Utamsimulia nini mjukuu wako? Ni swali na ushauri tu ndugu yangu Kibunango! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utamsimulia nini mjukuu wako? Ni swali na ushauri tu ndugu yangu Kibunango!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mag3, Oct 5, 2010.

 1. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #1
  Oct 5, 2010
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Pamoja na kumtaja Kibunango, huu ushauri wangu ni kwa wazalendo wote wa Tanzania wanaolipenda na kulitakia mema taifa letu.

  • Fikiria baadaye baada ya miaka mingi utakapokuwa umekaa na mjukuu wako ukimsimulia historia mpya ya taifa ilivyoandikwa mwaka 2010.
  • Fikiria faraja utakayokuwa nayo kumjuza ukombozi ulivyopatikana mwaka huo na kwamba wewe babu yake ulikuwa sehemu ya hayo mabadiliko muhimu.
  • Fikiria heshima atakayokupa mjukuu wako akifahamu wewe ulishiriki kikamilifu katika kulikomboa taifa mikononi mwa wale waliokuwa na nia ya kuliangamiza.
  • Fikiria fahari utakayoisikia ukikumbuka kwamba wewe pamoja na wazalendo wengine mliweza kuipiga mweleka chama kilichoididimiza nchi kwa miaka hamsini.
  • Fikiria atakavyoweza kutamba mbele ya rafiki zake kuwa babu yake alikuwa moja wa wanaharakati waliowezesha misingi ya utawala bora na maisha bora.
  • Fikiria amani utakayokuwa nayo moyoni ukiwaona wajukuu zako wanafurahia maisha bora kwa sababu tu hukukubali kuhadaiwa kwa kanga na kofia kuuza kura yako.
  • Fikiria, fikiria, fikiria........
  Kibunango et al, au mko tayari kujuta mkiona wajukuu wenu wanavyoteseka kwa sababu tu hamkutimiza wajibu kwa kutetea matumbo yenu badala ya maslahi ya taifa ? Hili nalo swali, naomba majibu ndugu yangu.

  [​IMG]

  Tumuunge mkono Dr. Slaa na kwa pamoja tuiandike upya historia ya taifa letu.
   

  Attached Files:

 2. S

  Selungo JF-Expert Member

  #2
  Oct 5, 2010
  Joined: Sep 23, 2009
  Messages: 1,273
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mag3.

  Hivi unategemea Kibunango akupe majibu sahihi katika hili? Kwa taarifa yako hana kauli tena, hata kijitawi chao cha CHMA CHA MAFISI kimesambaratika. Kila mmoja lwake. Member wengine wanauliza jamani tawi la CHADEMA lipo wapi hapa mjini?

  Pole Kibunango, umeyaona mambo ya KYELA? Sijui mkulu atazimika tena akiona hilo nyomi?
   
 3. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #3
  Oct 6, 2010
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Mkuu Selungo je ameaona ya Tunduma ?
  [​IMG]
  Watanzania saa ya ukombozi ni sasa, wewe wangoja nini ?
  Kibunango, Kasheshe, Gembe, Mwiba, Malaria Sugu, Kiranga, Maggid n.k.
  Achaneni na zilipendwa, andikeni historia tujenge taifa jipya
  Siku zayoyoma na tsunami inakuja, je kwa ukaidi wenu mtaizuia ?
  Wengine tulitambua mapema na tukaona alama za nyakati.
  Sasa tumekaa raha mstarehe, tukiwachekelea mnavyohangaika.
  Jua limechomoza, bye bye - giza halina nafasi tena.

   
 4. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #4
  Oct 6, 2010
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Mkuu mag3

  Hoja zako zimelala katika hisani, nami kwa kuwa sitegemei hisani zaidi ya juhudi zangu binafsi katika kujikomboa na ulofa sina sababu yoyote ya kuunga mkono ghasia hii inayoendelea hapa jamvini na nchini kwa ujumla. Ingependeza kukujibu kwa kila hoja ulioweka mbele yangu, hata hivyo baada ya majumuisho nimeona zengine zinajirudia ama zima mantiki sawa.

  Kwa ufupi naweza kusema hivi...:

  • Historia mpya katika Tanzania haiwezi kuletwa na mtu ambae tayali amewahi kuwa katika system. Mifano ipo mingi katika hili, kwa ukaribu unaweza kuangalia siasa za Visiwani.

  • Siwezi kuwa au kujisifia kuwa sehemu ya mtu/kiongozi ambaye mchana kweupe ameshindwa kujiheshimu katika maadili ya kifamilia. Nitawezaje kujisifia katika hili? Ama niwe miongoni mwa malofa wa karne hii, ambao wanaamii kuwa wanauwezo wa kufanya chochote kutokana na madaraka waliyonayo(slaa ni mbunge mstaafu ila kafanya kufuru kubwa kabla ya kupendekezwa kuwa mgombea urais!

  • Sijaona sehemu yoyote ambayo slaa and Chadema ambayo wataniwezesha kujuta iwapo ndoto za za mchana zitafanikiwa, kwani wao ni sehemu ya ile asilimia ya kufuata upepo. Mbaya zaidi kampeni zao zinalenga kuwepo na machafuko nchini, ambayo sitoweza kusimama kifua mbele na kujisifia.
   
 5. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #5
  Oct 6, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Afadhali Mkuu uendelee na slogan hii siasa acha, uko wapi leo nikucheck?


  Save Water Drink Beer. "Alcohol doesn't solve any problem,
  But, if you think again, neither does milk."
  Vituko Vya Zen
   
 6. Nyange

  Nyange JF-Expert Member

  #6
  Oct 6, 2010
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 2,180
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Kwamba hapo zamani tulisoma na kutibiwa bure, lakini wezi walipoingia madarakani, wakafuta hayo yote, na kuhakikisha hela ya serikali inaingia mifukoni mwao, ndipo uchaguzi wa 2010 tukawang'oa wote na kuweka viongozi wapya waadilifu!
   
 7. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #7
  Oct 6, 2010
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Labda sijajua system ya Tanzania sasa ikoje! ni vema ukanyumbulisha hoja yako.. so long is just a cheap crap!
   
 8. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #8
  Oct 6, 2010
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Tampere...
   
 9. The Dreamer

  The Dreamer JF-Expert Member

  #9
  Oct 6, 2010
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Seriously, kazi ipo mwaka huu
   
 10. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #10
  Oct 6, 2010
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  To be honest natamani kuona hawa wandugu wakipiga kura October 31. Patachimbika!
   
 11. Mtende

  Mtende JF-Expert Member

  #11
  Oct 6, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 4,072
  Likes Received: 338
  Trophy Points: 180
  kwa kweli uchaguzi wa mwaka huu utanipa cha kumsimulia mjukuu wangu
   
 12. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #12
  Oct 6, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  kudadadeki. Kibunango anajali kura mezani pa mfalme. Mambo ya wajukuu yanamhusu nini? wanawe watakuwa wamekimbilia ulaya kama wana wengi wa mafisadi walivyo sasa. Yeye ni sehemu ya ufisadi huo.
   
 13. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #13
  Oct 6, 2010
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Pengine sijui maana ya ufisadi, ama sijui ufisadi unachukuliwa vipi na nyie! Hebu jaribuni kutoa boriti katika macho yenyu kabla ya kuona kibanzi katika macho ya wengine.
   
 14. Mantissa

  Mantissa JF-Expert Member

  #14
  Oct 6, 2010
  Joined: Jul 24, 2010
  Messages: 870
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Tafuta kamusi ya kiswahili utapata ufafanuzi zaidi kuhusu swali lako. Pia usitumie maneno matakatifu kwa kutetea upumbavu.
   
 15. m

  mapambazuko Member

  #15
  Oct 6, 2010
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ni vyema bwana kibunango akaelimishwa hivi kuwa kwa sasa ni lazima kufanyika kwa kilajuhudi ili kuhakikisaha kuwa lile jumba la maamuzi linaluwa na wabunge ambao wanawiana kwa idadi swa ili maamuzi ya mlae ndani yawe ya kitaifa na sio ya kichama kama ambavyo tumekuwa tukishuhudia hawa jamaa wa CCm wakifanya kama ulimsikiliza siku ile mheshimiwa mmoja alichosema kwenye mdahalo wa wabunge vijana uliyorushwa na ITV au Star tv kama sikosei na wana jf wengi ni waelewa wanachokihtaji ni kuiona Tz yenye mabadiliko ,ccm ya sasa siyo ile ya leo imezunguukwa na manyag'au ni kweli we utapata na hao wajukuu zako je wakikuta ufamilia,utabaka wataanzaia wapi?

  acha kujifikiria wewe ubinafsi hatari,wafikirie waTz wajao ndio maana nchi za kiafrika haziendeleei tunatabia za kujifikiria kwa umimi na si vizazi vijavyo be care!! na kauli zako we need changes ambazo lazima ziwe na pahala pa kuanzia na mtu wa kuzianzisha hata dr slaa naye angeliweza kujifikiria kama ubunge nimeshapata sasa sina haja ya kuhangaika na mtu please chunga hoja zako kama ccm wako wengi zaidi yako we unafikiri kinachotokea zanzibar ccm wote wanakipenda lakini hawana jinsi ni lazima mabadiliko yawepo kwa faida ya wanzanzibar wote cha muhimu ni wapinzani kujipanga hilo ndilo tatizo kubwa mabadiliko yatakuja tu na ndo yameanza
   
 16. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #16
  Oct 6, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Tafuta kamusi ya kiswahili utapata ufafanuzi zaidi kuhusu swali lako. Pia usitumie maneno matakatifu kwa kutetea upumbavu.
  Tafuta kamusi ya kiswahili utapata ufafanuzi zaidi kuhusu swali lako. Pia usitumie maneno matakatifu kwa kutetea upumbavu.
  Tafuta kamusi ya kiswahili utapata ufafanuzi zaidi kuhusu swali lako. Pia usitumie maneno matakatifu kwa kutetea upumbavu.
   
 17. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #17
  Oct 6, 2010
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Nimekuelewa ndugu yangu, nilijua tangu mapema kuwa huwezi kuwa na jibu.

  • Utajibu kitu gani kama Raisi wako anawapigia magoti wahalifu akiwaomba warudishe fedha walizokwiba.
  • Utajibu kitu gani wakati aliyekula kiapo kuheshimu na kulinda anakuwa wa kwanza kuivunja.
  • Utajibu kitu gani mgombea Uraisi anasimama majukwaani kuwanadi washtakiwa/wahalifu.
  • Utajibu kitu gani kama chama unachokihusudu kimegeuka kuwa kokoro linazoa kila aina ya uchafu.
  • Utajibu kitu gani gani kama rushwa, hujuma na vitisho ndiyo mitaji ya CCM kushinda uchaguzi.
  Nakubaliana na wewe kuwa yanayoendelea hapa nchini kwa sasa hivi ni ghasia na wananchi lazima tuchukue hatua kuyashughulikia. Ndio maana ndugu yangu Kibunango, kama kweli unaipenda nchi yako muunge mkono Dr. Slaa tuutokomeze upuuzi huu kwa kuung'oa mzizi wa fitina - CCM.
  Tanzania bila CCM yawezekana !
   
 18. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #18
  Oct 6, 2010
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Mapinduzi ya kweli yanaanzia kwa mtu binafsi, ni nafsi ya mtu umtuma kubadilika. Iwapo mtu binafsi ameamua kubadilika hakuna cha kumzuia. "We need change" ni kauli ambayo imeanzia kwa mtu mmoja na kuweza kuenea kwa kasi kwa wengine ambao walipendezwa na kauli hiyo na kuona kuna umuhimu wa kuwepo na changes hizo.

  Hakuna asijejua ulofa mkubwa wa watanzania wa leo, ni vizuri sana kuwepo kwa mabadiliko yenye kuweza kuwatoa watanzania wengi kwenye ulofa huu! Zaidi ni vema kwa kila mtanzania kutamani kuendelea yeye binafsi pasipo kupangiwa na mtu yoyote yule. Hii ndio maana ya changes kwangu

  Iwapo slaa na Chadema yake wameshindwa kunishawishi, sio ajabu, kwani sioni changes zozote toka kwao, zaidi ya kutuendelezea ulofa miongoni mwetu. Upuuzi wa slaa upo wazi na kila mtu anaujua... ila kwa kuwa watu wengi wameamua kumpenda kipofu basi watasema slaa ana kengeza.

  Jaribu kufuatilia hotuba za slaa katika siku za karibuni na utajua ni wapi anataka kulipeleka taifa hili... Kumbuka sio yeye binafsi aliyekuwa na nadhiri ya kuongoza taifa hili..!
   
 19. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #19
  Oct 7, 2010
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Awali ya yote ni vema kujua nchi hii sasa ina uwelekeo wa aina gani! Kwa muda mrefu system imejaribu kutupangia kila kitu katika maisha yetu. Hili ni tatizo tena kubwa kiasi kwamba hata sie tunaoweza kujibizana hapa mtandaoni wengi wameshindwa kuligundua zaidi ya kupeleka lawama zao kwa chama tawala. Ukirudi nyuma kidogo kwenye system hiyo hiyo wapo Chadema na Vyama vingine! Inashangaza! Na sio chadema ambao kwa ilani ya chama chao wameweza kutambua hili! Ajabu. Ukisikiliza kampeni zao hazina lolote jipya la kuweza kumwondoa mtanzania wa kawaida katika kupangiwa nini cha kufanya! Je hapa unaweza kusema kuwa chadema hawana jipya? Binafsi naweza kusema hivyo.

  Ni wakati huu ambapo tunapaswa kujua kuwa kila mwananchi anahitaji kujua ni nini anataka katika maisha yake... na jumuija yake. Huu ndio wakati rasmi wa vijiji, miji na majiji kustoa viupambele vyao badala ya kusubili kupangiwa na vyama ama serikali. CCM hili wameliona, na ninawashukuru kwa hilo.

  Nikirudi nyuma kwenye maswali yako bado nayaona yamejaa mawazo ya kupangiwa kila kitu, na sio mawazo ya kiukombozi. Hapana shaka kila mtu anajua kuwa You're innocent until proved guilty, hivyo sioni shida yoyote ya watuhumiwa kutopigiwa kampeni. Zaidi sio kweli kama JK amewapigia magoti wahalifu....Zaidi ametoa nafasi kwa asasi husika kufanya kazi zao bila kuingiliwa.

  CCM ndio chama mama, iwapo unazungumzia vyama! Chama kokoro, basi ni vema ukaangalia kwa undani zaidi. Vyama kama Chadema, ambavyo bila kutafakali vimeweza kukumbatia makapi ya CCM bila haya. Vyama vyote zaidi ya CCM vimekuwa vikikenua meno pale mazagazaga ya CCM yanapotua kwenye vyama vyao. Mbaya zaidi ni kuweza hata kuwapa nafasi ya kugombea nafasi mbalimbali katika vyama hivyo. Hapa utajijua ni chama kipi kokoro!

  Rushwa kwa miongo minne sasa imekuwa inatutesa sana, wengi tunaojua maana ya rushwa, tunajua ni adui mkubwa wa haki. CCM kwa kila nafasi imejaribu kutokomeza tabia hii ya rushwa, hii ni pamoja na kutoa elimu ya rushwa kuanzia shule za msingi. Hata hivyo mafanikio sio mazuri kabisa... ! Ni tatizo kubwa na mbaya zaidi litazidi kuendelea kuwepo kwani hata huko Chadema kuna rushwa mbaya mno. Kutumia nafasi ya ubunge kulaghai wake za watu ni sehemu tu ya rushwa.

  Mwisho kabisa, siwezi kumuunga mkono slaa... Slaa ni fisadi na ni fisadi kiwembe, mwongo na asije jua anafanya nini na anataka nini! Hana nafasi ya kuwa ni mabadiliko ya nchi hii. **** slaa hakuwahi kuwa na ndoto yoyote ya usiku wala ya mchana ya kuongoza nchi hii kwenda kwenye mabadiliko. Ameamuriwa tu na kina Mbowe na Zitto kuchukua nafasi hii, ndio maana kila siku anajikanyaga... yeye binafsi ndie mtupu kabisa, eti anasema kapata msukumo mkubwa toka katika watumizi wa kompyuta...! Shame on him Tanzania ina watu milioni 40, watumiaji wa net ni laki sita, yeye mwenyewe kwenye facebook ana washabiki elfu moja tu... Anataka kuongoza changes gani huyu?
   
 20. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #20
  Oct 7, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Shame Kibunango Shame!
  Hapa ndipo huwa nawaona CCM mnaufahamu mdogo sana. Kwa taarifa yako Slaa kuwa na fans 1000 kwenye face book sio shida. Hao ni wawakilishi wa watanzania wote 40,000,000. Ndio maana wapiga kura sio watanzania wote wanaopiga kura bali bali ni wachache tu. Kuna watu 40 milioni na wanaopiga kura ni 19 milioni.

  Hivyo usijidanganye kwa vijihoja mfu hapa. Huyu anaependwa mitandaoni ndiye anakusanya mass kubwa sana tena watu wakija voluntarily bila kusombwa na mafuso! Na ndio chaguo la watanzania sasa hivi. Achana na huyu msanii anayeangushwa kila siku kwa mapepo kwa mujibu wa sheik Yahya.
   
Loading...