....:::Naam::.....
Nilitoa kama utangulizi hapo ili nitakapoanza kutoa maelezo yaende ndani ya kile nilichotangulia kusema..
Unapokuwa na binti katika mahusiano ya kimapenzi kiujumla inapunguza ile hamasa ya kuitamani ndoa sababu tayari mnakuwa mmeshajuana, na msingi mkubwa wa hayo mahusiano kwa wakati huo unakuwa ni ngono. Ni swala ambalo nikowazi kabisa thamani ya mahusiano ya watu wanaofanya tendo na wasio fanya ikotofauti kabisa,,inapotokea mkajuana thamani ya mwanzo inakuwa sio sawa,,hapa ni sawa kusuburia chakula kati ya mtu mwenye njaa kabisa na mtu ambae ameshaweka tonge mbili mdogomo japo hajashiba.
Angalizo; Nipinge kwa hoja sio maswali, sikatai maswali lakini ni vizuri tukapingana kwa hoja ili tuweze kutengeneza mtililiko mzuri wa majadiliano,,maswali yasichukue sehemu ya hoja.