Utani wa watu ninaoupenda hapa JF pamoja na watu na mada utakazowakuta

The Lastdream

JF-Expert Member
Jan 23, 2024
1,605
3,525
wakuu Mambo ni vipi.

Mimi huwa napenda sana kusoma mada mbali mbali hapa Jf
Kama kichwa cha habari kinavyosema hapo juu, Leo nitazungumizia utani wa watu hapa Jf na watu na mada ambazo utawakuta.

1 . Ni Accumen Mo na mgalatia Maghayo
Hawa ndugu zangu mimi huwa wananifurahisha sana. Nitakapoona komenti ya maghayo basi najua Accumen Mo lazima aweke wino wake hapo na lazima iwe ni kituko. Mwanzoni mgalatia huyu alikuwa ana battle sana na adriz nikaona utani umepungua umeamia kwa accumen mo. Sijui nyinyi mnauchukuliaje utani wenu ila kwangu ni burudani

2. Lucas Mwashambwa
CHIEF PRIEST
Tindo
Ma mmoja anaitwa Benjamin netanyhau

Sijui wao huenda wakawa wanaongea kwa kuchagua pande zao za siasa ila mimi kwangu huwa ni burudani. Hasa Kaka Lucas akiwa anamjibu Benjamin netanyhau huwa anamwambia hivi “ Punguza mibange unayovutia chooni “🤣🤣 binafsi kwangu ni burudani . Tindo na Lucas na ndugu chief priest hazijawahi kuiva ni paka na panya. Hili battle huwa ninalipenda.
Lakini kaka Lucas katokea kumuelewa Sana dada @ephen hata ukiangalia charts zao unaona kuna flow nzuri kabisa baina yao.

Kuna mtu mmoja sijui yeye kama yupo serious ila kwangu huwaga ni kucheka Etwege huyu jamaa yeye hata kama mada inahusu mboga za majani lazima neno Tundu Lissu liingie hapo na lazima atafute koneksheni ya mboga na Tundu lissu. Kwangu mm huwa ni kucheka tu na furaha tele. Nakukubali sana ndugu.

Ukitaka Infropreneur uone komenti yake wewe anzisha mada ya kusema Mungu yupo, kama si komenti ya kwanza mpaka ya tano tangu mada ianzishwe labda hayupo online😂😂 huwa nafurahi sana.

Ukitaka kuona uzi wa mpira unanoga wawepo Hawa watu sana sana kuhus SIMBA VS YANGA

Okwa BOBAN SUNZU mhasibu
Labani og
NALIA NGWENA
Scars
Hapo kuna wananchi na kuna simba watoto wa kariakoo, Mimi huwa majadiliano yao yananifurahisha sana. Ninawakubali sana.

Ngoja niishie hapa next time nitakuja na kitu kinachonifanya Niipende zaidi Jf .

Weka watu unaopenda aidha utani wao au chemistry waliyonayo.
 
Back
Top Bottom