Utapeli Kwa Njia ya SMS – Tuwe Makini

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
218
Utapeli Kwa Njia ya SMS – Tuwe Makini



Ndugu zangu kuna watu wameanza kulalamika kwamba wanapata ujumbe kwenye simu zao za mikono kutakiwa kuchangia vyama kadhaa vya kisiasa nchini , nilipopata habari hii sikuamini kabisa kwamba sasa vyama hivyo vimeamua kuanza kutuma ujumbe wa kuomba michango kwa watanzania mbalimbali kutumia simu zao za mikono
Ukicha hili huko nyuma haswa wale wateja wa mtandao wa tigo walikuwa wanapokea ujumbe unaofanana na huu ingawa wao walitakiwa kuchagua habari wanazozitaka kama ni za simba au yanga na kupokea habari toka klabu hizo au kuchangia klabu hizo kupitia simu zao za mikono ingawa mwishoni baadhi ya wanachama wa simba walilalamika kuhusu upotevu wa fedha hizo sijui kwa yanga .


Ndugu zangu hali inaonekana kuwa mbaya sasa wajasiriamali wanaamua sasa kutumia mwanya wa kutokuwa na sheria kali za mawasiliano kuamua kuanzisha vitu na mengine mengi ambayo hayata tija kwa taifa kuchukulia wenzao fedha na kutokomea kwa kushirikiana na baadhi ya vigogo kwenye sehemu kadhaa bila vigogo hao kujua kwamba nini kinachoendelea .


Ndugu zangu tuwe makini sana na mialiko hii ya kuchangia vyama , makundi na aina nyingine zozote za michango tunazotakiwa kutoa bila ridhaa zetu huku ni kutunyanyasa na ninaomba utaratibu wa kushitaki kampuni ya simu ambayo inaruhusu mtandao wake kutumika kutuma matangazo na kuanzisha michango kama hii ambayo haina maslahi na imelenga katika kutapeli na udanganyifu wa hali ya juu
 
Back
Top Bottom