Utamu wa mabasi ya mwendokasi

Mkuu umenifanya nicheke sana. Kweli aisee hakuna kulipiana nauli.
 
Duh..... Hiyo ni kali kuliko Bujibuji.

Kwa hiyo wewe unawapiga vita sana wale wapenda miteremko kwenye daladala wanaopenda kulipiwa nauli, hususani wale wa jinsia fulani..........
 
Vile Vile 'machungu' mengine ya mabasi ya mwendo kasi ni kwa kuwa hawana cha ofa za walimu wala wajeda.

Kwa kuwa mashine za DART hazimtanbui Mwalimu wa Makonda wala wale walinda usalama wetu.
 
Hata ukikutana na mtu anayekudai kwa siku nyingi mfano umepandia Ubungo Terminal, unashukia tu mbele pale Tanesco umbali wa mita mia 2 tu unabadili basi kwa nauli ile ile.
Huu ndio mwendokasi bwana.
Hii safi sana, kuna wakati nilitaka kwenda kimara kuonana na jamaa..akanipigia akasema na yeye anakuja wakati huo nishapanda brt..nikashuka nikaenda upande wa pili nikapanda lingine tukakutana town
 
Kwel dar ndo TZ wanafaidi kwel, sisi wa huku vijijin tunasikilizia kene bomba
 
Magufuri au kikwete?


Haijalishi TanZania ni moja, na Uraisi wa TZ wanapokezana vijiti, hakuna Raisi aliyenzisha kitu chake kwa 100% TZ, Nyerere alipokea ktk kwa Wakoloni, Mwinyi alipokea ktk kwa Nyerere, Mkapa alipokea ktk kwa Mwinyi, Kikwete ktk kwa Mkapa na Raisi Magufuli ktk kwa Kikwete...
 
Back
Top Bottom