MAMMAMIA
JF-Expert Member
- Feb 26, 2008
- 3,811
- 1,603
Hapo ninakubaliana na wewe. Nimeangalia kwenye makamusi maana yake zinalingana na haya uliyosema.Well. . . mi nadhani ni ile hali ya kitu kunoga/kufurahisha nafsi ya mtu.Iwe kwa chumvi, sukari au limao au hata nje ya vitu tunavyoonja kwa mdomo, kikinoga mtu anaweza kusema ni kitamu.
*Utamu: hali ya kunoga kwa kitu, mambo au hali. (Raha - hii ni nyongeza yangu).
*Utamu: Sweetness, deliciousness. Ya mwanzo inahusu zaidi ladha tamu, ya pili inahusu zaidi hisia.
Mfano, anayepigwa makonde anaumia lakini wanaweza kuwepo watazamaji wakaona/wakahisi utamu/raha kuona mtu anavyochakazwa au ufundi wa mchakazaji.
*Maana zote zimetoka kwenye makamusi ya TUKI ambako pia wametoa maana za neno tamu. 1 -enye ladha ya sukari. 2 -enye ladha ya kufurahisha kinywani. Mf. Nyama hii ni tamu. 3 -enye kufurahisha hisia. Mf. Mziki huu mtamu.