utanashati: Mpangilio wa veranda na sebule yako...

utanashati: Mpangilio wa veranda na sebule yako...

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,687
Katika kipengele cha mitindo na utanashati, leo tutajikita katika kuangalia mpangilio wa veranda au sebule kama inavyofahamika na wengi.
Katika familia za kiafrika, sebule ni eneo muhimu ndani ya nyumba kwani ndiyo sehemu ya kwanza, ambayo mgeni hufikia kabla ya kujua maeneo mengine.
Ni eneo linaloweza kumjengea mtu au watu picha ya kujua wanaoishi ndani ya nyumba husika kutokana na mwonekano wa haraka haraka wa sehemu hiyo.
Endapo sebule itakosa mpangilio mzuri na unaoleweka, hata anayeishi ndani ya nyumba hiyo ataonekana hovyo.
Kutokana na hali hiyo ni vyema kuzingatia dondoo zifuatazo ili kuhakikisha sebule inakuwa na mwonekano mzuri kuliko eneo lolote ndani ya nyumba.
Mpangilio wa sebule kwa jumla
Ili kuhakikisha sebule ina mwonekano mzuri ni lazima kuwepo na mpangilio, utakaoonyesha kila kilichomo ndani ya eneo hilo kwa nafasi yake.
Siyo lazima yawepo makochi ya gharama sana ili nyumba iwe na mwonekano mzuri, yanaweza kuwapo hata makochi ya kawaida, lakini yakapangiliwa kwa mtindo unaofaa, yakapendezesha nyumba.
Epuka kurundika vitu visivyo na ulazima wa kukaa sebuleni kama vile viatu, nguo, chupa na vitu vingine vinavyoweza kuleta picha mbaya vikiwapo eneo hilo.
Sebule inapendeza zaidi ikiwa na vitu vichache, vitakavyowekwa katika mpangilio sahihi na kulifanya eneo hilo kuwa na mvuto wa aina yake.
Makochi, meza ya kawaida na meza au kabati la kuwekea runinga na redio, ndiyo vitu vinavyopaswa kuwapo sebuleni na siyo vinginevyo.


Mapambo


Watu wengi hususan wanawake, hupenda kurembesha sebule zao kwa mapambo mbalimbali, wakati mwingine bila kufahamu kuwa mapambo hayo yanaweza kuharibu mwonekano wa nyumba.
Sebule ya kisasa, haipaswi kuwa na mapambo mengi zaidi ya samani na rangi ya kuta. Kwa jumla, hivyo vinaweza kuifanya sebule iwe na mvuto wa hali ya juu.
Fremu chache za ukutani, ambazo zinaweza kuwa za maua au picha nazo zina uwezo wa kuleta nakshi ya aina yake katika sebule na kuifanya ivutie na kupendeza.
Usafi
Pamoja na kuwa unaweza kuweka samani za bei ghali, lakini suala la usafi linapaswa kuwa muhimu zaidi ndani ya nyumba kwa kuhakikisha muda wote sebule inapitika na kutazamika.



mcl
 
Naungana nawe katika hili lakini mi zaidi napendelea kuwekeza zaidi chumbani na kumaliza ufundi wote huko kwakuwa hapo ndipo mahali niwekapo mgongo wangu mimi na mtima wangu
Sebuleni ni kwa ajili ya wageni zaidi panafaa kupendezeshwa lakini bedroom napo tusipasahau kabisa
 
Mi napenda sana bed room iwe tulivu;
walau ikaribiane na hii hapa:
small-bedrooms.jpg
 
Hapa umeweka picha, umenikumbusha picha za millard ayo kwenye instagram..

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
source please

"miss neddy" source ni mimi mwenyewe! Baada ya kuangalia SEBULE kwangu, kila pande imejaa makandokando kibao; kwenye VERANDA! ndiyo kabisa; viauti, vinguo vya watoto na vibakuli vya uji' Juu ya kabati kumejaa makorokoro kibao' na mengine hayatumika zaidi ya miaka mitata! Loh!
 
Naungana nawe katika hili lakini mi zaidi napendelea kuwekeza zaidi chumbani na kumaliza ufundi wote huko kwakuwa hapo ndipo mahali niwekapo mgongo wangu mimi na mtima wangu
Sebuleni ni kwa ajili ya wageni zaidi panafaa kupendezeshwa lakini bedroom napo tusipasahau kabisa

"mshana jr" umenena! kuhusu SEBULE' tulio wengi tunapajali kuliko huko kwa "BEDROOM" kuna sehemu nyingine tangia kitanda kimewekwa hawajawai safisha uvunguni' huko utakuta vumbi, nguo chafu zilizovaliwa juma zima, vyup* na vitaulo' ukitazama pembezoni mwakuta juu unakutana buibui kibao, loh! na Kama chumba hakina ceiling roof...!
 
Mi napenda sana bed room iwe tulivu;
walau ikaribiane na hii hapa:
small-bedrooms.jpg

"Mamndenyi" nami hii nimeipenda!
Lakini tulio wengi tunaishi kwenye nyumba za kupanga maeneo yenye msongamano; kama Sinza, Buguruni, Mazese Uwanja wa fisi, Kinondoni nk.
 
Mwaka Mungu atakaokujalia
na wewe utakuwa na kwako;

Usijali; wengi tulianzia huko huko.

"Mamndenyi" nami hii nimeipenda!
Lakini tulio wengi tunaishi kwenye nyumba za kupanga maeneo yenye msongamano; kama Sinza, Buguruni, Mazese Uwanja wa fisi, Kinondoni nk.
 
"miss neddy" source ni mimi mwenyewe! Baada ya kuangalia SEBULE kwangu, kila pande imejaa makandokando kibao; kwenye VERANDA! ndiyo kabisa; viauti, vinguo vya watoto na vibakuli vya uji' Juu ya kabati kumejaa makorokoro kibao' na mengine hayatumika zaidi ya miaka mitata! Loh!

acha uwongo mkuu hii habari yako source ni GAZETI LA MWANANCHI JUMAPILI TENA LA JANA
 
"Mamndenyi" nami hii nimeipenda!
Lakini tulio wengi tunaishi kwenye nyumba za kupanga maeneo yenye msongamano; kama Sinza, Buguruni, Mazese Uwanja wa fisi, Kinondoni nk.

ni malengo tu wee jiwekee kuwa one day yes kumbuka perception creates reality
 
acha uwongo mkuu hii habari yako source ni GAZETI LA MWANANCHI JUMAPILI TENA LA JANA

...umepatia! kumbe unajua maana ya "mcl" ! "Mwananchi Communication Limited"
 
Back
Top Bottom