Utamaduni wa woga ndiyo umempa Lissu na Seif umashuhuri

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,629
8,806
Lissu na Seif ni mashuhuri sana kwasababu hatuna viongozi majasiri wengi nchini kwetu. Tanzania imekuwa nchi ya kuogopa tunaogopa mabeberu, tunaogopa wakenya, tunaogopa wachagga!, tunaogopa wapemba, tunaogopa ndugu zetu wa diaspora, tunaogopa serikali! .

Wakati wa wakoloni nchi yetu ilikuwa na viongozi majasiri sana Karume, Nyerere, viongozi wa kimila, kawawa. Lakini kizazi kipya cha wakina Mkapa na waliofuata ni waoga kama kuku.

Sasa wakitokea viongozi ambao ni safi hawana rekodi za rushwa na ni majasiri watu wanapenda maana hatuna mashujaa kwenye jamii zetu siku hizi. Yaani wanawake wengi ni mashujaa Yukiko wanaume. Hebu tafuta shujaa ndani ya CCM kama Halima mdee hata wanaume! hakuna. Ni tafutie watu waliowekwa vizuizini kama Seif mwaka 1987 au kwenda jela kwa Siasa, au kupigwa kwasababu ya Siasa, kuchukuliwa biashara kwasababu ya Siasa kama Mbowe hakuna na ndiyo maana kuna kundi ambalo litaenselea kuwahabikia sio kwasababu ya chama bali ushupavu wao. Msishangae watu wamehama CUF kwenda ACT na Seif sio chama ni ushupavu unaovutia watu.

Viongozi wote wanakumbukwa kwa ushujaa wao sio umri, pesa wala Kabila.
 
Kuna ushujaa na umbumbumbu, mtu mbumbumbu hana cha kuofia kwa sababu akili anakua kaazima hana uwezo wa kutathimini matokeo.

Kiukweli hakuna mwanasiasa mbabe kama Mkapa r.i.p na mzee Magufuli
 
Umashuhuri wa SEIF umemsaidia nini tuanzie hapa kwanza.
Unafikiri alikuwa Makamu wa Kwanza wa Raisi kuzembezembe tu????

Tena mwaka huu yule ndo Raisi Zanzibar. Sijui mtapeleka majeshi wapi mwaka huu. Zanzibar wanakataa wizi wa kura na Tanzania Vara tunakataa wizi wa kura mwaka huu
 
We mtu km Kangi anaona kuna Yesu duniani unategemea nini🤒🤒
 
Back
Top Bottom