Sentensi yako ya kwanza inabeba ujumbe mzito..."kusoma vitabu siyo ni kwamba lazima uwe darasani bali ni vizuri pia ukiwa nyumbani keke yako" ambao maana yake ni kwamba jukumu la kuwa na utamaduni wa kujisomea vitabu linakwenda beyond wizara ya elimu. Ni kweli kwa wanafunzi kuanzia chekechea Wizara ya Elimu ina jukumu hilo kwa kushirikiana na wazazi na jamii. Lakini katika ngazi nje ya shule ni jukumu la kila mmoja wetu mwenyewe kujijengea utamaduni wa kusoma vitabu. Watanzania wengi hatupendi kusoma, hata magazeti hatusomi....tunapenda kuangalia vichwa vya habari...mpaka televisheni siku hizi wana vipindi vya vichwa vya habari....watu utawakuta kwenye counter ya muuza magazeti wanaangalia vichwa vya habari. Yale magazeti ya udaku yanauzika sana sio sababu watu wanasoma, bali wanapenda kuangalia picha.
Hili jukumu la kujenga utamaduni wa kujisomea ni la kila mtu. Tubadilishe lifestyle zetu. Wenzetu nje hasa wazungu wana utamaduni wa kuwasomea watoto wao hadithi za vitabu kabla hawajalala, na wao wenyewe wakiingia kitandani hupenda kutafuta usingizi kwa kusoma kitabu. Sisi baada ya kutoka kazini tunakwenda bar kupiga mtungi, au tunakwenda kikao cha harusi, au tunakwenda kupiga siasa vijiweni.....ukirudi nyumbani watoto washalala (umemiss muda wa kusoma kitabu na wanao) umechoka kiasi cha kutoweza kujisomea gazeti ulilonunua leo, achilia mbali vitabu....sasa kwa utaratibu huo, tutamlaumu Kawambwa kweli? Serikali ndio ije majumbani kwetu kusimamia homework za watoto wetu? Serikali ndio ije kuwasomea vitabu watoto wetu?
Jukumu hili ni langu na ni la kwako. Hakuna mahala pa kukimbia. Upo msemo usemao "If you want to hide something from an African, put it in a book or simply write it down" huu msemo una ukweli ndani yake. Tukiamua tunaweza kuubadili.
Mahala pazuri pa kuanzia kujihoji.....wataalam wetu, waalimu wetu...wangapi wameandika vitabu vya watu kusoma? Barak Obama alipochaguliwa kuwa mgombea urais wa marekani vitabu viwili alitoa kuhusu maisha yake na uzoefu wake....hapo hajawa Rais. Sisi mpaka leo hii hatuna kitabu cha Rais Mstaafu Mwinyi wala Mkapa kuelezea experience yao ya uongozi katika kipindi cha miak 10 ambayo kila mmoja aliongoza. Mageuzi mengi yalitokea kipindi chao, mambo mengi makubwa, mazuri na mabaya yalifanyika. Kwanini hawaandiki vitabu kwa manufaaa ya vizazi vijavyo? Viongozi wa kesho watajifunza kutoka wapi yaliyo mazuri waendeleze, na mabaya wayaache? Pengine tuanzie hapo.....mtu akistaafu...,,aandike kitabu....serikali imsaidie kugharamia kupublish..
Pongezi kwa Mwalimu Julius Nyerere. Mzee George Kahama, Sir Andy Chande, Familia ya Mzee Kawawa, Balozi Juma Mwapachu na Rais Jakaya Kikwete.....walau wao na wengine wachache ambao sijawataja wamethubutu kuandika vitabu kuhusu maisha yao. Changamoto kwa historians wetu....andikeni vitabu kuhusu akina Chief Mkwawa na mashujaa wengine ili tuwafahamu.
Salaama nakubaliana nawe kwa asilimia 100. Jukumu la kuwa na utamaduni wa kujisomea vitabu ni la kila mmoja wetu. Big up!