Tuna nini cha kuwafanya DP World na wakala wake?

hermanthegreat

JF-Expert Member
Mar 2, 2021
871
2,070
Wakuu,

Naona Kama watanzania hatuna Cha kuwafanya Hawa DP World na wakala wao kwasababu

Sisi ni waoga
Tunaogopa kutoa sauti zetu kukemea Mambo yasiyo mazuri kwenye nchi yetu wenyewe.

Hatuna ushirikiano
Mfano, tumewaachia watu wachache watutetee akina mdude, hatuwezi kuwa wamoja kama nchi.

Sisi sio wazalendo
Watanzania wengi tunapenda maeneo au viwanja tunavyoishi tu na sio nchi yetu , yaani mtu wa Kigoma anaona anaona Kama Dar haimhusu hata ichukuliwe yote.

Ndiyo maana viongozi na wageni wengine wanatudharau Sana kiasi kwamba wanaoona hata hatuna jitihada za kujipenda wenyewe.

Tutabaki kwenye utumwa Hadi lini?
Tutachukua hatua gani Kama wakitumia nguvu kuichukua bandari bila kuwasikiliza watanzania?
 
Tatizo ni umasikini, ujinga na maradhi, hawa ni maadui watatu tangu tupate uhuru bado hatujawashinda. Mabwenye kama DP World wanawatumia kujiingiza ili kuteka mali za nchi kama bandari
 
TEC wamesema wamepitia kila familia nchi hii, kwa vile taasisi yao ni kubwa na zote wanasema zinapinga ndo maana wakaja na lile tamko......wanasema linatokana na 'maoni ya wananchi'.
 
Back
Top Bottom