao wala si unhcr. Unhcr wanahusika kugawa non-food commodities, mahema/turubai, mashuka, nguo n.k
kitu kingine, si kwamba wana-wazungu et wanaongea kiingereza fasaha!, jamani mmemsahau steeve nyerere anayeigiza sauti ya bush, obama, marehemu sadam hussein na sarkozy! So suala la kuiga lugha na kujifanya mzungu, mkenya ama mganda, sio issue ni kuiga tu!
Kuna suala la line ya simu eti inadisplay code za uganda ama kenya. Hata wewe ukienda na voda ama zain ya tanzania ukiwa kenya ama uganda itaonesha uko tanzania. So hawa watu wanatumia line za nchi hizo tu na si kwamba wako huko, wako sinza tu hapa dar.
Beware again and again!!!!!!!!!!!!!!!!!!!