Utamu au uchungu ..!?

Utamu au uchungu ..!?

wala besti usifungue hiyo thredi kwani utajaza server bure hapa panapotosha kukupa ushauri

wewe umefanya jambo la mbolea kama kweli hujamgusa huyo mbinti wa watu, endelea na msimamo wako huohuo wala usiache ila msigusane mtawaka tamaa na kufanya hicho kitendo lala
cha kufanya wewe kaa na huyo binti mweleze kuwa hutaki kufanya KITENDO LALA mpaka ndoa yenu ifike
na ndoa ikifika niite mm niwe MSHENGA wa hiyo ndoa yenu

Najaribu kutafakari hii topic maana inanihusu kwelkweli. Myself niko kwenye uhusiano na mdada 1 amabye bd yuko college, Moyoni mwangu napata amani sna hata ninapoomba Mungu kuhusu mke nasikia ohoni kuwa huyo uliyenae ndo wangu . Hatujafanya mapenz zaid ya kushikana na mengneyo . Kuna wazo huwa linakuja kuwa nikae nae mpak nifunge ndoa ndipo nimjue hy mwenz wangu kimwili. Lakini nkiangalia dunia hii huy mwanamke ataniona mtu wa namna gani nkimwambia hivyo bdo niko kwnye hatihat kwelkwel nampenda huy dada maana Ushuhuda wa Rohoni ndiye mke mtarajiwa hebu nisaidien au nifungue thread ya Yangu Yenye Title: Niko NJIA PANDA
 
thamani ya ndoa ni ile hali ya watu wawili waliomo kwenye mapendo
pasipo kushirikiana kabla na kushirikiana baada ya KITENDO LALA

hiyo ndo thamani ya ndoa kwani mshiriki kwenye KITENDO LALA mapema
kunaleta kutokuaminiana tena kwani uaminifu huondoka kwa kuwa pamoja
kabla pasipo baada ya ndoa

Thamani ya ndoa ni mambo mangapi?
 
thamani ya ndoa ni ile hali ya watu wawili waliomo kwenye mapendo
pasipo kushirikiana kabla na kushirikiana baada ya KITENDO LALA

hiyo ndo thamani ya ndoa kwani mshiriki kwenye KITENDO LALA mapema
kunaleta kutokuaminiana tena kwani uaminifu huondoka kwa kuwa pamoja
kabla pasipo baada ya ndoa

Kwahiyo kwa maelezo yako haya thamani ya ndoa ni Tendo la ndoa,si ndio?
 
Hata brand NEW CAR kabla haijaingia sokoni TEST is a MUST
But kwa wabuduo/wakristo ni DHAMBI kuonja kabla ya kuhalalishwa!
:israel:
 
Kumbuka serekalini ukiishi na mtu kwa muda wa miezi 6 kwenye chumba kimoja na mkawa na uhusiano, tayari ni mkeo

so iwapo wameishi pamoja hiyo miezi sita au zaidi na ikitokea mwanaume anataka kuoa, mwanamke anaweza zuia hiyo ndoa au?
 
Kila kitu kinamuda kwasababu huko zamani kuna mambo mengi na tabia nyingi ambazo kwa sasa zimeshika kasi hazikuwepo, pili siku hizi ukutanaji wa wapenzi ni tofauti na zamani mfano ukiangalia wazee wetu wengi walioana wakiwa wanatoka kijiji kimoja au maeneo karibu, na hata kama mwanaume alikuwa akipata kazi mbali ulipofikia muda wa kutaka kuoa basi alifunga safari kwenda nyumbani kuoa hivyo alioa mtu ambae anamfaham na hata mwanamke aliolewa na mtu anaemfaham. Ni tofauti na sasa watu tunakutana hata kwenye daladala tayari wapenzi, unajikuta upo kwenye mahusiano na mtu unaemfaham kuanzia siku mlipotongozana sasa kwamahusiano ya sasa kuanza kukaa ni muhimu na ndio mana hili swala la kutongoza na kuoa limesababisha migogoro mingi ya ndoa sasa hv, mfano ndoa inavunjika baada ya miezi mitatu moja kwa moja unapata jibu hawa ni watu waliokuwa hawafahamiani

dah! sisi enzi zetu ndoa ilikuwa zaidi ya kujamiiana. ndoa ilikuwa ni sawa na kuongeza ukoo, hivyo ilituwia rahisi zaidi kuoa kijijini tutokako kwani tulikuwa tunaoa katika ukoo tunao ufahamu vyema. hata kama akitokea mtu kuoa nje ya kijijini kwake basi ilikuwa shurti kupeleleza huo ukoo au watu wachache watokao ukoo huo.

siku hizi naona vijana wetu wanalenga kwa binti. kumfahamu binti ndio kigezo tena sio kumfahamu tabia tu, bali pia katika yale mambo. ndio hapo unakuta mtu anataka kuishi kwanza na binti kwa kisingizio cha kufahaminiana. bahati mbaya siku hizi usanii ni mwingi hivyo watu huficha "makucha" katika hicho kipindi cha kufahaminiana. na makucha hayo hutokeza iwapo ndoa itatokea. hii ukichanganya na ndugu unaoanza kuwafahamu baada za ndoa basi hukawii kusikia watu wakilalama "ooh mi sikujua...ooh, mawifi hivi, mama mkwe vile, shemeji nae!...".

kuishi pamoja kabla ya ndoa haisaidii ndoa ni fix tu...
 
Mie kwa maoni yangu kuishi pamoja kabla hamjafunga pingu za maisha si sawa maana mara nyingi hasa wanaume baada ya hili kutokea wengi wao huanza kusogeza kalenda kuhusu ni lini harusi itafungwa na hatimaye miaka hukatika hata anayetaka kuolewa kukata tamaa na kuacha kuulizia. Kuhusu tendo la ndoa pamoja na kuwa vitabu vya dini haviruhusu hili kabla ya ndoa dunia ya leo imebadilika sana watu wanajua mengi sana kuhusu tendo la ndoa. Hivyo kabla ya kufunga pingu za maisha wengi hupenda kujua kama kuna compatibility kwenye idara hiyo au ni midebwedo tu. Wahusika wakisharidhishana katika idara hiyo basi pingamizi linakuwa halipo tena.




Ni kama kawaida siku hizi watu kuoana wakati wameshakutana kimwili au pengine kuwa tayari wameshaishi kama mke na mume,nadhani jambo hili lilianza zamani sana kwani wengine tulizaliwa wakati wazazi wetu hawajaoana kwa maana ya kufunga ndoa

Hili jambo limekuwa kama kawaida lakini je ni kweli?

Kuna jamaa yangu mmoja tuliwahi kujadiliana kuhusiana na hili jambo la kuanza kuishi kinyumba kabla ya kuoana au mnaweza kutumia siku kadhaa kwenye wiki mkiwa mnalala pamoja na pengine kutumiana kama mke na mume na wakati mkiwa pamoja huduma zote ambazo mume au mke anatakiwa azipate mnakuwa mnapeana

Huyu jamaa yangu yeye alisema kuwa kitendo cha kuishi pamoja kabla ya kuoana au kutumia siku kadhaa kwenye wiki mkiwa pamoja kinasababisha watu hao kutokuja kuoana baadae kwasababu mnakuwa mmeshazoeana.Jamaayangu huyu alikwenda mbali sana akasema kuwa hata kitendo cha kubanjuana kinasababisha watu kutokuja kuoana

Mimi nilikuwa na mtazamo tofauti kidogo nae,nilimwambia kuwa vitendo hivyo havisababishi hilo ila vinaweza vikawa sababu za kuoana au kutooana yaa ni unaweza ukamuoa au kuolewa na mtu kwasababu hii au kutoingia nae ndoani

Cha msingi nilichosema ni kuwa kile ambacho mtu anakifanya kuwa kama priority ndio kitakuwa tatizo kama hakitakuwa chamsingi

Hebu niambie wewe unaonaje suala hili?
Kuishi pamoja na kubanjuana kabla ya kuoana kunasababisha ndoa kuwa chache au hakusababishi?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom