Utamaduni wa kujisomea, kuelewa na siasa za Tanzania

Sentensi yako ya kwanza inabeba ujumbe mzito..."kusoma vitabu siyo ni kwamba lazima uwe darasani bali ni vizuri pia ukiwa nyumbani keke yako" ambao maana yake ni kwamba jukumu la kuwa na utamaduni wa kujisomea vitabu linakwenda beyond wizara ya elimu. Ni kweli kwa wanafunzi kuanzia chekechea Wizara ya Elimu ina jukumu hilo kwa kushirikiana na wazazi na jamii. Lakini katika ngazi nje ya shule ni jukumu la kila mmoja wetu mwenyewe kujijengea utamaduni wa kusoma vitabu. Watanzania wengi hatupendi kusoma, hata magazeti hatusomi....tunapenda kuangalia vichwa vya habari...mpaka televisheni siku hizi wana vipindi vya vichwa vya habari....watu utawakuta kwenye counter ya muuza magazeti wanaangalia vichwa vya habari. Yale magazeti ya udaku yanauzika sana sio sababu watu wanasoma, bali wanapenda kuangalia picha.

Hili jukumu la kujenga utamaduni wa kujisomea ni la kila mtu. Tubadilishe lifestyle zetu. Wenzetu nje hasa wazungu wana utamaduni wa kuwasomea watoto wao hadithi za vitabu kabla hawajalala, na wao wenyewe wakiingia kitandani hupenda kutafuta usingizi kwa kusoma kitabu. Sisi baada ya kutoka kazini tunakwenda bar kupiga mtungi, au tunakwenda kikao cha harusi, au tunakwenda kupiga siasa vijiweni.....ukirudi nyumbani watoto washalala (umemiss muda wa kusoma kitabu na wanao) umechoka kiasi cha kutoweza kujisomea gazeti ulilonunua leo, achilia mbali vitabu....sasa kwa utaratibu huo, tutamlaumu Kawambwa kweli? Serikali ndio ije majumbani kwetu kusimamia homework za watoto wetu? Serikali ndio ije kuwasomea vitabu watoto wetu?

Jukumu hili ni langu na ni la kwako. Hakuna mahala pa kukimbia. Upo msemo usemao "If you want to hide something from an African, put it in a book or simply write it down" huu msemo una ukweli ndani yake. Tukiamua tunaweza kuubadili.

Mahala pazuri pa kuanzia kujihoji.....wataalam wetu, waalimu wetu...wangapi wameandika vitabu vya watu kusoma? Barak Obama alipochaguliwa kuwa mgombea urais wa marekani vitabu viwili alitoa kuhusu maisha yake na uzoefu wake....hapo hajawa Rais. Sisi mpaka leo hii hatuna kitabu cha Rais Mstaafu Mwinyi wala Mkapa kuelezea experience yao ya uongozi katika kipindi cha miak 10 ambayo kila mmoja aliongoza. Mageuzi mengi yalitokea kipindi chao, mambo mengi makubwa, mazuri na mabaya yalifanyika. Kwanini hawaandiki vitabu kwa manufaaa ya vizazi vijavyo? Viongozi wa kesho watajifunza kutoka wapi yaliyo mazuri waendeleze, na mabaya wayaache? Pengine tuanzie hapo.....mtu akistaafu...,,aandike kitabu....serikali imsaidie kugharamia kupublish..

Pongezi kwa Mwalimu Julius Nyerere. Mzee George Kahama, Sir Andy Chande, Familia ya Mzee Kawawa, Balozi Juma Mwapachu na Rais Jakaya Kikwete.....walau wao na wengine wachache ambao sijawataja wamethubutu kuandika vitabu kuhusu maisha yao. Changamoto kwa historians wetu....andikeni vitabu kuhusu akina Chief Mkwawa na mashujaa wengine ili tuwafahamu.

Salaama nakubaliana nawe kwa asilimia 100. Jukumu la kuwa na utamaduni wa kujisomea vitabu ni la kila mmoja wetu. Big up!
 
Siku hizi tunasoma blog na maforum kama jamiiforum. Kuna mada za kusisimua na uchambuzi wa kina kutoka kwa wachangiaji mbalimbali. Tuna iPad na Smartphone na ebook readers. Tunasoma sana bro usiwe na wasiwasi
 
Hilo nalo neno,yaani kama Dar utakutana na bar 1,000 bila kuona hata public library moja.Lakini sishangai maana sidhani kwa watu aina ya Mungai,Magembe na Mulugo wangekuwa na fikra pevu zaidi kuhusu maana ya elimu. Pia serikali kwa ujumla wanadhani elimu inaishia shule za kata na kutolipa kipaumbele somo la sayansi ya kilimo huku upande wa pili wakiimba kilimo kwanza.

Magamba wanatakiwa wapumzishwe 2015 labda watu ndo wataamka lakini sasa ni kama watu hawajielewi kabisa.Inakuwaje maktaba na viwanja vya kujisomea vilikuwepo miaka ya 1970 lakini sasa hakuna kitu? Wanaosema wanasoma kwa social media ni matokeo ya fikra changa,la sivyo dunia isingekuwa inalilia maktaba iliyochomwa Timbuktu huko Mali na waasi wa Kiislamu wenye itikadi kali.

Pia idadi ya Watanzania wanaoweza kusoma kwa mitandao haizidi 0.07% ya raia wote na haitakuwa hadi 2100.La zaidi hata hao watumiaji wengi wanatafutana uchumba tu,porojo bila utafiti n.k Let's doubt everything...(John Dewey)
 
Tarehe 31 mwezi wa 12 mwaka 2012 kwenye ukurasa wangu wa facebook niliwashirikisha na kuwashauri watu kwa mwaka huu 2013 wajitahidi wasome vitabu vitatu ambavyo ni THINK AND GROW RICH, POOR DAD RICH DAD na THE RICHEST MAN IN BABYLON.

Nilitoa utaratibu kwa watakaovitaka vitabu hivyo kunitumia barua pepe zao na mimi kuwatumia vitabu hivyo kwa barua pepe bila gharama yoyote. Nilipata mwitikio mkubwa sana kwani mpaka mwezi wa kwanza unaisha nilikuwa nimewatumia watu zaidi ya mia mbili(200) vitabu hivyo. Kwa sasa ni miezi mitatu imekwisha tangu nilipowatumia watu vitabu, wachache wamenitumia ujumbe kuniambia jinsi gani walivyojifunza mambo mengi na mapya kutokana na vitabu hivyo.

Sijapata mrejesho kutoka kwa wengi, ila ni rahisi tu kutabiri kwamba asilimia kubwa ya watu niliowatumia vitabu vile hawajamaliza kuvisoma na baadhi hawajaanza kabisa kuvisoma.

Utaratibu niliokuwa naufikiria ni kwamba kama kwa mwezi mmoja mtu akasoma kitabu kimoja kwa sasa vingekuwa vimeisha na ningeandaa vitabu vingine niwatumie. Ila kwa sababu naona utaratibu huo ni mgumu kwa watu kuufikia nimefikiria utaratibu mwingine ambapo kila mwezi nitawashirikisha na kuwatumia watu kitabu kimoja wakisome.

Vitabu ninavyowashirikisha watu ni vitabu vinavyohusu maisha, maendeleo binafsi, biashara, uchumi, usimamizi wa fedha na mbinu za kutoka kimaisha. Ni vitabu vizuri sana kwani vinakupa mtazamo tofauti wa maisha hasa kwa kipindi hiki ambacho maisha yamekuwa magumu sana. Ni vitabu vizuri sana ambavyo wenzetu wazungu wanavisoma sana na vinawasaidia sana.

Sote tunajua utaratibu wa kujisomea vitabu ni mgumu sana kwa watanzania ila ni lazima tubadilike kama tunataka kwenda na kasi ya dunia la sivyo tutaachwa tukishabikia tu vya wazungu na kutegemea misaada.

Naomba maoni yako kuhusu huo utaratibu mpya wa kusoma kitabu kimoja kwa mwezi.

NAIPENDA TANZANIA.
 
Vitabu hivyo vina alot of pages mm niliwahi kukisoma think and grow rich nilipokuwa university kwa style ya maisha ya wabongo kumaliza kitabu kama hicho inaweza kuchukua miezi 6 hadi mwaka coz kuna kiu,ijumaa,sani nk vilevile facebook na twitter then usisahau kuna muda maalum wa kuangalia bongo movies lini mtu atasoma kitabu chako kaka chenye page kibao:nono:
 
Makirita Amani nikupongeze kwa jitihada zako binafsi juu ya hili unalolifanya, nikutie moyo kwani nia ni zaidi ya njia. Usikatishwe tamaa na mrejesho hasi kwani hawa wasomaji wa vitabu kwakua wanapata bure sio rahisi sana kuweka mkazo, kwani hawakutumia nguvu. Utamaduni wakujisomea pia ni kikwazo sana, ila ni bora mbegu moja idondoke kwenye udongo mzuri itakuzalia matunda. Kila la kheri.
 
Last edited by a moderator:

kitabu cha think and grow rich kina page 235, poor dad rich dad kina page 130, the richest man in babylon 164, sasa sijui wingi wa pages unaouzungumzia hapo ni upi.
hivyo vitabu sio vyangu mimi nawashirikisha watu kwa kuwa nimevisoma na ninahamu kila mtanzania avisome, vina msaada sana.
unachonishangaza unajiita american dream wakati maisha ya tanzania tu yanakupa shida, hao wamarekani wenyewe wanatoana sana, yani waliofanikiwa wanatumia muda mwingi sana kuwafundisha wenzao njia za kufanikiwa kupitia vitabu, dvd na semina.
tukiendelea hivi watanzania kwa kupinga mambo mazuri kwa excuse za kijinga tunaelekea kubaya.
 
asante mkuu nashukuru sana kwa kunipa moyo.
 
Tarehe 31 mwezi wa 12 mwaka 2012 kwenye ukurasa wangu wa facebook niliwashirikisha na kuwashauri watu kwa mwaka huu 2013 wajitahidi wasome vitabu vitatu ambavyo ni THINK AND GROW RICH, POOR DAD RICH DAD na THE RICHEST MAN IN BABYLON.

Nilitoa utaratibu kwa watakaovitaka vitabu hivyo kunitumia barua pepe zao na mimi kuwatumia vitabu hivyo kwa barua pepe bila gharama yoyote. Nilipata mwitikio mkubwa sana kwani mpaka mwezi wa kwanza unaisha nilikuwa nimewatumia watu zaidi ya mia mbili(200) vitabu hivyo. Kwa sasa ni miezi mitatu imekwisha tangu nilipowatumia watu vitabu, wachache wamenitumia ujumbe kuniambia jinsi gani walivyojifunza mambo mengi na mapya kutokana na vitabu hivyo.

Sijapata mrejesho kutoka kwa wengi, ila ni rahisi tu kutabiri kwamba asilimia kubwa ya watu niliowatumia vitabu vile hawajamaliza kuvisoma na baadhi hawajaanza kabisa kuvisoma.

Utaratibu niliokuwa naufikiria ni kwamba kama kwa mwezi mmoja mtu akasoma kitabu kimoja kwa sasa vingekuwa vimeisha na ningeandaa vitabu vingine niwatumie. Ila kwa sababu naona utaratibu huo ni mgumu kwa watu kuufikia nimefikiria utaratibu mwingine ambapo kila mwezi nitawashirikisha na kuwatumia watu kitabu kimoja wakisome.

Vitabu ninavyowashirikisha watu ni vitabu vinavyohusu maisha, maendeleo binafsi, biashara, uchumi, usimamizi wa fedha na mbinu za kutoka kimaisha. Ni vitabu vizuri sana kwani vinakupa mtazamo tofauti wa maisha hasa kwa kipindi hiki ambacho maisha yamekuwa magumu sana. Ni vitabu vizuri sana ambavyo wenzetu wazungu wanavisoma sana na vinawasaidia sana.

Sote tunajua utaratibu wa kujisomea vitabu ni mgumu sana kwa watanzania ila ni lazima tubadilike kama tunataka kwenda na kasi ya dunia la sivyo tutaachwa tukishabikia tu vya wazungu na kutegemea misaada.

Naomba maoni yako kuhusu huo utaratibu mpya wa kusoma kitabu kimoja kwa mwezi.
Kwa wale ambao hawakupata vitabu vitatu nilivyotoa mwanzo bonyeza hapa na uandike jina na email yako utatumiwa papo hapo.

NAWATAKIA HERI YA PASAKA WATANZANIA WOTE………..

NAIPENDA TANZANIA.

Mkuu hardcopies za hivi vitabu naweza kuvipata wapi hapa Dar,msaada wako mkuu Makirita Amani
 
Last edited by a moderator:
Mkuu hardcopies za hivi vitabu naweza kuvipata wapi hapa Dar,msaada wako mkuu Makirita Amani
hardcopy zinapatikana kwa wauza vitabu wa barabarani wale wanaopanga chini au kwenye meza, maeneo ya ubungo, kariakoo mtaa wa uhuru pale pembeni ya round about au posta mkabala na tanzania postal bank. pia waweza kuvipata kwenye bookshops kama scholastic bookshop iliyopo mlimani city.
 
Kujisomea vitabu nikipaji mkuu, sio kila mtu anaweza kusoma, hii ndio sababu kubwa ya vitabu vingi kuwekwa kwenye mfumo wa video ( movie ) ili ata wale wasioweza kujisomea wapate ujumbe kwa njia ya video.

Vitabu vyote ulivyovitaja, nimevisoma nikiwa form six, nimejijengea utaratibu wa kununua kitabu kimoja kila mwisho wa mwezi nikipata salary, kusoma vitabu kumeshakua sehemu ya maisha yangu, huwezi kumfanya mtu kuanza kusoma vitabu mda huu. Nijukumu langu mimi na wewe kujenga tabia hii kwa watoto wetu na wadogo zetu mapema, tupende pia kuwasomea hadithi ili wavutiwe na elimu iliyoko kwenye vitabu.
 
JF ni kila kitu Dr. km watu wangekua na ka utamaduni ka kujisomea mbona kila kitu kipo humu? Binafsi nina stock kubwa sana ya vitabu nilivyojipakulia humu of which vinanijenga mental,vinainspire,vinanijengea uwezo wa kujiamini zaidi na kunifanya nithubutu...
 
Makirita Amani nakupongeza sana kwa kazi nzuri ambayo haina mshahara moja ya njia ya kuulea umasikini kwa watanzania wengi ni kukosa desturi ya kujisomea.
Hata mimi sikuwa na desturi ya kusoma vitabu ila nimeangalia movies nyingi sana kiasi kwamba mara nyingine nimeanza kuona idea zinajirudia nimeamua kuhamisha mizuka kwenye vitabu na nina mpango wa kuwa na ka shelf au library ya kutunzia vitabu ili nimzoeshe na mwanangu ustaarabu huu.Ki ukweli nimefurahishwa na post yako wewe ni mwanamapinduzi wa ukweli kushinda hao wanaohimiza maandamano bila kumuandaa muandamanaji kwa elimu ya kujitambua.
We ni mmoja kati ya watanzania wachache wenye mapenzi mema na hii nchi.
 
Last edited by a moderator:
Kujisomea vitabu nikipaji mkuu, sio kila mtu anaweza kusoma, hii ndio sababu kubwa ya vitabu vingi kuwekwa kwenye mfumo wa video ( movie ) ili ata wale wasioweza kujisomea wapate ujumbe kwa njia ya video.

Vitabu vyote ulivyovitaja, nimevisoma nikiwa form six, nimejijengea utaratibu wa kununua kitabu kimoja kila mwisho wa mwezi nikipata salary, kusoma vitabu kumeshakua sehemu ya maisha yangu, huwezi kumfanya mtu kuanza kusoma vitabu mda huu. Nijukumu langu mimi na wewe kujenga tabia hii kwa watoto wetu na wadogo zetu mapema, tupende pia kuwasomea hadithi ili wavutiwe na elimu iliyoko kwenye vitabu.
unakosea sana mkuu, kila mtu anaweza kujifunza kitu mwa umri wowote alioko nao, ishu ni kuchange mentality tu. kazi unayoifanya ulifundishwa kuifanya ukiwa mtoto?? je hakuna vitu vingi na tofauti kabisa unavyovifanya kazini ambavyo hukufundishwa hata chuoni?? stop being negative bana, kila kitu kinawezekana, tatizo watanzania hatujui mambo ya msingi ni yapi ndio maana tunayumbishwa kama upepo.
 
Makirita Amani nakupongeza sana kwa kazi nzuri ambayo haina mshahara moja ya njia ya kuulea umasikini kwa watanzania wengi ni kukosa desturi ya kujisomea.
Hata mimi sikuwa na desturi ya kusoma vitabu ila nimeangalia movies nyingi sana kiasi kwamba mara nyingine nimeanza kuona idea zinajirudia nimeamua kuhamisha mizuka kwenye vitabu na nina mpango wa kuwa na ka shelf au library ya kutunzia vitabu ili nimzoeshe na mwanangu ustaarabu huu.Ki ukweli nimefurahishwa na post yako wewe ni mwanamapinduzi wa ukweli kushinda hao wanaohimiza maandamano bila kumuandaa muandamanaji kwa elimu ya kujitambua.
We ni mmoja kati ya watanzania wachache wenye mapenzi mema na hii nchi.

asante sana dada, tunajukumu kubwa la kuwakomboa watanzania wenzetu kifikra.
 
Hongera sana!! Usikate tamaa kwa kupata mwitikio (feedback) hafifu, kumbuka Watanzania wengi hatuna tabia ya kutoa mwitikio (au hata shukrani). Mimi ni miongoni mwa walevi wa kusoma vitabu. Hicho cha RICH PEOPLE IN BABLOON sijakiona. Naomba unitumie.
Utaratibu huu ni mzuri, nafurahi sana kuona watu wakiwashrikisha wengine mambo ya msingi. Ila naomba kama inawezekana, uwe na watu kwa ajili ya kuwatumia vitabu tuu. Nasema hivyo kwa kuwa nimeona katika huo mtandao una dhamira ya kuwatumia watu habari, pamoja na mengineyo. Kumbuka ya kwamba wengi wetu hatupendi Email zikawa na mambo mengi, ikizingatiwa hutushukua hata miezi kadhaa ndipo tufungue Email zetu, hivyo hatupendi tukute rundo la Email hata kulazimika kufungua kurasa kadhaa ndipo mtu apate Email anayoitaka.
Siri za dunia zimewekwa katika maandishi. watanzania tusome vitabu vyenye mambo ya msingi.
 
Hongera sana! Mimi ni miongoni mwa walevi wa kusoma vitabu. Hicho cha RICH PEOPLE IN BABLOON sijakiona. Naomba unitumie.
Utaratibu huu ni mzuri, nafurahi sana kuona watu wakiwashrikisha wengine mambo ya msingi. Siri za dunia zimewekwa katika maandishi.
asante na karibu sana mkuu, utamaduni wa kusoma vitabu ni mzuri sana kwani unapata mambo mengi mno.
 
ILA MKUU, ungeviweka tu hapapa, watu wajichotee,

Humu JF watu wachache watakutumia email address zao, kwanza hawapendi kujulikana, kukutumia email address moja kwa moja ni kujiweka wazi wewe ni nani?

JF ni sehemu tunayoweka vitu bila kificho, please tunaomba weka vitabu hapa kila mtu ajichukulie atakayependa..

Kuna kipindi vitabu vimewekwa vingi humu vingi na kila mtu aliyetaka akajisomea,

Nashukuru coz utaviweka hapa.
 
kitabu cha think and grow rich kina page 235, poor dad rich dad kina page 130, the richest man in babylon 164, sasa sijui wingi wa pages unaouzungumzia hapo ni upi.
hivyo vitabu sio vyangu mimi nawashirikisha watu kwa kuwa nimevisoma na ninahamu kila mtanzania avisome, vina msaada sana.
unachonishangaza unajiita american dream wakati maisha ya tanzania tu yanakupa shida, hao wamarekani wenyewe wanatoana sana, yani waliofanikiwa wanatumia muda mwingi sana kuwafundisha wenzao njia za kufanikiwa kupitia vitabu, dvd na semina.
tukiendelea hivi watanzania kwa kupinga mambo mazuri kwa excuse za kijinga tunaelekea kubaya.
Kama unaona pages 200 na ushei ni chache ni kwasababu una culture ya kusoma vitabu but for those who r not utasubiri sana na kuhusu jina nnalotumia lisikuumize kichwa wala usihoji coz its non of ur bisnes librarian na kingine usije ukajidanganya kwa kujitapa eti unaweza kuwatoa wabongo kwa vitabu vilivyoandikwa na westerners na vilivyozingatia uchumi na mazingira yao acha kutuletea hizo pretitude andika cha kwako poor boy, am out
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom